Hesperian Health Guides
Maumivu tumboni, kuhara, na minyoo
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Maumivu tumboni, kuhara, na minyoo

Matatizo ya tumboni yanaweza kusababishwa na mambo mengi. Kwa mfano, mtu anaweza kuwa na maumivu ya kawaida kwa sababu ya mafua, au kutokana na kula chakula kibaya, au kwa sababu ana wasiwasi juu ya watoto wake. Kila sababu huhitaji aina tofauti ya msaada (dawa ya vidonge kwa ajili ya maumivu kama haya haitafanya chochote kuondoa sababu hizo).
Lakini sababu ya kuhara, maumivu tumboni, au kichefuchefu inaweza kutokuwa wazi. Kama ilivyo kwa matatizo mengine ya kiafya, kuelewa chanzo cha tatizo ndiyo mwanzo wa tiba. Anza kwa kuuliza maswali juu ya tatizo, kama vile kuhara, halafu ulizia maswali ya kukusaidia kufahamu zaidi.
![]() |
Baadhi ya matatizo tumboni ni hatari na yanapaswa kutibiwa bila kuchelewa.
|
Yaliyomo
Maswali ya kuuliza kama kuna maumivu
![]() Je maumivu ni makali sana? Yanazidi kuongezeka?
![]() |
![]() Maumivu makali yanayoanza ghafla na kuzidi kuongezeka ni hatari! Chukua hatua haraka. Unapaswa kwenda hospitali.
|
![]() Mwanamke mwenye dalili hizi anaweza kuwa na maambukizi makubwa eneo la nyonga au mimba iliyotunga nje ya mji wa mimba au kizazi. | |
![]() Je tumbo linavuruga au kusokota?
|
![]() Maumivu makali ya ghafla yanayoambatana na kupata choo kidogo au kushindwa kupata choo kabisa pia ni dalili ya tatizo kubwa tumboni.
|
![]() Je maumivu yanaambatana na kichefuchefu na kutapika?
|
![]() Hii inaweza kuwa imesababishwa na kula ckakula kilichoharibika. Tumia vinywaji kwa wingi kama vile kinywaji maalum cha kuuongezea mwili maji.
|
![]() Je maumivu yanatokea baada ya kula? Je kuna hisia ya kuungua au moto kifuani au tumboni?
![]() |
![]() Huenda ni kiungulia, au vidonda vya tumbo.
![]() Inaweza pia kuwa tatizo la kibofu cha nyongo.
|
![]() Je kuna maumivu upande mmoja wa mgongo? Ni kama maumivu yamefunika mwili hadi kwenye nyonga?
|
![]() Hii inaweza kuwa mawe ya tumboni.
|
Maswali ambayo yanapaswa kuulizwa kama kuna kuharisha
Tatizo la kuharisha limeelezewa hapa. Tiba muhimu zaidi kwa tatizo la kuharisha ni kunywa vinywaji kwa wingi.Haraka iwezekanavyo, mgonjwa anapaswa kula chakula.
![]() Je ameharisha sana, bila maumivu kwa muda mfupi?
|
![]() Kuharisha sana choo chenye majimaji inaweza kuwa dalili ya kipindupindu. Kuharisha sana kunaweza kumdhoofisha mtu haraka au kusababisha kifo chake. Kumsaidia haraka kunywa kwa uendelevu na kula haraka iwezekanavyo kunaweza kusaidia kuponya maisha yake.
|
![]() Je kuna damu kwenye kinyesi?
|
![]() Kuharisha kinyesi kilichochanganyika na damu (ugonjwa wa kuhara damu) hutibiwa kwa kunywa vinywaji kwa wingi. Dawa za aina ya viua vijasumu au antibiotiki pia zinaweza kutumika.
|
![]() Je mharo una povupovu na unanuka sana ? Je mgonjwa anajamba sana?
|
![]() Hii inaweza kuwa aina ya ugonjwa wa kuharisha unaosababishwa na vijidudu viitwavyo giardia. Kunywa vinywaji kwa wingi. Dawa za aina ya antibiotiki (viuavijasumu) zinaweza kusaidia.
|
![]() Ni kwa muda gani amekuwa akiharisha ?
