Hesperian Health Guides

Dawa za vidonda kutokana na kung'atwa au kuumwa na wanyama

Huduma ya kwanza: Madawa

Majeraha kutokana na kung’atwa na wanyama yanapaswa kusafishwa vizuri kwa maji na sabuni. Mpe dawa ya antibiotiki kwa sababu majeraha hayo yana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi.

Amoksilini yenye klavulaniki asidi (amoxicillin with clavulanic acid) ndiyo dawa bora zaidi kwa kutibu majeraha kutokana na kung’atwa na wanyama.

Kama huna amoksilini yenye klavulaniki asidi, mpe dawa mojawapo:
Doksisaikilini (doxcyline) AU
Kotrimozazo (cotrimoxazole) AU
Penisilini V.

NA dawa mojawapo:
Metronidazo (metronidazole) AU
Klindamaisini (clindamycin).

Kama jeraha lilisababishwa na mbwa, choma chanjo ya kichaa cha mbwa na pia chanjo nyingine ya kusaidia kupambana na ugonjwa huo- rabies immunoglobulin (angalia chini).

Dawa ya kichaa cha mbwa ya immunoglobulini (immunoglobulin) na chanjo ya kichaa cha mbwa


Mahali penye wanyama wenye ugonjwa wa kichaa cha mbwa, majeraha yote au mkwaruzo kwenye ngozi kutokana na mnyama yatahitaji kusafishwa kwa sabuni na maji kwa angalau dakika 15, chanjo kadhaa za kichaa cha mbwa, na, kama hatari ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni kubwa, pia apewe sindano ya ugonjwa huo ya immunoglobulini.

Kuna aina kuu mbili za protini au antibodi kwa ajili ya kusaidia kupambana na kichaa cha mbwa (rabies immunoglobulin): moja imetengenezwa kutokana na majimaji ya damu ya binadamu (HRIG ), na nyingine kutokana na majimaji ya damu ya farasi (ERIG ). HRIG ni salama zaidi lakini ni ghali zaidi na huenda isipatikane sehemu unapoishi.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Kunaweza kutokea uviliaji na maumivu sindano ilipochomwa.

MuhimuNBgrnimportant.png

Immunoglobulini kwa ajili ya kichaa cha mbwa inaweza kusababisha mzio mkali kwa baadhi ya watu. Wakati wote, kuwa na dawa ya epinefrini (epinephrine au adrenaline) karibu kama tahadhari mzio utatokea.

Jinsi ya kutumiaNBgrninject.png

Choma imunoglobulini kwa ajili ya kichaa cha mbwa ndani ya kidonda kilichosafishwa na eneo linalozunguka.

Kama kuna vidonda kadhaa na huna chanjo ya kutosha kwa ajili ya kuchoma ndani ya vidonda vyote, ongeza myeyusho wa chumvi na maji (saline) ili kupata kiasi cha kutosha. Kwa njia hii mgonjwa atapata dozi sahihi na vidonda vyote angalau vitapata dawa.


Kutumia chanjo ya HRIG (Human Rabies Immune Globulin)
Choma uniti 20 kwa kilo mara moja.

Kutumia chanjo ya ERIG (Equine Rabies Immune Globulin)
Choma uniti 40 kwa kilo mara moja.


Pia toa chanjo ya kichaa cha mbwa (angalia Chanjo - inaandaliwa), lakini tumia sindano tofauti na kuchoma katika sehemu tofauti kwenye mwili. Choma miligramu 1 kwenye msuli siku ya kujeruhiwa, na baada ya hapo siku ya 3, 7, 14 (wiki 2) na 28 (wiki 4) baada ya siku ya kujeruhiwa.

Jinsi ya kutumia chanjo ya kichaa cha mbwa

Unapotoa dawa ya kichaa cha mbwa ya immunoglobulini, pia toa chanjo ya kichaa cha mbwa, lakini tumia sindano safi tofauti na kuchoma sehemu tofauti kwenye mwili. Choma kichupa chote cha chanjo (aidha 0.5 miligramu au miligramu 1 kutegemea na maelekezo ya mtengenezaji wa chanjo) kwenye msuli, sehemu ya juu ya mkono siku ya kujeruhiwa, na baada ya hapo siku ya 3 na ya 7. Halafu sindano ya 4 inapaswa kutolewa kati ya siku ya 14 (wiki 2) na 28 (wiki 4) baada ya siku ya kujeruhiwa.

Kwa mtoto wa miaka 2 au chini ya hapo, sindano hutolewa sehemu ya juu ya paja. Usichome chanjo ya kichaa cha mbwa kwenye makalio.

Hata kama hakuna dawa ya kichaa cha mbwa ya immunoglobulini, kuosha ngozi husika vizuri bila kuchelewa na kutoa chanjo kadhaa za kichaa cha mbwa kunaweza kusaidia kuzuia ugonjwa huo wa kichaa cha mbwa.