Hesperian Health Guides
Vidonda ambavyo vimeingia ndani
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Huduma ya kwanza > Vidonda ambavyo vimeingia ndani
Vidonda ambavyo vimeingia ndani vinaweza kupata ambukizo la tetanasi (pepopunda). Majeruhi anapaswa kupewa chanjo ya tetanasi (angalia Chanjo – kinaandaliwa) na sindano ya immunoglobulin ya kupambana na sumu ya tetanasi mwilini. Kama huna uhakika kuwa kufunga kidonda ni wazo zuri, huenda likawa siyo wazo zuri.
Kama kuna uhakika kuwa kufunga kidonda ni wazo zuri, huenda likawa siyo wazo zuri.
Kamwe usifunge vidonda vinavyotokana na kuumwa na wanyama, kutobolewa na vitu vikali, au vidonda ambavyo vimekaa vibaya au kuvurugika.
Yaliyomo
Majeraha kutokana na kuumwa na wanyama
Safisha majeraha hayo vizuri kwa maji na sabuni kwa dakika 15 au zaidi. Majeraha kutokana na wanyama yanaweza kupata maambukizi. Hivyo mpatie majeruhi dawa ya antibiotiki.
Kwa majeraha ambayo yanatokana na kuumwa na nyani, popo na wanyama wadogo, wapatie majeruhi chanjo ya kichaa cha mbwa na dawa ya immunoglobulini (immunoglobulin) haraka. Fanya hivyo kwa majeraha kutokana na kuumwa na mbwa kama mbwa husika anaweza kuwa na ugonjwa huo.
Dalili za ugonjwa wa kichaa cha mbwa hufanana sana na dalili za mafua, lakini tofauti na mafua, ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni hatari sana. Hivyo kama huna chanjo ya kichaa cha mbwa au immunoglobulini (immunoglobulin), wasiliana haraka na Ofisi au viongozi wa Idara ya Afya au Wizara ya Afya.
Majeraha ya visu
Majeraha ya visu ambayo yameingia ndani kawaida yanapaswa kuachwa wazi na kufanyiwa usafi mara kwa mara. Mpatie majeruhi dawa ya kloksasilini (cloxacillin) au klindamaisini (clindamycin) kwa ajili ya dalili yoyote ya maambukizi.
Majeraha ya visu kifuani au tumboni yanaweza kuhatarisha maisha. Tafuta msaada wa daktari haraka. Ili ufanye nini ukiwa njiani kuelekea hospitali au kituo cha afya, angalia jeraha la kisu kifuani au jeraha la kisu tumboni.
Majeraha ya risasi
Fuata maelekezo juu ya kusimamisha uvujaji damu kwa mgandamizo–pale mahali risasi ilipoingilia na mahali ilipotokea. Kama hakuna jeraha ilipotokea, huenda ikahitajika risasi kuondolewa mwilini. Tafuta msaada wa haraka.
Katika hali yoyote ile, safisha kidonda vizuri na mpatie majeruhi dawa ya kloksasilini (cloxacillin), klindamaisini (clindamycin), AU sefaleksini (cephalexin).
Kwa kidonda cha risasi kichwani, tafuta msaada hospitalini haraka. Ukiwa njiani, inua kichwa kidogo kwa kutumia blanketi iliyokunjwa au mito. Funika kidonda kwa kutumia bandeji safi.
Vidonda vya risasi vinaweza kupata maambukizi. Tafuta msaada wa daktari, hata kama dalili za maambukizi hazijajitokeza.
Kama risasi ilipiga mfupa, huenda mfupa umepasuka au kuvunjika. Funga kwa banzi au gongo na usiutumie mguu huo kwa wiki kadhaa. Angalia juu ya mifupa iliyovunjika. |
Ndoana ya samaki
Hatua 1: | Hatua 2: | Hatua 3: | |
Sukumzia ndoana kupita kwenye ngozi ili ijitokeze upande wa pili kama hivi: | Kata na kuondoa chembe au kipini. | Vuta nje sehemu ya ndoana iliyobaki. | |