Hesperian Health Guides

Sumu

Kwa aina nyingi za sumu: haraka punguza nguvu za sumu na kuiondoa mwilini kwa kunywa maji mengi. Kutumia dawa ya mkaa ya kunyonya sumu mwilini (activated charcoal) husaidia kunyonya sumu hiyo, ambayo baadaye huondolewa kutoka mwilini kupitia kinyesi. Kama unajua ni aina gani ya sumu, angalia kwenye chati chini kupata taarifa za kukusaidia kufanya maamuzi.

Kwa mtu mzima: Mpe gramu 50 hadi 100 za dawa ya mkaa ya kunyonya sumu.
Kwa ajili ya mtoto: Mpe gramu 1 ya dawa ya mkaa ya kunyonya sumu iliyochanganywa kwenye maji kwa kila kilo ya uzito.


Dawa ya mkaa ya kunyonya sumu ni kitulizo muhimu chenye gharama nafuu ambacho kinatakiwa kuwepo kila mara kwenye akiba yako ya dawa.

Kwa mgonjwa ambaye hawezi kupumua vizuri au ameanza kupoteza fahamu, usimpe maji, mkaa au kitu chochote kingine cha kumeza. Kumbuka: kuendelea kupumua ni muhimu daima.

Kutapika mara nyingi hakusaidii dhidi ya sumu, na kunaweza kuzidisha hatari. Mtu ambaye amemeza kemikali zenye uwezo wa kukwang’ua kama vile asidi, petroli, mafuta ya taa au mafuta ya kuyeyusha au kuchanganya rangi, au ambaye ana matatizo katika kupumua, kamwe asijaribu kuitapika sumu.

Kama atajaribu kutapika, afanye hivyo mapema kadri iwezekanavyo, ndani ya saa chache za mwanzo wa tukio. Kuchochea kutapika, chomeka kidole mdomoni na kugusa nyuma ya koo au meza chumvi kijiko kimoja kilichojaa.

Mtoto anajaribu kuifikia kabati iliyofungwa.
Weka sumu zote mahali ambapo watoto hawawezi kuzifikia.
Uzuiaji

Inawezekana kuzuia ajali za sumu. Weka onyo kwenye sumu na dawa zote. Weka mahali ambapo watoto hawawezi kuzifikia- kwenye kabati zilizofungwa na kufuli juu ukutani. Kamwe usitumie vyombo vya kuhifadhi au kubebea sumu kwa ajili ya vyakula au vinywaji hata kama vinashafishika. Vivyo hivyo, kamwe usiweke sumu kwenye chupa au vyombo ambavyo vimetengenezwa maalum kwa ajili ya vyakula au vinywaji.

Kula au kunywa sumu ni njia ambayo mara nyingi hutumika kujiua au kujidhuru. Hivyo, kuzifungia sumu, bunduki, na vifaa vingine hatari ni njia muhimu sana katika kuzuia vifo kutokana na kujiua. Kwa taarifa zaidi juu ya kumsaidia mtu ambaye anataka kujiua, angalia Afya ya akili (kinaandaliwa).

SUMU ZA KEMIKALI

Aina za kemikali
Danger.png
 Dalili za kuathirika
+
Ufanye nini
Zenye uwezo wa kukwangua au kubabua:
 • Amonia
 • Betri
 • Asidi
 • Dawa ya kusafisha mitaro
 • Magadi kali inayobabua (caustic soda)
 • Maji ya magadi kali yanayobabua (lye)
Betri na maji ya magadi kali

Asidi.
Kemikali hizi huchoma ndani ya mwili.
 • Kutokwa sana na mate.
 • Maumivu mdomoni, kooni, kifuani, tumboni, au mgongoni.
 • Kutapika.
 • Shida katika kumeza.
 • Usijaribu kutapika.
 • Dawa ya mkaa ya kunyonya sumu mwilini (activated charcoal) haitasaidia sana.
 • Mpe maji mengi kadri uwezavyo. Tafuta msaada.
Haidrokaboni:
 • Petroli na dizeli
 • Dawa ya kuchanganya au kuyeyusha rangi
 • Kilainishi
 • Mafuta ya taa
 • Fenoli (phenol)
 • Kaboliki asidi (carbolic acid)
 • Kafuri (camphor)
 • Mafuta misindano (pine oil)
Debe la petroli

