Hesperian Health Guides
Maambukizi
Katika sura hii:
- Huduma ya kwanza
- Weka utulivu na kudhibiti dharura
- Kupoteza fahamu (kuzirai)
- Kupumua
- Pasipo mapigo ya moyo
- Kutokwa damu
- Mshituko
- Vidonda
- Vidonda ambavyo vimeingia ndani
- Maambukizi
- Ueneaji wa sumu ya vimelea kwenye damu (sepsisi)
- Tetanasi (pepopunda)
- Majeraha ya uti wa mgongo na shingo
- Majeraha ya kichwa
- Vidonda kwenye kifua na mbavu ambazo zimevunjika
- Majeraha na vidonda kwenye tumbo
- Mshituko wa moyo
- Mifupa iliyovunjika, kutenguka, na misuli au tishu zilizoumia
- Kuvia damu kutokana na majeraha chini ya ngozi
- Ubakaji
- Majeraha ya moto
- Kupigwa na umeme
- Kuunguzwa na kemikali
- Silaha za kipolisi
- Dharura zinazohusu afya ya akili
- Sumu
- Dharura zinazohusiana na ugonjwa wa kisukari
- Shambulio linalofanana la kifafa (seizures), mtukutiko wa maungo (convulsions)
- Kuumwa au kung'atwa na wadudu au viumbe wengine
- Mzio: Mzio mdogo au mzio mkali
- Dharura kutokana na joto kali
- Dharura kutokana na baridi kali
- Madawa
Kidonda chochote kinaweza kupata maambukizi.
Dalili za maambukizi
Kidonda kitakuwa kimeambukizwa iwapo kutatokea:
- kuvimba, kugeuka chekundu na kupata moto
- kutunga usaha
- kutoa harufu mbaya
Maambukizi yatakuwa yanaenea sehemu zingine za mwili iwapo itatokea:
- homa
- tezi za limfu au mitoki kuvimba na kuanza kuuma kwa ndani
Tezi za limfu —ambazo mara nyingi huitwa mitoki— ni mitego midogo kwa ajili ya vijidudu vinavyosababisha magonjwa ambavyo hujenga uvimbe mdogo chini ya ngozi ya mwili panapotokea maambukizi. Kuvimba matezi au mtoki humaanisha maambukizi yameingia.
![]() Chini ya taya humaanisha maambukizi ya meno au kooni.
Nyuma ya sikio humaanisha maambukizi kichwani au kwenye ngozi ya kichwa na nywele zake, mara nyingi yanayosababishwa na vidonda kwenye ngozi au chawa. Au surua ya rubella inaweza kuwa chanzo.
Chini ya sikio na shingoni humaanisha maambukizi ya sikio,usoni,au kichwani. Au inaweza kuwa kifua kikuu.
Mitoki kwapani, humaanisha maambukizi kwenye mkono, kichwani, au ziwani. Au wakati mwingine saratani ya ziwa (angalia Saratani).
Mitoki kwenye nyonga humaanisha maambukizi kwenye mguu, kikanyagio, ukeeni au umeeni, au unyeo. |
Matibabu ya maambukizi
Safisha vizuri kidonda. Inaweza kuhitaji kutoboa au kupasua jipu au kuondoa nyuzi. Kwa taarifa zaidi juu ya majipu angalia Matatizo ya ngozi (kinaandaliwa). Isipokuwa tu kama eneo ambalo limeambukizwa ni dogo na linapata nafuu haraka, kawaida ni bora zaidi kumpa dawa ya antibiotiki. Mpe dikloksasilini (dicloxacillin), sefaleksini (cephalexin), AU klindamaisini (clindamycin). Kama kidonda kimeingia sana ndani, mpe chanjo ya tetanasi (angalia Chanjo – kinaandaliwa) na tetanus immunoglobulin.
Kama maambukizi hayapungui, yanaweza kueneza sumu kwenye damu (sepsisi).