Hesperian Health Guides

Matatizo mengine ya tumboni

Katika sura hii:

Tumbo kufunga au kupata choo kigumu

Choo kigumu, kikavu, au kwenda chooni kwa nadra vinaashiria tatizo la tumbo kufunga au kupata choo kigumu. Tatizo hili linaweza kuambatana na maumivu tumboni. Tatizo la kupata choo kigumu mara nyingi hutibika kwa urahisi.

Matibabu
  • Usitumie vilainisha tumbo au vitu vya kuchochea kutapika. Vitu hivi vinaweza kuwa hatari – hasa kwa watoto.
atl="nanasi, tikitimaji, papai, ndimo, zabibu, na matunda mengine"
  • Kula matunda kila siku.
  • Kula milo ya nafaka nzimanzima ambazo hazijasindikwa au kukobolewa – kama vile mchele au ngano.
  • Chotama unapokuwa unajisaidia kurahihisha kinyesi kutoka.
  • Tembea, tembeza viungo vya mwili wako na kufanya mazoezi zaidi. Watu wenye umri mkubwa, dhaifu au wagonjwa wanahitaji pia kutembeza viungo vya miili yao. Huenda wakahitaji msaada kufanya hivyo. Mtu yoyote hasitahili kubaki kwenye mkao mmoja siku nzima.
  • Kunywa maji zaidi. Jaribu kunywa angalau vikombe vya chai 8 au zaidi vya maji kila siku.
mwanamke amelalia upande mmoja, akijitoa kinyesi kigumu ambacho kimekwama kwa kutumia kidole kilichovalishwa glovu.


Kama tatizo la choo kigumu litaendelea, baada ya siku chache za kunywa maji zaidi na ulaji wa matunda na nafaka zaidi, tafuta msaada wa daktari.

Kama choo kigumu na kikavu kinakwama kwenye unyeo na kusababisha maumivu, huenda ukahitajika kukitoa. Paka mafuta kidogo, Vaseline, au sabuni kwenye kidole kilichovalishwa glovu na kuondoa kinyesi kilichokwama kwa kutumia mkono wako.

Kupata choo kigumu mara nyingi hujitokeza kama tatizo la pembeni baada ya kutumia vidonge vya madini chuma na dawa zingine kali kama vile morphine na codeine. Fuata maelekezo yaliyoorodheshwa juu. Mwili wako utakapoanza kuikubali dawa hiyo, ugumu wa choo utapungua.

Kinyesi kutokea ukeni

Kama kinyesi kitavuja kupitia ukeni, hii inamaanisha kuna tundu kati ya utumbo na uke, linalojulikana kama fistula. Hali hii mara nyingi husababishwa na kukaa katika uchungu wa uzazi muda mrefu na matatizo katika kujifungua ambayo husababisha sehemu ya mwili wa mwanamke kuchanika na kuacha tundu. Pia fistula inaweza kutokana na kubakwa. Mara nyingi zaidi, tundu hutokea kati ya uke na kibofu, na kusababisha mkojo kuvuja. Hivyo, fistula imeelezewa kwa undani kama sehemu ya matatizo mengine yanayohusiana na mfumo wa mkojo katika sura ya Matatizo yanayohusiana na kukojoa (inaandaliwa).

Damu kutoka kwenye njia ya haja kubwa

Damu nyekundu enye kung’aa kutoka kwenye njia ya haja kubwa mara nyingi ni dalili ya ugonjwa wa bawasiri. Tafuta msaada wa daktari haraka kama kuna damu nyingi, kama kuna mabonge ya damu iliyoganda kutoka kwenye njia ya haja kubwa, au maumivu.

Damu yeyote kutoka kwenye njia ya haja kubwa (nyekundu inayong’aa, nyekundu nzito, au nyeusi) inaweza pia kuwa dalili ya saratani.

Dalili za hatari
  • Kinyesi cheusi na ambacho kinaonekana kama lami.
  • Matapishi yaliyochanganyika na damu au ambayo yanaonekana kama kahawa iliyosagwa.


Dalili moja wapo inamaanisha kuwepo uvujaji damu juu kwenye mfumo wa chakula. Kawaida hali hii ni hatari na inahitaji msaada wa haraka wa daktari.