Hesperian Health Guides

Kupungukiwa maji mwilini

Katika sura hii:

mtoto aliyekonda na kuonekana mchovu, macho yake yakiwa yameigia ndani Kupungukiwa na maji mwilini humaanisha kuwa hakuna maji ya kutosha mwilini. Tatizo hili linaelezewa kwenye sura hii kwa sababu chanzo chake kikuu ni kuharisha. Kupungukiwa na maji mwilini kunaweza kutokana pia na kutapika, mwili kupata sana joto kutokana na jua kali, kufanya kazi kubwa kupita kiasi, au kuvaa nguo nyingi nzito. Hasa kwa watoto wadogo, tatizo la kupungukiwa na maji mwilini linaweza kuongezeka haraka na kuweza kusababisha mauti.

Bila kuzingatia kisababishi, tiba ambayo mtu yoyote anaweza kutoa nyumbani kwa mtu mwenye dalili za kupungukiwa na maji mwilini ni kumuongezea maji mwilini kwa kumpatia vinywaji kwa wingi. Kwa njia hii unaweza kuponya maisha yake.

Dalili
  • Kiu
  • Mdomo na ulimi mkavu (unapogusa ndani ya shavu la mgonjwa, unahisi pakavu)
  • Kukojoa mara chache na mkojo ukiwa na rangi nzito

Unapobaini dalili hizo, anza tiba mara moja kabla hali haijawa mbaya zaidi.

Dalili zinazoonesha upungufu mkali wa maji mwilini
  • Udhaifu mwili mzima: uchovu,kukosa nguvu, usingizi nk
  • Mapigo ya moyo kwenda haraka
  • Pumzi nzito
  • Macho kuingia ndani yasiyo na machozi
  • Ngozi inapofinywa kubaki katika hali hiyo ya kufinywa
ngozi imebaki katika hali ya kufinywa
Vuta ngozi katikati ya vidole viwili kama kwenye mchoro... kama ngozi haitarudi katika hali yake ya kawaida, huenda mtu huyu ana upungufu mkali wa maji mwilini.
  • Miongoni mwa watoto wachanga, shimo laini juu ya kichwa
Tiba na uzuiaji

Wakati wote, ni bora, salama na rahisi zaidi kuzuia upungufu wa maji mwilini kuliko jitihada za kuutibu pale unapotokea. Mpatie vinywaji kabla ya dalili za kupungukiwa maji kujitokeza.

Upungufu wa maji mwilini huweza kuzuilika na kutibika kwa njia ile ile-kunywa vinywaji kwa wingi.


mwanamke akikatisha kazi zake kidogo kiwandani ili aweze kunywa maji

Unaamini kwamba kunywa vinywaji kutasababisha tatizo la kuharisha kuongezeka? Ni rahisi kufikiria hivyo unapoangalia mharo wenye majimaji ukimtoka mtoto. Lakini vinywaji havisababishi kuharisha.

happy, healthy-looking child holding a glass of water

Kuhara hutokana na maambukizi ya vijidudu vya magonjwa. Kuhara kutaendelea hata kama mtu atakunywa au la. Lakini kumpatia vinywaji husaidia mtu anayeharisha kubaki na nguvu za kutosha ili aweze kupona kutokana na maambukizi.

Mtu anayeharisha asipotumia vinywaji atapungukiwa na maji mwilini na huenda akapoteza maisha. Unaweza kunusuru maisha kwa kutoa vinywaji ili kufidia maji ambayo yamepotea. Kutotoa vinywaji siyo kinga kwa watoto kutoharisha. Badala yake huwaweka watoto hatarini.

Kunywa vinywaji kwa wingi hukusaidia kubaki na nguvu, na pia kupata nafuu.

Vinywaji maalum vya kuongeza maji mwilini

Kuongeza maji mwilini humaanisha kuurudishia mwili maji ambayo tunakuwa tumepoteza kupitia kuharisha na njia zingine zinazochangia upungufu huo. Tunapokua tunaharisha, tukitapika, na tunapotoa jasho, huwa tunapoteza maji ya mwilini. Hivyo vinywaji maalum vya kuongeza maji mwilini lazima vijumuishe maji. Pia huwa tunapoteza virutubishi ambavyo hutokana na chakula tunachokula, hasa chumvi na nishati( ambavyo huwa tunapata kutokana na vyakula vyenye sukari au nafaka au protini. Katika kuurudisha maji mwili, tunapaswa kufidia virutubishi hivi pia. Maji + sukari kidogo + vyakula vya wanga(sukari au ugali = kinywaji maalum cha kuurudishia mwili maji).

