Hesperian Health Guides

Kupumua

Katika sura hii:

Kukabwa

NWTND fa Page 4-1.png

Mtu alieyekabwa ambaye hawezi kukohoa au hawezi kuongea pia hawezi kupumua. Unaweza kuponya maisha yake kwa kumsaidia haraka.

Kama mtu anaweza kukohoa au kuongea, basi anaweza kupumua.



Mpige makofi mgongoni
Mwinamishe kwa kumpinda eneo la nyonga, na kumpiga makofi ya kushindilia 5 katikati mgongoni, kati ya mifupajembe (shoulder blades) ya mabegani. Tumia kiganja cha mkono wako.

Kama hili halitasaidia:
Makofi mgongoni.
Mmbinye tumboni
Simama nyuma ya majeruhi na kuzungusha mikono yako kiuno chake.

Weka mkono wako ukiwa umekunjwa kama ngumi dhidi ya tumbo lake, juu kidogo na kitovu na chini ya mbavu.

Funika ngumi yako na mkono ule mwingine na kuitumia mikono yote 2 kubinya kwa nguvu na haraka juu na ndani. Tumia nguvu ya kutosha kumwinua majeruhi juu ya miguu yake. (Tumia nguvu kidogo kiasi kwa ajili ya mtoto mdogo.) Rudia zoezi mara 5 mfululizo.
Mibinyo tumboni.


Kama kuna kitu ambacho kinazuia hewa kufika kwenye mapafu au kooni, nguvu ya hewa ambayo inasukumwa kwa nguvu inapaswa kukiondoa.

Kwa mwanamke mjamzito au mtu yoyote mnene, weka mikono kuzunguka sehemu ya kati ya kifua chake (weka ngumi yako katikati ya maziwa). Halafu binya kwa ndani.

Kama majeruhi atapoteza fahamu

Taratibu mlaze chini kwenye mgongo wake na angalia ndani ya mdomo wake. Kama utaona chakula au chochote kinachoziba koo, kiondoe kwa kutumia kidole ambacho umekunja kama ndoana. Lakini usisukume ndani kwa sababu hii inaweza kusababisha kitu kinachoziba kooni kuingia ndani zaidi. Halafu sukuma kwa nguvu na haraka eneo la kati kifuani hadi atakapoanza kupumua.

Kwa mtoto zaidi ya mwaka 1

Kama mtoto anakabwa na hawezi kulia wala kukohoa, jaribu kuzibua koo lake kwa kumpa makofi mepesi yenye mkazo mgongoni na mibinyo ya kifuani.

Kuzama majini

Mtoe mtu kwenye maji haraka iwezekanayo na bila kuchelewa anzisha pumzi maalum ya uokozi na mibinyo kifuani. Toa pumzi za uokozi kwanza ili kuingiza hewa kwenye mwili wa mgonjwa.

Kama mgonjwa atatapika, mgeuze alaliye upande na pole pole tumia kidole chako au kitambaa kupangusa matapishi ili asije kukabwa.

Pumzi maalum ya kuokoa maisha

Watu wanaweza kuishi kwa dakika 4 tu bila kupumua. Unaweza kunusuru maisha ya mtu mwingine kwa pumzi maalum za kuokoa maisha kama pumzi yake itasimama kwa sababu ya kukabwa, kupigwa kichwani, kukaribia kuzama, au kupigwa na shoti ya umeme, kuzidiwa na dozi ya dawa au akiwa na baridi kali (hypothermia).

Kama mtu atashindwa kupumua, unaweza kuponya maisha yake kwa kumpatia pumzi maalum ya kumuokoa mara moja.