Hesperian Health Guides

Dharura zinazohusu afya ya akili

Katika sura hii:

Mabadiliko ya ghafla katika kufikiri, tabia, kupata ndoto za jinamizi na kuchanganyikiwa sana vinaweza kumtishia sana mtu anayeipitia hali hiyo, na wale wanaomzunguka. Sura inayohusu Afya ya akili (inaandaliwa) ina taarifa zaidi juu ya afya ya akili, tofauti katika kufikiri, na hali halisi ya akili ya mtu.

Pale ambapo fikra na mtazamo wa mtu vinaposababisha mawazo ya kutaka kujiumiza mwenyewe na wengine, inakuwa dharura ambayo inahitaji msaada haraka. Kama ilivyo kwa dharura zingine, kwanza chunguza hali yake ya kupumua, simamisha uvujaji damu,na angalia kama kuna majeraha mengine ya kimwili. Halafu kumtia moyo mtu mwenye tatizo la kiakili, kumtuliza na kumsaidia kujisikia vizuri vinaweza kunusuru maisha.

Kama mtu mwingine atasema anataka kujiumiza au kuwaumiza wengine, unapaswa kumuamini.

Kama mtu mmoja ni hatari kwa watu wengine, mara nyingi inakuwa rahisi zaidi kuwaondoa watu wengine mbali naye kuliko kumuondoa yeye. Unaweza kuhitaji msaada kumweka salama pamoja na eneo linalomzunguka. Pia chukua tahadhari kuhusu usalama wako.

Wanaume 2 wakiongea; mmoja amekaa chini, kichwa chake kikiwa katikati ya mikono yake.
Unaonekana kuna kitu kinakutatiza.
Nimeteseka vya kutosha.

Kama anasema anataka kujiumiza au kujiua, kitu cha kwanza anachohitaji ni kumsikiliza kwa upole. Muulize maswali kwa upendo, kuonesha unajali na upate fursa ya kuelewa hali yake kwa uhakika. Maswali yako yanaweza kusaidia pia kuvuruga mawazo yake na kumuondoa kwenye kile alichokuwa anakusudia.

  1. Muulize kama anapanga kujiumiza yeye au mtu mwingine, au kama tayari amekwisha fanya hivyo.
  2. Wanaume 2 wakiendelea kuongea
    Kweli unafikiri unaweza kujiua?
    Huwa nafikiria jambo hilo muda wote! Na sasa nakwenda kulitekeleza!
  3. Uliza jinsi anavyopanga kulitekeleza, na kama anazo njia za kulitekeleza. Kadri mpango utakapoonekana bayana, ndivyo ulivyo ukubwa wa tatizo.
  4. NWTND fa Page 43-2.png
    Utalitekelezaje?
    Nina bunduki. Nitalifanya watoto watakapokwenda shuleni.
  5. Mwombe mwathirika aahidi kuwa hatajiumiza wala kuwaumiza wengine. Ondoa nyenzo ambayo angetumia kujidhuru na kuwadhuru wengine.
NWTND fa Page 43-3.png
Unaweza kuahidi kwamba hutajidhuru leo?
Huenda kwa leo tu.
NWTND fa Page 43-4.png
Unaweza kuniruhusu nikutunzie silaha yako — angalau kwa leo tu?

Kufikia makubaliano kama haya kunaweza kumweka mwathirika salama kwa muda wa kutosha kabla msaada zaidi wenye manufaa ya muda mrefu kupatikana. Usimwache peke yake. Kaa naye, au wahimize baadhi ya wanafamilia kukaa naye. Hakikisha anabaki mtulivu — asitumie pombe au madawa ya kulevya. Pombe na madawa ya kulevya vinaweza kuathiri maamuzi yake na kujenga mazingira yanayorahihisha kujidhuru. Msaada kutoka kwa kiongozi wa kiroho au mwanajamii ambaye anamuamini au kumheshimuni muhimu. Pia fuatilia kuhakikisha kuwa anaendelea kupata msaada, na kuonesha kuwa unamjali. Angalia sura kuhusu Afya ya akili (inaandaliwa) kwa taarifa zaidi juu ya namna ya kutoa misaada endelevu.

Kumuuliza mtu iwapo anataka kujiua hakuimarishi uwezekano wake wa kujiua.