Mpe kinywaji maalum cha kuurudishia maji mwili kadri atakavyoweza kunywa, kipimo kimoja baada ya kila anapoharisha. Kila kipimo kiwe angalau na ujazo wa kikombe kimoja cha mtoto mdogo, kikombe kimoja au zaidi ya cha mtoto mwenye umri mkubwa kidogo au mtu mzima.

Endelea kutoa kinywaji cha kuurudishia mwili maji hadi tatizo la kuharisha litakaposimama na dalili za kupungukiwa na maji mwilini kutoweka.


Ni vinywaji gani vizuri kwa ajili ya kuurudishia mwili maji? Karibu kila kinywaji ambacho unaweza kutengeneza kwa urahisi nyumbani ni kinywaji kizuri kwa ajili ya kuongeza maji mwilini!

Kinywaji cha chumvi na sukari

NWTND bag Page 22-1.png

Nyumbani au kwenye kiliniki, unaweza kutengeneza kinywaji rahisi cha kuongeza maji mwilini. Ni kinywaji chenye gharama ya chini lakini ubora unaolingana na kinywaji kutokana na paketi za mchanganyiko wa chumvichumvi ambao umetengenezewa viwandani.

1. Katika lita 1 ya maji masafi.

2. Changaya chumvi ½ kijiko cha chai. NWTND bag Page 22-2.png

Onja mchanganyiko huo. Unapaswa kuwa na chumvichumvi kidogo kuliko machozi.

3. Halafu changaya ndani vijiko 8 vya chai vya sukari-vyenye ujazo wa tambarare.

AU, badala ya sukari, changanya ndani vijiko vya chai 8 vilivyojaa kabisa nafaka, kama vile mchele au unga wa mahindi. Kama utatumia nafaka, pika mchanganyiko huu kwa dakika chache kabla ya kumpatia mhitaji. NWTND bag Page 22-3.png NWTND bag Page 22-3.png


Kuchangaya kipimo kimoja cha maji ya kuongeza maji mwilini:

NWTND bag Page 41-2.png
NWTND bag Page 22-5.png
NWTND bag Page 22-6.png
child being fed rehydration drink from a glass
Glasi 1 + Kipimo cha chumvi 1 + Vijiko vya chai 2 au 3 vya sukari au nafaka zilizochemshwa

Maji ya mchele

Maji ya mchele hufanya kazi vizuri sawa na mchanganyiko wa chumvi na sukari katika kuurudishia mwili maji. Pika mchele kwenye maji mara mbili ambayo ungetumia katika hali ya kawaida. Ongeza chumvi kidogo kwenye maji. (Takriban ½ kijiko cha chai cha chumvi kwa kila lita ya maji.) Unaweza kuongeza sukari kidogo kama utataka. Kunywa kiasi kadri uwezavyo. Unaweza pia kula wali uliopo kwenye machangayiko huo.

Nafaka zingine za nyumbani

Kama huwa unatengeneza uji au chakula kingine aina ya ujuuji kwa ajili ya matumizi yako au ya watoto wadogo, chakula aina hiki kinaweza kuongezwa maji ili kiweze kutumika kumuongezea mtu maji mwilini. Unga wa mahindi, viazi au mhogo vyote vinaweza kusaidia kumuongezea mtu maji mwilini(kama vitapikwa vizuri, kupondwapondwa, kuongezwa maji mengi na pia kutiwa chumvi kidogo).

Uji mwepesi kama huo hauwezi kufidia hitaji la chakula. Kama uji utafanywa mwepesi na kutumika kama kinywaji cha kuongeza maji mwilini, pia uji mzito uandaliwe kwa ajili ya kula kama kawaida. Ili kupona haraka kutokana na upungufu wa maji mwilini, mpatie mgonjwa chakula sambamba na vinywaji.

