Hesperian Health Guides
Vidonda kwenye kifua na mbavu ambazo zimevunjika
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Huduma ya kwanza > Vidonda kwenye kifua na mbavu ambazo zimevunjika
Maumivu yanayochoma pale mtu ambaye amejeruhiwa kifuani anapopumua au kukohoa, au kuhisi ulaini sehemu inapoguswa, vinaweza kuashiria mbavu zilizovunjika. Chunguza mbavu na kuzigusa na vidole vyako. Kama kuna sehemu ambayo imejitokeza juu chini ya ngozi, au mahali ambapo ikibonyezwa inaingia ndani na ni laini sana, mbavu hiyo imevunjika. Kama ni mbavu moja ambayo imevunjika na haijajitokeza chini ya ngozi au nje ya mwili, mpe dawa ya kupunguza maumivu. Anapaswa kuepuka kubeba vitu na kazi nzito kwa wiki kadhaa. Itapona bila matibabu maalum. Mkumbushe kupumua pumzi nzito kila baada ya saa chache. Hii inaumiza lakini husaida kuwezesha mapafu kuendelea kufanya kazi.
Mbavu nyingi kuvunjika
- Tumia kitambaa kilichokunjwa au pedi nzito iliyokunjwa na plasta kufunika mbavu zilizovunjika.
- Mlaze majeruhi katika hali yoyote ile inayomsaidia kupumua.
- Chunguza iwapo kuna dalili za mshituko na kutafuta msaada.
Vidonda kwenye kifua ambavyo vimeingia ndani
Kupigwa risasi, kuchomwa na kitu kikali, mlipuko, au mbavu ambayo imevunjika vibaya sana inaweza kusababisha hewa kuingia ndani na nje ya mapafu.
- Bila kuchelewa, funika uwazi huo ili hewa isingie kwa kutumia mathalan, bandeji ambayo imepakwa mafuta ya jeli, mfuko wa nailoni uliokunjwa vizuri, au hata jani la mgomba.
- Funga na plasta pande 3 tu ili hewa iweze kutoka lakini siyo kuingia.
- Mlaze katika nafasi yoyote ile itakayomwezesha kupumua. Tafuta msaada.