Hesperian Health Guides

Kupoteza fahamu (kuzirai)

Katika sura hii:

NWTND fa Page 4-1-a.png
Visababishi vya kawaida vya kupoteza fahamu ni:


Kama mtu amepoteza fahamu na hujui kwa nini, haraka angalia kila jambo lifuatalo:

  1. Je anapumua vizuri? Kama hapana, pindisha kichwa chake nyuma na kuvuta taya na ulimi mbele. Kama kuna kitu ambacho kimekwama kwenye koo lake, vuta ukitoe. Kama hapumui, haraka tumia pumzi ya mdomo kwa mdomo (pumzi ya kuokoa maisha) kumsaidia kupumua.
  2. Je anapoteza damu nyingi? Kama ndiyo, jaribu kusimamisha utokaji damu.
  3. Yupo katika hali ya mshituko (anatokwa kijasho, ngozi imepauka; ni dhaifu, mapigo ya moyo yanakwenda haraka)? Kama ndiyo, mlaze kichwa chake kikiwa kwenye usawa wa chini ya miguu na legeza nguo zake.
  4. Je linaweza kuwa pigo la joto kali (hakuna jasho, homa kali, ngozi nyekundu ikiwa na joto)? Kama ndiyo, mkinge na jua, weka kichwa chake kwenye usawa juu ya miguu yake, na kumloweka kwenye maji baridi (kama inawezekana kwenye maji ya barafu) na kumpepea.

Jinsi ya kumlaza mtu aliyepoteza fahamu::

Ngozi imepauka sana: (mshituko, anazirai, nk.) NWTND fa Page 4-2-a.png
Ngozi nyekundu au ngozi ya kawaida: (pigo la joto kali, kiharusi, matatizo ya moyo, jeraha kichwani) NWTND fa Page 4-3-a.png

Kama mtu aliyepoteza fahamu anaweza kuwa na jeraha shingoni au mgongoni:

Ni bora kutombadilisha mkao wake hadi atakapopata fahamu. Kama unalazimika kumbadilishia mkao au kumshafirisha, mwondoe kwa uangalifu mkubwa, kwa sababu kama shingo au mgongo wake umevunjika, mabadiliko yoyote katika nafasi aliyomo yanaweza kusababisha majeraha makubwa zaidi. Angalia kama kuna vidonda au mifupa iliyovunjika, lakini usimtingishe sana. Usipinde mgongo au shingo lake.

Kamwe usimpe mtu aliyepoteza fahamu kitu chochote kwa njia ya mdomo.



Ukurasa huu ulihuishwa: 14 Feb 2024