Hesperian Health Guides

Silaha za kipolisi

Katika sura hii:

NWTND fa Page 41-1.png

Kuwa mwangalifu: watu wanaowahudumia waathirika wa operesheni za kipolisi za kutumia nguvu mara nyingi nao hujikuta wanalengwa. Jaribu kumtoa majeruhi na wewe mwenyewe kwenye matukio ya hatari haraka.

Vinyunyizio vya gesi zenye pilipili na bomu za gesi ya machozi

Kama unaweza jiondoe sehemu mabomu ya gesi ya machozi na vinyunyizio vyenye pilipili vinatumika. Madhara yatapungua. Gesi kutokana na mabomu ya machozi hupungua haraka, wakati manyunyu yenye pilipili huweza kudumu kwa saa moja au zaidi.

Usiguse makombora ya gesi ya machozi na mikono yako. Ni ya moto na yanaweza kukuunguza kama utayaokota hivi hivi.

Kitambaa kilicholowekwa kwenye maji au siki (vinegar) kikifungwa juu ya pua hutoa kinga kidogo.

NWTND fa Page 41-2.png
  1. Angalia jinsi anavyopumua. Vinyunyizio vyenye pilipili vinaweza kusababisha matatizo makubwa katika kupumua, hususan kwa watu wenye pumu. Hii inaweza kutishia maisha. Msaidie mwathirika kupata utulivu.
  2. Tiririsha maji mengi machoni kuanzia ndani (karibu na pua) kuelekea nje ya jicho.
  3. Ondoa nguo zilizofikiwa na manyunyu hayo mara utakapokua sehemu salama na hupo katika hatari ya kufikiwa tena na kemikali hizo.
  4. Osha ngozi, sehemu moja kwa wakati, (au subiri hadi rasharasha itakapotoweka): loweka kitambaa kwenye mafuta ya kupikia chakula. Pangusa sehemu moja ya ngozi kwa kutumia kitambaa hiki chenye mafuta. Baada ya hapo ondoa mafuta hayo haraka kwa kutumia kitambaa kingine kilicholowekwa kwenye spiriti au dawa nyingine inayotokana na sukari au vitu vyenye sukari vilivyochacha (alikoholi). Kama mafuta yatabaki kwenye ngozi kwa zaidi ya dakika 30, yatachanganyika na kemikali na hatimaye kuunguza ngozi. Kama huna mafuta na spiriti, ni bora kutumia maji mengi tu. Au subiri tu. Baada ya muda, maumivu yatatoweka.


Jinsi ya kusafisha jicho na mdomo kupunguza madhara ya vinyunyizio vyenye pilipili

Changaya kwenye chupa ndogo ½ maji, ½ kimiminika chenye kupambana na asidi kilichotengenezwa kutokana na alminiamu au magnesiamu, (kama vile Maalox).

Kwa ajili ya macho, fungua wazi jicho la mwathirika na kutiririsha majimaji hayo kutoka ndani (karibu na pua) kulekea nje ya jicho (karibu na sikio).

Kwa ajili ya mdomo, mwambie mwathirika kusukutua na kutema nje.

Mchanganyiko huu unaweza pia kusaidia kusafisha manyunyu ya pilipili kutoka kwenye ngozi.

Silaha zingine za kipolisi

Risasi za mpira, bomu za gesi za kutoa machozi, magari ya kurusha maji, na virungu vyote hutumika na kusababisha damu kutoka, mifupa kuvunjika, au majeraha au uvujaji wa damu ndani ya mwili. Majeraha kwenye macho na kichwani yanaweza kuhatarisha maisha. Mchunguze mwathirika kuanzia kichwa hadi kidole. Chunguza iwapo kuna dalili za mshituko: kujisikia kuzirai, ngozi kupauka, au kukosa nguvu. Angalia Sura inayohusu Matatizo ya macho (inaandaliwa) kuhusu majeraha ya macho.