Hesperian Health Guides
Huduma ya kwanza
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Huduma ya kwanza
Weka utulivu na kudhibiti dharura
Jikinge kwanzaJitahidi kuepuka kugusana na damu na majimaji yanayotoka mwilini unapokuwa unawahudumia watu wanaovuja damu.
|
Dharura au ajali inapotokea, kukabiliana na dharura hiyo hatua kwa hatua kunaweza kukusaidia kufikiri vizuri na kuyashughulikia matatizo muhimu kwanza.
1. Chukua pumzi nzito. Dharura au ajali zinaweza kutisha sana. Lakini kadri unapokuwa mtulivu, ndivyo utakavyoweza kutoa msaada zaidi. Utulivu wako utawapa moyo na kuwasaidia majeruhi na wengine wanaokuzunguka. |
2. Jiulize: hii sehemu ni salama? Mweke mgonjwa na wewe mwenyewe mbali na moto, sehemu zenye shughuli nyingi, na hatari zingine. (Kama mgonjwa amejeruhiwa shingoni au mgongoni, mwondoe kwa uangalifu ili usitikishe shingo.) |
3. Shughulikia kwanza matatizo ambayo ni hatari zaidi. Bila kuzingatia sababu ya jeraha, haraka chunguza jinsi anavyopumua. Kupumua ni muhimu zaidi kwa ajili ya uhai. Angalia kama anapumua kwa shida. |
4. Baada ya kupumua, chunguza uvujaji damu. Kupoteza damu nyingi kunaweza kusababisha mauti. |
5. Mtu anapokua anapumua na uvujaji mkubwa wa damu ukiwa umedhibitiwa, chunguza mwili mzima kwa ajili ya majeraha na mifupa iliyovunjika. Anzia kichwani na kuchunguza kila sehemu ya mwili, mbele na nyuma, hadi chini kwenye vidole miguuni. Kwa upole uliza maswali, mwangalie mgonjwa mwili mzima, na kwa uangalifu kushika na kukagua mwili wake kujua iwapo kuna majeraha yaliyojificha. Ni kawaida kuwa na jeraha zaidi ya moja, na baadhi ya majeraha hayawezi kubainishwa kwa kutazama mara moja tu. |
6. Jitahidi kuwa mpole na kumfariji kadri uwezavyo. Mtu aliyejeruhiwa anaweza kuwa amepata mshituko na ana maumivu. Kwa kumtuliza, unaweza kusaidia kuboresha upumuaji wake na mapigo ya moyo kurudi katika hali ya kawaida. |
Chunguza tena upumuaji na uvujaji damu mara kwa mara. Kama unaweza kupima shinikizo la damu, pima mara kwa mara. Mtu aliyejeruhiwa mwanzoni anaweza kuonekana mwenye hali nzuri na baadaye hali ikabadilika ghafla kuwa mbaya. Chunguza dalili hizi muhimu za uhai kila baada ya muda hadi utakapokuwa na uhakika kwamba yu salama. Endelea kuongea naye. Hii itakusaidia kuona iwapo amechanganyikiwa au hali hiyo ya kuchanganyikiwa inazidi kuwa mbaya.
Watu ambao kawaida hukusanyika pale ajali inapotokea wanapaswa kuhimizwa kusaidia. Waombe kwa sauti ya juu kutengeneza nafasi ya kutosha ili uweze kumhudumia majeruhi. Mwombe mojawapo kutafuta msaada zaidi au mahitaji muhimu kama vile misaada ya kitabibu, vitambaa (kwa ajili ya bandeji) au blanketi. Mpe kila mmoja jukumu la kusaidia kuimarisha utulivu na kuhakikisha hatua zote muhimu na za haraka zinachukuliwa. Kama watu wengi wamejeruhiwa, soma Maafa na uhamaji wa ghafla wa kulazimishwa (kinaandaliwa) kuhusu jinsi ya kuamua nani wakumuhudumia kwanza.
