Hesperian Health Guides
Tetanasi (pepopunda)
Yaliyomo
Katika sura hii:
- Huduma ya kwanza
- Weka utulivu na kudhibiti dharura
- Kupoteza fahamu (kuzirai)
- Kupumua
- Pasipo mapigo ya moyo
- Kutokwa damu
- Mshituko
- Vidonda
- Vidonda ambavyo vimeingia ndani
- Maambukizi
- Ueneaji wa sumu ya vimelea kwenye damu (sepsisi)
- Tetanasi (pepopunda)
- Majeraha ya uti wa mgongo na shingo
- Majeraha ya kichwa
- Vidonda kwenye kifua na mbavu ambazo zimevunjika
- Majeraha na vidonda kwenye tumbo
- Mshituko wa moyo
- Mifupa iliyovunjika, kutenguka, na misuli au tishu zilizoumia
- Kuvia damu kutokana na majeraha chini ya ngozi
- Ubakaji
- Majeraha ya moto
- Kupigwa na umeme
- Kuunguzwa na kemikali
- Silaha za kipolisi
- Dharura zinazohusu afya ya akili
- Sumu
- Dharura zinazohusiana na ugonjwa wa kisukari
- Shambulio linalofanana la kifafa (seizures), mtukutiko wa maungo (convulsions)
- Kuumwa au kung'atwa na wadudu au viumbe wengine
- Mzio: Mzio mdogo au mzio mkali
- Dharura kutokana na joto kali
- Dharura kutokana na baridi kali
- Madawa
Tetanasi ni ambukizo hatari ambalo huingia kwenye kidonda au kiungamwana, na baadae kusambaa mwili mzima.

Dalili
- Kutokwa na jasho kusiko kwa kawaida.
- Mapigo ya moyo kwenda haraka.
- Misuli kukakamaa na kuuma.
- Wakati wa mikakamao ya misuli, upumuaji unaweza kusimama.
- Kukaza au kubana kwa misuli unaokuja na kuachia.
- Mdomo hauwezi kufunguka kwa urahisi.
- Shingo kukakamaa, tumbo kukaza kama ubao.
Tafuta msaada wa kitabibu haraka kwa ajili ya dalili hizi!
Uzuiaji
Ni rahisi kuzuia tetanasi kuliko kuitibu. Njia bora zaidi ni chanjo na matunzo mazuri ya kidonda. Kwa ajili ya ratiba ya chanjo, angalia Chanjo (kinaandaliwa).
Vidonda ambavyo ni rahisi kuambukizwa na tetanasi
- Vidonda ambavyo vinatokana na kutobolewa na vitu vikali.
- Vidonda vya risasi.
- Mifupa iliyovunjika, hasa inapojitokeza nje ya ngozi.

- Vidonda vikubwa vya moto au kutokana na ugonjwa wa kuganda tishu kutokana na barafu.
- Utoaji mimba kwa njia zisizo salama na kuchoma sindano au utoboaji, au kuchanja kwa kutumia sindano na vifaa ambavyo tayari vimetumika, na havijatakaswa.
![]() |
![]() Zamu yangu. |
![]() |
![]() |
Safisha vidonda hivi vizuri na kutoa dawa dhidi ya tetanasi (antitetanus immunoglobulin) kama ratiba yake ya chanjo ya tetanasi iko nyuma.
Pia mpe metronidazo (metronidazole).
Tetanasi miongoni mwa watoto wachanga
Watoto wachanga huambukizwa tetanasi kupitia kiungamwana au kitovu. Unaweza kumkinga mtoto mchanga kwa kukata kiungamwana kwa kutumia wembe uliochemshwa kwenye maji, kutunza usafi wa kitovu, na kumchanja mama mjamzito. Angalia Chanjo (kinaandaliwa).