Hesperian Health Guides

Dawa za kutia ganzi

Huduma ya kwanza: Madawa

Lidokeni (lidocaine), lignokeni (lignocaine)


Lidokeni ni dawa ya ganzi ambayo inaweza kuchomwa eneo linalozunguka kidonda kutia ganzi ili mtu asisikie maumivu. Hii husaidia sana kabla ya kusafisha au kushona kidonda.

Lidokeni mara nyingi huja kama kimiminika chenye 2% ambayo ni miligramu 20 za lidokeni kwa mililita. Kama una dawa ya majimaji yenye asilimia (%) tofauti, rekebisha kiasi utakachotumia.

Jinsi ya kutumiaNBgrninject.png

Choma ndani na chini ya ngozi eneo ambalo unakwenda kuchana au kushona, ukiacha wastani wa sentimeta 1 kutoka sehemu ulipochoma sindano ya kwanza hadi nyingine. Choma lidokeni karibu na sehemu ya juu ya ngozi. Tumia takriban mililita 1 ya lidokeni kwa kila sentimeta 2 za ngozi. Usitumie zaidi ya mililita 20.