Hesperian Health Guides

Dawa za kuzuia tetanasi (pepopunda)

Huduma ya kwanza: Madawa

Dawa yenye protini au antibodi za kusaidia kupambana na ugonjwa wa tetanasi (antitetanus immunoglobulin)


Kama ratiba ya mtu ya chanjo za tetanasi iko nyuma (chanjo zote 3, na chanjo za kushtua (boosters) kila miaka 10), basi majeruhi anahitaji kutibiwa na dawa yenye protini au antibodi za kupambana na tetanasi (antitetanus immunoglobulin) haraka iwezekanavyo baada ya kidonda ambacho kinaweza kuambukizwa tetanasi kujitokeza. Mpe antitetanus immunoglobulin kabla dalili za tetanasi hazijaanza. Kama mgonjwa anapata chanjo ya tetanasi (angalia Chanjo - inaandaliwa) na antitetanus immunoglobulin kwa wakati mmoja, tumia sindano tofauti na kuchoma katika sehemu tofauti za mwili.

Usitoe chanjo yenye virusi hai kwa miezi 3 baada ya mtu huyu kupewa antitetanus immunoglobulin kwa sababu inaweza kusababisha chanjo kutofanya kazi ipasavyo.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Maumivu yanaweza kujitokeza pamoja na kuvia na wekundu sehemu chanjo ilipochomwa.

MuhimuNBgrnimportant.png

Dawa yenye antibodi au protini za kusaidia kupambana na tetanasi (antitetanus immunoglobulin) inaweza kusababisha mzio mkali kwa baadhi ya watu. Wakati wote kuwa na dawa ya epinefrini (epinephrine/adrenaline) karibu ili iweze kutumika mara moja iwapo mzio utajitokeza.

Jinsi ya kutumiaNBgrninject.png

Ingiza sindano ndani kwenye msuli.

Kwa ajili ya kidonda ambacho kimedumu chini ya saa 24, choma uniti 250 mara moja.

Kwa ajili ya kidonda ambacho kimedumu zaidi ya saa 24, au kidonda ambacho kwa asilimia kubwa kinaweza kuwa kimeambukizwa na virusi vya tetanasi.

Choma uniti 500 mara moja. Pia mpe dawa ya antibiotiki kama vile metronidazo AU penisilini G.