Hesperian Health Guides

Kuunguzwa na kemikali

Katika sura hii:

Sw NWTND fa Page 40-1.png

Jikinge kwanza: Vaa vazi lenye mikono mirefu na glovu juu ya mikono yako. Funika mdomo wako na kitambaa. Nawa vizuri na kufua nguo zako kikamilifu baada ya kumsaidia mtu yeyote ambaye amechafuliwa au kufikiwa na kemikali.

Njia bora zaidi ya kuzuia madhara kutokana na kuunguzwa na kemikali ni kuondoa kemikali husika haraka iwezekanavyo.

  1. Ondoa nguo na vito karibu na jeraha.
  2. Kama kemikali inanata, haraka kwangua kwa kutumia kijiti au kitu chochote imara ambacho ni bapa.
  3. Mara baada ya kuondoa kemikali yote ambayo unaweza, suuza eneo hilo na maji mengi sana. Maji yanaweza kusababisha baadhi ya kemikali kuanza kuungua. Hivyo hakikisha kuwa unaondoa kiasi kikubwa cha kemikali kadri uwezavyo. Kwa kemikali yenye mafuta, tumia sabuni na maji. Tumia mpira au bomba. Kama uso umedhurika, osha vizuri kwanza. Hasa safisha michaniko au sehemu zote za uwazi kwenye ngozi. Kadri utakavyowahi kunawa na kutumia muda mfupi kunawa ndivyo utakuwa katika nafasi bora zaidi kunusuru ngozi yako.


Baada ya kuosha kemikali yote kutoka kwenye mwili wa mtu aliyedhurika, tibu sehemu iliyounguzwa na kemikali kama jinsi unavyotibu vidonda vingine vya moto.

Osha au tupa nguo zozote ambazo zimeguswa na kemikali, kwani zinaweza kusababisha madhara.

NWTND fa Page 40-2.png
Kama kemikali zitaingia machoni, tiririsha maji kwenye jicho ukianzia ndani ya jicho (karibu na pua) kuelekea nje ya jicho (karibu na sikio).