Hesperian Health Guides

Dharura kutokana na joto kali

Katika sura hii:

Madhara kutokana na joto kali – mkakamao, kupungukiwa sana nguvu, na kuugua

NWTND fa Page 55-2.png

Kufanya kazi sana katika mazingira ya joto kali kunaweza kusababisha mkakamao (cramps) wenye maumivu miguuni, mikononi, au tumboni. Hii inaweza kutokana na kupoteza kiasi kikubwa cha chumvi kupitia jasho.

Dalili

Kuzidiwa na joto kali (ugonjwa wa joto) husababisha:

  • Kiu kali.
  • Udhaifu.
  • Maumivu ya kichwa.
  • Kichefuchefu au mkakamao tumboni.
  • Ngozi kawaida inakuwa inatoa kijasho na inaweza kuwa baridi na imepauka.
  • Hisia za vitu kuchomachoma kwenye ngozi na upele.
Sw NWTND fa Page 55-3.png
Matibabu
  • Pumzika sehemu yenye ubaridi. Vua nguo za ziada.
  • Mpe vinywaji vya kuongeza maji mwilini — changanya chumvi nusu kijiko cha chai katika lita 1 ya maji.
  • Mpe pia vinywaji vingine vingi ambavyo vimepoa.
  • Taratibu nyoosha mikakamao, chezesha miguu, au tembea polepole.

Kama mtu hatatibiwa, kuzidiwa na joto kunaweza kusababisha hali mbaya zaidi ya mshituko wa moyo.

Mshituko wa moyo kutokana na joto kali

Mshituko kutokana na joto kali ni hali ya hatari ambayo inatokana na kukaa katika joto kali kwa muda mrefu. Ukiachwa bila kutibiwa, mshituko huo una uwezo wa kuua.

Dalili
  • Mapigo ya moyo kuenda haraka na kupumua haraka
  • Ngozi ya mwili inavia na kuwa na wekundu, enye joto, kavu au inanata
  • Kutapika na kuharisha
  • Kuchanganyikiwa
  • Kuzirai au mashambulio yanayofanana na ya kifafa
  • Homa kali, zaidi ya nyuzijoto 40° sentigredi
Mwanamke mnene amekamata pepeo akionekana kutojisikia vizuri.
Mwanaume mwenye umri wa kati akitokwa jasho wakati akifanya kazi nje.
Mshituko wa moyo kutokana na joto kali hutokea kwa watu ambao hawana uwezo wa kustahimili joto kali: wazee, watoto wachanga, wagonjwa, watu wanene sana, na watumiaji sana wa pombe wako katika hatari kubwa zaidi. Mshituko wa moyo kutokana na joto kali unaweza pia kumpata kijana mwenye afya ambaye amefanya kazi au mazoezi muda mrefu kwenye joto kali bila kupumzika. Watu hao kawaida hutokwa na kijasho badala ya kuwa na ngozi kavu.


Matibabu

Mpoze haraka iwezekanavyo: mweke kwenye kivuli. Vua nguo za ziada. Mpepee na kumpangusa mwili mzima kwa nguo zenye ubaridi zilizoloweshwa. Weka vipande by barafu au nguo baridi kwenye shingo, kwapani, na kuzunguka kinena. Kama ni mtu mwenye afya, anaweza kuchovywa kwenye bafu ya maji baridi kama barafu, lakini hii ni hatari kwa mtu mwenye umri mkubwa au ambaye tayari ni mgonjwa.

Mtu anapokua timamu, mpe kinywaji cha kumuongezea maji mwilini. Au mpe kinywaji chochote baridi kwa wingi. Lakini chukua tahadhari asikabwe: matatizo ya kupumua hujitokeza sana kuhusiana na mshituko.

Hali ya mtu ambaye amepata mshituko wa moyo kutokana na joto kali inaweza kuzidi kuwa mbaya haraka. Hivyo ni bora zaidi kutafuta msaada wa kitabibu haraka.

Uzuiaji

Ili kuzuia matatizo yanayohusiana na joto kali unapokua nje, vaa nguo zenye rangi nyeupe –nyeupe zinazoweza kukengeusha joto na pia funika uso na nyuma ya shingo na kofia. Sehemu za kazi ndani ya majengo zinapaswa kuwa na mzunguko mzuri wa hewa na feni. Weka utaratibu wa kujipumzisha na kuny wa viny waji baridi mara kwa mara. Chukua tahadhari na uny waji wa bia au pombe baridi unapokuwa unafanya kazi, au kucheza kwenye mazingira ya joto. Pombe husababisha upungufu wa maji mwilini.

Mbabuko kutokana na jua kali

Matatizo yanayohusiana na mbabuko kutokana na jua kali (sun burns) kawaida huwa mabaya zaidi kwa watu wenye rangi kama ya wazungu. Ngozi hugeuka nyekundu, inauma sana, na ya moto. Katika hali mbaya zaidi, ngozi huota malengelenge na kuvimba. Malengelenge kutokana na mbabuko wa juakali yanaweza kupata maambukizi kwa urahisi. Mbabuko wa mara moja siyo hatari, lakini mibabuko mingi na kwa muda mrefu inaweza kusababisha saratani ya ngozi.

NWTND fa Page 57-1.png

Mbabuko kutokana na jua kali hupona bila dawa baada ya siku kadhaa. Alovera au dawa za kawaida za kupunguza maumivu zinaweza kusaidia. Huenda kuna tiba za asili katika eneo lako ambazo hupoza na kuipa ngozi unafuu.

Uzuiaji

Vaa kofia na nguo zinazofunika ngozi jua linapokua kali. Mafuta ya kukinga ngozi kutokana na mionzi ya jua, yakipakwa kwenye ngozi kabla ya kwenda kwenye jua yanaweza kusaidia kuzuia mbabuko.