Hizi ndiyo hatari zaidi kama hewa yake inavutwa na kuingia mapafuni.
 • Kupumua kwa shida.
 • Kukohoa, kukabwa, kutapika.
 • Homa.
 • Dalili zinazofanana na za kifafa na kupoteza fahamu.
 • Pumzi kutoa harufu kama ile ya sumu
 • Usijaribu kutapika.
 • Usimpe dawa ya mkaa ya kunyonya sumu mwilini.
 • Mpe maji mengi.
 • Osha kuondoa haidrokaboni kwenye ngozi na nywele na vua nguo zote zilizochafuliwa.
 • Msaidie katika kupumua kama inahitajika na angalia upumuaji wa mgonjwa angalau kwa siku 2.

Msaidie katika kupumua]] kama inahitajika na angalia upumuaji wa mgonjwa angalau kwa siku 2.

 • Tafuta msaada
Sainidi (cynide):
Hutumika katika uchimbaji madini, kazi za viwandani, kusindika ngozi za wanyama, sumu ya panya.


Inaweza kuvutwa ndani ya mwili kupitia pumzi ya kawaida au kwa njia ya mdomo kupitia chakula na maji ambavyo vimechafuliwa na sumu hiyo.

a box of rat poison.

Moto wa ndani unaweza kusababisha uvute sumu ya sainidi iliyokuwa kwenye vifaa ambavyo vinaungua. Unaweza kusikia harufu chungu kama ile ya mti uitwao mlozi kwenye moshi ambao una sainidi ndani yake.
 • Matatizo ya kupumua.
 • Maumivu ya kichwa, kuchanganyikiwa, na dalili zinazofanana na za kifafa.
 • Kunaweza kutokea madhara ya muda mrefu ambayo huharibu ubongo.
Oganofosfeti (organophosphates) na kabameti (carbamate):

Inapatikana katika baadhi ya viua wadudu vikiwemo:

 • malathion
 • parathion
Boksi la viuawadudu.

Kemikali hizi zinaweza kusimamisha kupumua au matatizo mengine yanayohusu mwili mzima.
 • Kasi ya mapigo ya moyo kupungua, udhaifu wa misuli, matatizo katika kupumua.
 • Kamasi laini, kutokwa machozi, na mate mengi mdomoni
 • Dalili zinazofanana na kifafa
 • Pumzi kutoka ndani inaweza kuwa na harufu kama ya mafuta ya gari au kitunguu saumu.
 • Matatizo yanayotishia maisha yanaweza kujitokeza siku kadhaa baada ya kula sumu hii na madhara ya neva ya muda mrefu yanaweza kutokea wiki kadhaa baada ya tukio.
 • Angalia iwapo kuna matatizo katika kupumua na toa pumziya kuokoa maisha kama inahitajika.
 • Dawa ya Atropini (atropine) husaidia kupambana na sumu.
 • Mpe dawa ya mkaa ya kunyonya sumu mwilini kama haijapita saa1 tangu ale sumu hiyo.
 • Osha ngozi ya mwili mara moja na ondoa na kutupa nguo zote zilizochafuliwa.
 • Tibu dalili zinazofanana na kifafa kwa kutumia diazipamu (diazepam).
Dawa za sumu za kudhibiti magugu (herbicides):
 • Parakati (paraquat) Gramoxon, Cyclone, Herbikill, Dextron, na majina mengi ya kibiashara)
 • Glaifoseti
  (glyphosate) Roundup, Touchdown, na majina mengine kibiashara)
aMwanaume akinyunyizia viuawadudu uwanjan

Vinaweza kuingia mwilini kupitia ngozi, wakati wa kupumua,au kwa njia hatari zaidi kuliko zote-kumezwa.
 • Matatizo ya kupumua (yanaweza kutokea baada ya siku kadhaa).
 • Maumivu mdomoni.
 • Mkojo mwekundu, wa rangi ya udongo, au kupata mkojo kidogo au kutopata mkojo kabisa (dalili ya figo kuanza kushindwa kufanya kazi — hii ni hatari).
 • kikubwa kinaweza kusababisha majeraha ya kuungua mdomoni na kooni, maumivu tumboni, na matatizo katika kupumua.
 • Angalia kama kuna matatizo katika kupumua na toa pumziya kuokoa maisha kama inahitajika.
 • Mpe dawa ya mkaa ya kunyonya sumu mwilini.
 • Tafuta msaada.