![]() |
![]() Baadhi ya vijidudu vya magonjwa kama vile giardia au ameba, husababisha kuharisha kuendelea kwa muda mrefu. Lakini kuharisha kunaweza kuendelea kwa muda mrefu zaidi kwa sababu mgonjwa ana tatizo lingine la kiafya kama vile:
|
![]() Je mhusika ana dalili nyingine ya ugonjwa-kama vile maumivu sikioni, homa, au mwili kuota upele ?
|
![]() Kuharisha kunaoambatana na homa inaweza kuwa homa ya matumbo au taifodi. Angalia sura kuhusu Baadhi ya magonjwa hatari ya kuambukiza (inaandaliwa). Kuharisha miongoni mwa watoto wakati mwingine husababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili na kutatoweka pale maambukizi hayo yatakapopona au kutibiwa. Kwa ajili ya:
|
![]() Je mgonjwa anatumia dawa za antibiotiki?
|
![]() Dawa za antibiotiki husababisha kuharisha kwa watu wengi na zinapaswa kuepukwa kama siyo lazima.
|
![]() Je ni idadi kubwa ya watu katika kaya au jamii ambao wamekumbwa na tatizo la kuhara kwa wakati mmoja?
|
![]() Watu wengi wanapokumbwa na ugonjwa wa kuharisha, kila mtu anapaswa kuchukua tahadhari kuzuia usienee. Unaweza kusaidia usienee kwa kunawa mikono mara kwa mara, kuosha au kumenya matunda na mbogamboga, kutibu maji ya kunywa, na kujenga vyoo mahali ambapo havipo. Angalia sura ya Maji na usafi wa mazingira. Kula chakula haraka mara bada ya kutayarishwa na kunawa mikono yako pamoja na kusafisha vifaa vinavyotumika kuandaa chakula. Kama kila mtu ambaye anaharisha atakuwa alikula chakula hicho hicho, yawezekana chakula kilikuwa kibaya.
|
Maswali ya kuulizwa kama huenda tatizo ni minyoo
Minyoo imeelezewa hapa. Baadhi ya minyoo ni kubwa kiasi cha kuonekana kwa macho katika kinyesi. Baadhi inaweza kuonekana tu kwa kutumia darubini.
Kama minyoo ni tatizo la kawaida katika eneo lako, watoto watibiwe minyoo kila baada ya muda.
![]() Je umeiona minyoo kwenye kinyesi? Minyoo ni tatizo la kawaida eneo lako?
|
![]() Kama mtu ana minyoo, mpe tiba sahihi ya minyoo.
|
![]() Tumbo limevimba?
![]() |
![]() Hali hii inaweza kusababishwa na mambo mengi yakiwemo:
|
![]() Kuna hisia ya kuungua, kuwashwa, au maumivu kwenye njia ya haja kubwa
|
![]() Kawaida hii ni bawasiri, au sehemu ya ngozi iliyochanika kutokana na kujipangusa baada ya kujisaidia.
![]() Kama mtoto atakuwa anajikuna sana kwenye njia ya haja kubwa, hasa usiku, hii inaweza kuwa dalili ya minyoo aina ya mchangouzi (pinworm).
|
Maswali juu ya matatizo mengine yanayohusiana na kinyesi
![]() Je choo kina weupe au rangi ambayo haijakolea ikilinganishwa na choo cha kawaida?
|
![]() Hii ni dalili ya ugonjwa wa ini-homa ya manjano au
|
![]() Je kuna damu nyekundu kwenye kinyesi?
|
![]() Kawaida hii ni bawasiri au kidonda kingine kwenye njia ya haja kubwa. Kawaida siyo hatari, lakini inaweza kuwa dalili ya saratani ya utumbo mkubwa (angalia sura ya Saratani - inaandaliwa).
![]() Mharo wenye damudamu na kamasi unaweza kuashiria ugonjwa wa kuhara damu.
|
![]() Je choo cheusi na kinanata kama gundi?
|
![]() Kawaida hii ni damu kutoka sehemu za juu kwenye utumbo au tumboni. Hii ni hatari. Bonyeza hapa.
|