Hesperian Health Guides
Dawa za kupunguza wasiwasi, kukosa utulivu
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Huduma ya kwanza > Dawa za kupunguza wasiwasi, kukosa utulivu
Diazipamu (diazepam)
Diazipamu inaweza kutumika kulegeza misuli na kutuliza maumivu. inaweza pia kutumika kusimamisha shambulio la mara moja. Kwa watu wenye mashambulizi ya mara kwa mara (kifafa), tumia dawa tofauti, dawa ambayo inaweza kutumika kila siku.
Kusinziasinzia.
- Kuzidisha kiasi cha dawa ya diazipamu kinyume na maelekezo huweza kupunguza kasi ya kupumua au kusimamisha kupumua kabisa. Usitoe zaidi ya dozi ya dawa iliyoelekezwa na usitoe zaidi ya dozi 2.
- Diazipamu ni dawa inayojenga kiu cha kuendelea kuitumia. Epuka matumizi ya muda mrefu au ya mara kwa mara.
- Usitoe dawa hii kwa mjamzito au mama ambaye ananyonyesha isipokua tu kama amepata shambulio (kwa mfano kutokana na kifafa cha mimba).
- Usichome sindano ya diazipamu isipokuwa tu kama una uzoefu au umepitia mafunzo ya kufanya hivyo. Ni vigumu kutoa dawa hii kwa njia ya sindano. Badala yake, wakati wa shambulio, unaweza kuiweka kwenye njia ya haja kubwa (angalia chini).
Kulegeza misuli na kumtuliza mtu
Chini ya miaka 5: toa miligramu 1.
Zaidi ya miaka 5: toa miligramu 2.
Kwa ajili ya shambulio
Chini ya miaka 7: mpe miligramu 0.2 kwa kilo, mara moja.
Miaka 7 hadi 12: toa miligramu 3 hadi 5, mara moja.
Zaidi ya miaka 12: toa miligramu 5 hadi 10, mara moja.
Kama shambulio halijadhibitiwa baada ya dakika 15 za kutoa dawa hii, rudia dozi. Usirudie zaidi ya mara moja.
Lorazipamu (lorazepam)
Lorazipamu inafanana sana na diazipamu. Inaweza kutumika kulegeza misuli na kumtuliza mtu. Inaweza pia kutumika kusimamisha shambulio la mara moja. Kwa watu wanaopatwa na mashambulio ya mara kwa mara(kifafa), tumia dawa tofauti, dawa ambayo inaweza kutumia kila siku.
Kizunguzungu.
- Kuzidisha dozi ya dawa ya lorazipamu kunaweza kupunguza au kusimamisha pumzi kabisa.
- Lorazipamu ni dawa inayojenga kiu ya kuendelea kuitumia. Epuka matumizi ya muda mrefu au ya mara kwa mara.
- Usitoe dawa hii kwa mjamzito isipokuwa tu kama ana kifafa cha mimba au shambulio
- Usichome diazipamu kwenye msuli au mshipa isipokuwa tu kama una uzoefu au umepitia mafunzo ya kufanya hivyo. Ni vigumu kutoa dawa hii kwa njia ya sindano. Badala yake, wakati wa shambulio, unaweza kuiweka kwenye njia ya haja kubwa (angalia sehemu inayofuata).
Kulegeza misuli na kumtuliza mtu
Mwezi 1 hadi miaka 12: toa miligramu 0.05 kwa kilo, mara moja.
Zaidi ya miaka 12: toa miligramu 1 hadi 2, mara moja.