SUMU AMBAZO ZINATOKANA NA DAWA ZA TIBA NA MADAWA MENGINE


Aina ya Dawa
Danger.png
 Dalili ya uzidisha kiasi cha dawa
+
Utafanya nini
Madini chuma:
 • Ferasi salfeti(ferrous sulfate)
 • Ferasi glukoneti (ferrous gluconate)
 • Vitamini zinazotolewa kabla mtoto kuzaliwa (prenatal vitamins)
 • Vitaminimseto (multivitamins) au sirapu
chupa ya vidonge vya madini chuma.

Kuzidisha dawa kuliko kiasi kinachohitajika huharibu tumbo na matumbo
 • Maumivu, kutapika au matapishi yaliyochanganyika na damu, kuhara, kuchanganyikiwa.
 • Mshituko baada ya tukio au siku kadhaa baadaye.
 • Kutapika mara baada ya tukio huweza kusaidia
 • Mpe maji mengi.
 • Dawa ya mkaa ya kunyonya sumu mwilini haisaidii
 • Deferoksamini (deferoxamine) ni dawa ya kupambana na madhara ya sumu.
 • Angalia iwapo kuna matatizo katika kupumua.
Parasetamo
 • Asetaminofeni (acetaminophen- Panadol, Tylenol, Crocin, na majina mengine ya kibiashara)
 • Dawa mseto baridi nyingi na dawa za kupunguza maumivu (soma taarifa kwenye ganda)
NWTND fa Page 47-2.png

Kuzidisha kiasi cha dawa kuliko kinachohitajika ni sumu kwa ini lako.
 • Kichefuchefu, kutokwa na jasho, ngozi kupauka, uchovu.
 • Baadaye huenda kukawa na maumivu ya ini (tumboni sehemu ya juu upande wa kulia), homa ya nyongo ya manjano, kuchanganyikiwa, au mkojo uliochanganyika na damu.
 • Kama unaweza kumfanya mtu atapike mara baada ya tukio huenda ikasaidia.
 • Mpe dawa ya mkaa ya kunyonya sumu mwilini na maji mengi.
 • Asetisaisteni (acetylcysteine) ni dawa ya kupambana na sumu mwilini.
Dawa za kulevya:
 • Mofini (morphine)
 • Heroini
 • Methadoni (methadone)
 • Bangi
 • Oksikodoni (oxycodone)
 • Madawa mengine yenye nguvu ya kupunguza maumivu
Kuzidisha kiasi cha dawa kuliko kinachohitajika kunaweza kusababisha upumuaji kusimama
 • Kufikiri polepole, kuitikia polepole, kupumua polepole, pumzi fupi, au upumuaji kusimama.
Pombe:
NWTND fa Page 47-3.png
Kutumia dawa nyingi kuliko kiasi kinachohitajika kunaweza kusababisha pumzi kusimama.
 • Kutapika.
 • Kuchanganyikiwa.
 • Dalili zinazofanana na za kifafa
 • Kupumua polepole au kasi ya upumuaji kupanda na kushuka.
 • Kupoteza fahamu. Kuchanganyikiwa, mabadiliko katika uwezo wa kufikiri na utambuzi, upumuaji usiyo wa kawaida, na hisia au kuonekana mgonjwa zinaweza kuwa dalili za tatizo la kisukari ambazo zinapaswa kushughulikiwa mara moja.
 • Fuatilia upumuaji wa mgonjwa na toa pumzi ya kuokoa maisha kama inahitajika.
 • Mgeuze upande kuzuia kukabwa kama atatapika.
 • Mpatie joto la kutosha.
 • Kama anaweza kunywa, mpe kinywaji maalum cha kumuongezea maji mwilini.