Hesperian Health Guides

Shambulio linalofanana la kifafa (seizures), mtukutiko wa maungo (convulsions)

Katika sura hii:

Mashambulizi yanayofanana na kifafa ni vipindi vifupi (mara nyingi) vya upotevu wa fahamu, au mabadiliko katika hali ya kiakili, kawaida vikiambatana na mtikishiko wa viungo mbalimbali vya mwili.

Mashambulio ya aina hii husababishwa na homa kali, kupungukiwa na maji mwilini, jeraha, malaria, madhara ya sumu kwenye damu (sepsisi), au sababu zingine. Mashambulio kama haya yanayojirudia huitwa kifafa—angalia Matatizo ya kichwa na ubongo (kinaandaliwa). Kama mashambulio hayakusababishwa na baadhi ya vigezo hatari vilivyoelezwa juu, shambulio moja huenda lisiwe tatizo kubwa (ingawa linatisha kutazama). Lakini kama mashambulio yatarudia, muone mtaalam wa afya.

Matibabu

Wakati wa shambulio, ondoa vitu vyote katika eneo linalomzunguka mgonjwa ili asidhurike. Mgeuze upande ili asikabwe anapokuwa anatapika. Usimkandamize chini mtu ambaye anapata shambulio au kujaribu kukamata ulimi wake.

Kwa ajili ya shambulio kutokana na kupungukiwa na maji mwilini, tafuta msaada wa kitabibu. Baada ya shambulio kutoweka, mpe vinywaji vya kumuongezea maji mwilini.

Kwa ajili ya shambulio linalotokana na homa ya uti wa mgongo (meningitis) tafuta msaada wa kitabibu.

Kwa ajili ya shambulio kutokana na malaria, tafuta msaada wa kitabibu haraka. Ukiwa njiani, mpe diazipamu [diazepam]. Tibu malaria kwa dawa zake (angalia Baadhi ya maambukizi hatari: Madawa - kinaandaliwa).

Kama shambulio linadumu zaidi ya dakika 15, ingiza dawa ya diazipamu ya majimaji kwenye njia ya haja kubwa kwa kutumia bomba la sindano (bomba tu bila sindano). Angalia Taarifa juu ya dozi za dawa.

Mkazo wa ghafla wa misuli unaosababishwa na tetanasi unaweza kufikiriwa kuwa shambulio. Taya hufunga kwa nguvu na mwili hujipinda kuelekea nyuma. Jifunze kutambua dalili za mwanzo za tetanasi.

Baada ya shambulio, mtu anaweza kuonekana amechanganyikiwa au kuwa mzito kwa usingizi. Mfariji.

NWTND fa Page 50-1.png