Mtindi au maziwa mengine yaliyochachushwa

Hivi ni vinywaji vizuri kwa ajili ya kuurudishia mwili maji na pia hutoa protini. Kama mtindi utakuwa mzito sana, changanya na maji kidogo. Pia ongeza chumvi kidogo kwenye kila glasi.

Maziwa ya mama

mwanamke akimyonyesha mtoto

Kama unanyonyesha mtoto anayeharisha, endelea kufanya hivyo. Mnyonyeshe mtoto mara nyingi zaidi – angalau kila baada ya kuharisha. Mruhusu anyonye kadri atakavyotaka. Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji mwilini anapaswa kupewa kinywaji mchanganyiko wa chumvi na sukari kila anapomaliza kunyonya.

Epuka vinywaji ambavyo huzidisha upungufu wa maji mwilini

Chupa ya Coca-cola ikiwa na alama kubwa ya HAPANA kupita katikati yake t
Hapana!

Vinywaji vilivyokolezwa sukari,vinywaji vyenye kemikali ya kafini (caffeine), na pombe huzidisha tatizo la upungufu wa maji mwilini. Hivyo epuka:

  • Soda (Coke, Fanta, Pepsi) na vinywaji vingine vilivyokolezwa sukari.
  • Kahawa na chai iliyokolea sana.
  • Biya, mvinyo na pombe zingine.


Vipi kuhusu maji ya kawaida ambayo hayajachanganywa na chochote?

Unapokuwa umepungukiwa na maji mwilini,maji ya kawaida ambayo hayajachanganywa na chochote siyo bora kama vinywaji maalum kwa ajili ya kuuongezea mwili maji kwa sababu hayana virutubishi ambavyo mwili wako unahitaji. Unapokuwa umepungukiwa maji mwilini, kunywa maji ya kawaida kunaweza kusababisha uugue kwa sababu unahitaji pia chumvi na nishati. Lakini ni bora kumpa mgonjwa maji ya kawaida ambayo hayajachanganywa na chochote kuliko kutompa kinywaji chochote-angalau kwa muda mfupi. Mpe maji wakati unasubiri maji ya mchele au uji wa nafaka kuiva.

Lazima maji yachemshwe kwanza?

Maji ambayo yamechemshwa au kutibiwa kuua vijidudu ni bora zaidi. Kwa taarifa zaidi juu ya jinsi ya kuyafanya maji kuwa salama zaidi kwa ajili ya kunywa, bonyeza hapa.

Lakini kama huna kuni kwa ajili ya kuchemsha maji, au kupata maji safi ni shida, tumia maji uliyonayo hadi utakapoweza kuboresha usalama wa maji yako.

Paketi ya chumvichumvi kwa ajili ya kuongeza maji mwilini

packet of oral rehydration salts

Paketi za chumvichumvi kwa ajili ya kuongeza maji mwilini zinaweza kupatikana kwenye duka la dawa, kiliniki, au sokoni. Kama vilivyo vinywaji vya kuurudishia maji mwili ambavyo hutengenezewa nyumbani, paketi hizi zina mchanganyiko wa chumvi na sukari kwa kiasi kinachostahili kutibu upungufu wa maji mwilini. Pia ndani kuna madini ya potasiamu, saitreti, na zinki-virutubishi ambayo husaidia sana watu wanaoharisha. Mahali ambapo bidhaa hii inaweza kupatikana, hutoa njia rahisi ya kutengeneza kinywaji cha kuurudishia mwili maji. Kumbuka kuongeza kiasi sahihi cha maji – kawaida lita 1 ya maji kwa kila paketi. (Lakini soma maelekezo kwenye paketi kwa sababu kuchanganya na maji kidogo sana au maji mengi sana kunaweza kusababisha ugonjwa kuzidi.)

Kama paketi za chumvichumvi hizi (ORS) hazipatikani kwa urahisi, ni bora zaidi kutengeneza kinywaji chako mwenyewe cha kuurudishia mwili mali – gharama yake ni nafuu zaidi. Tumia fedha zako kwa kununua mboga mboga, maharagwe, mayai, au vyakula vingine vinavyofaa kiafya. Kinywaji chako ulichotengeneza nyumbani kinalingana katika ubora na paketi iliyotengenezewa kiwandani, na chakula chenye virutubishi kitakusaidia kupona haraka.