Mtu aliyejeruhiwa pia anaweza kujihudumia. Watu wengi wanaovuja damu wanaweza kuweka shinikizo au mgandamizo juu ya majeraha yao ili kupunguza uvujaji damu. Hii pia inaweza kuhamisa mawazo ya majeruhi kwa jambo hilo na kukuruhusu kuchunguza na kushughulikia majeraha mengine au majeruhi wengine.
? | Muulize iwapo ana maumivu, anahisi mwili kufa ganzi, au matatizo katika kutembea. | Hizi ni dalili za kutenguka au mifupa iliyovunjika. Angalia taarifa juu ya mbavu zilizovunjika na mifupa iliyovunjika. Kama anahisi sehemu hiyo kufa ganzi au ugumu katika kutembeza sehemu ya chini ya mwili au mwili mzima, huenda kuna jeraha la uti wa mgongo. | |
Muulize au chunguza iwapo anapumua kwa shida, au iwapo ana dalili ya kukabwa. | Maumivu ya kuchoma anapokua anapumua yanaweza kuwa dalili ya ubavu uliovunjika. | ||
Kupumua haraka haraka, kifua kubana, na kupumua na sauti inayofanana ya filimbi au inayokoroma ni dalili za pumu (angalia Matatizo katika kupumua na kukohoa - kinaandaliwa). | |||
Matatizo katika kupumua yanaweza kusababishwa na madhara ya sumu ya kemikali au kuzidisha dozi ya dawa. | |||
Chunguza iwapo anaonekana kuchanganyikiwa au kupata matatizo katika kuongea vizuri. Hii inaweza kukusaidia kutathmini kwa kiwango gani amejeruhiwa. Angalia utafanya nini iwapo mtu amepoteza fahamu. | Watu wengi huchanganyikiwa baada ya ajali. Lakini kutoongea vizuri, kupoteza fahamu, na kuchanganyikiwa kabisa zinaweza kuwa dalili za jeraha kichwani au ulevi wa madawa au pombe. | ||
Kuongea kwa kukokoteza maneno au sauti au uongeaji usio wa kawaida inaweza kuwa dalili ya kiharusi. Je upande mmoja wa uso unainama au unaonekana kuwa dhaifu? Angalia Matatizo ya kichwa na ubongo (kinaandaliwa). | |||
Kuchanganyikiwa au mabadiliko katika utambuzi inaweza kuwa dalili ya dharura inayohusiana na ugonjwa wa Kisukari. Angalia jinsi ya kufanya kama mtu ataanza kuumwa ghafla. | |||
? | Tazama kwa makini: Je kuna uvujaji damu, uvimbe, michubuko, wekundu kwenye ngozi, au viungo vya mwili kutoka katika muonekano wake wa kawaida? Linganisha upande mmoja wa mwili na mwingine.Kwa mfano, kama mguu mmoja unaonekana kuwa mfupi kuliko mwingine, unaweza kuwa umevunjika. | Angalia jinsi ya kufanya kwa ajili ya uvujaji damu. | |
Kwa ajili ya mifupa iliyovunjika, angalia taarifa juu ya mbavu zilizovunjika na mifupa iliyovunjika. | |||
Kuchubuka, kuvimba na wekundu zinaweza kuwa dalili za uvujaji damu ndani ya mwili. Angalia iwapo kuna hali ya mshituko. |
? | Gusa polepole eneo la kichwa, uso, shingo, mgongo, sehemu ya mbele, kwenye mikono na miguu. Je kuna maumivu, hisia ya kufa ganzi, au mifupa kutoka sehemu zake? Kama upo uwezekano wa majeraha mgongoni au shingoni, gusa kila kiungio cha uti wa mgongo kuanzia kichwani hadi kwenye sehemu kati ya makalio. | Angalia nini cha kufanya juu ya dalili za majeraha kichwani. | |
Angalia nini cha kufanya kama unahisi uwepo wa jeraha kichwani, shingoni, au mgongoni kabla ya kumuondoa majeruhi. |