Hesperian Health Guides

Mzio: Mzio mdogo au mzio mkali

Katika sura hii:

Mzio mdogo husababishwa na vumbi, chavua, kuumwa na wadudu, au baadhi ya vyakula, kemikali au dawa. Mzio wa aina hii hutibiwa kwa kutumia dawa za antihistamini (antihistamines).

Dalili za mzio mdogo
Mtu anakabiliana na madhara ya mzio mdogo.
Macho kuwasha, kuvimba na kuwa mekundu
Upele au wekundu
Chafya
Vimbe kadhaa kwenye miguu kutokana na kuumwa na viumbe fulani.
Kama ameumwa na mdudu, unaweza kuvimba

Mzio mkali ni hatari zaidi na unaweza kusababisha haraka mtu kuacha kupumua.

Dalili za mzio mkali

  • Wekundu usoni, mwasho, au upele
  • Kuvimba midomo, kinywa, au kooni, kumeza kwa shida
  • Kupumua kwa shida
  • Mikono au miguu kuvimba
  • Kichefuchefu au maumivu ya tumbo


Dalili zinazojitokeza sana ni upele na matatizo ya kupumua.

Kama mgonjwa hawezi kumeza, au anapata shida kupumua, mpe sindano ya epinefrini (epinephrine) mara moja. Choma miligramu 0.3 hadi 0.5. Unaweza kurudia dozi hiyo baada ya dakika 5 ikibidi.

Epinefrini huja katika nguvu na vipimo tofauti. Piga hesabu ya kiasi sahihi cha dawa kinachohitajika na kuwa nayo kwenye kabrasha lako la dawa kabla dharura hazijatokea. Au kaa na sindano ambayo tayari imejazwa dawa inayoitwa EpiPen au kama inavyojulikana kwa majina mengine ya kibiashara.

Choma sindano ya epinefrini kwenye msuli wa paja:

mshale ukionesha sehemu ya nje kwenye paja la mwanamke ambaye ameinua juu miguu yake kwa kutumia mito kadhaa.
Inua miguu iwe juu ya usawa wa moyo

Kwa matatizo ya kupumua unaweza kumpa salbutamo (salbutamol). Ni bora pia kumpa dawa ya antihistamini (antihistamine).

Katika matukio mengi, kama utapata mzio kutokana na dawa fulani, chakula, shambulio la nyuki, au kitu kingine, unapaswa kuepuka kitu hicho kabisa. Ukikumbana na kitu hicho tena, tarajia kupata madhara makubwa zaidi.