Hesperian Health Guides

Maji na afya

Katika sura hii:

 woman carrying an infant, a bag, and a water jug

Matatizo mengi yanayotufanya tuugue yanaweza kuzuilika. Baadhi ya njia za kuzuia magonjwa huhitaji muda, juhudi na fedha zaidi mwanzoni, lakini hunusuru muda na fedha baadae kwa kutuepeusha na magonjwa. Sura hii inaelezea jinsi ya kuzuia kuharisha na magonjwa mengine yanayosababishwa na vijidudu vilivyomo kwenye kinyesi cha binadamu na wanyama. Matatizo mengi yanayoathiri tumbo na matumbo yanaweza kuepukwa kwa kunawa mikono, kuzingatia usafi katika kuandaa na kuhifadhi chakula, kutumia vyoo kwa usahihi, na kunywa maji safi na salama.

Ili kujifunza jinsi ya kuzuia:

  • utapiamlo, kisukari, ugonjwa wa moyo, na matatizo mengine yanayosababishwa na lishe duni, angalia Lishe bora hutengeneza afya bora,
  • nimonia au kichomi,kifua kikuu, na matatizo mengine ya kupumua angalia Matatizo katika kupumua na kikohozi(kinaandaliwa).
  • matatizo ya kiafya yanayosababishwa na utupaji hovyo wa taka za kawaida na taka zingine, angalia Taka za kawaida, Taka za hospitalini na uchafuzi wa mazingira (kinaandaliwa).
  • malaria, homa ya denge, na magonjwa mengine yanayoambukizwa kupitia mbu, angalia Baadhi ya magonjwa hatari ya kuambukizwa (kinaandaliwa).

Maji ambayo ni salama kwa ajili ya kunywa

Pamoja na hitaji la kuwepo maji ya kutosha, watu pia wanahitaji maji ambayo ni salama kwa ajili ya kunywa, yasiyo na vijidudu na kemikali hatari. Maji yaliyochafuliwa husababisha:

NWTND was Page 17-1.png
  • Homa ya manjano(hepatitis A), homa ya matumbo (taifodi), na magonjwa mengine hatari.
  • Ugonjwa wa kuhara, ambao husababisha kupungukiwa na maji mwilini na hatimaye vifo hasa kwa watoto.
  • Maambukizi kama vile kichocho ambayo yanaweza kuchangia upungufu wa damu mwilini(anemia) na utapiamlo.


Njia kadhaa za kusafisha maji zimeelezewa katika sehemu inayofuata. Ni muhimu kwa jamii yako kuzuia uchafuzi wa maji au matumizi hovyo ambayo husababisha maji kupungua.

Yanapokuwepo maji salama yakutosha, watoto hukua vizuri na hawasumbuliwi sana na ugonjwa wa kuharisha.


Kutafuta maji

Maji yanapaswa kuchotwa kwenye chanzo chenye usalama zaidi katika eneo husika. Unapochota maji kutoka kwenye mto, chota eneo la juu la mto maji yanapotokea:

kijito kinachotirika pembeni mwa shamba na kijiji, ng’ombe akijisaidia kwenye maji, pia kuna taka zilizotupwa ndani ya maji, na mwanamke ambaye anafulia nguo ndani ya kijito hicho
mashamba yanayotumia viuatilifu au mbolea za kemikali
mahali ambapo watu na wanyama hujisaidia
mahali watu huogea, au kuoshea vyombo vya nyumbani au kufulia
uchafuzi wa aina mbalimbali kutoka kwenye makazi (taka mchanganyiko, gesi, au mafuta)


Uvunaji wa maji ya mvua

vipande vya mianzi vikining’inia kutoka kwenye paa kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua

Maji ya mvua ni rahisi kuvunwa kutoka kwenye paa za nyumba na kukusanywa kwenye vyombo vya kuhifadhia kama vile mapipa au matenki yaliyoweka pembeni ya nyumba. Paa ambazo zimetengenezwa kutokana na mabati ni bora zaidi kwa ajili ya uvunaji wa maji ya mvua. Maji yanahitaji kutibiwa kabla ya kunywa (angalia sehemu inayofuata) kwa sababu huenda kukawa na vijidudu kwenye paa kutokana na uchafu, au vinyesi vya ndege au wanyama wengine. Paa ambazo zimetengenezwa kutokana na madini chuma yakiwemo risasi, asbesto, au lami yana kemikali zenye sumu ndani yake ambazo huyafanya maji hayo kutokuwa salama kwa ajili ya kunywa. Hakikisha chombo cha kuvunia au kuhifadhia maji ni safi na hakijawahi kutumika kwa ajili ya kemikali kama vile mafuta au viuatilifu.

Kuyafanya maji kuwa salama kwa ajili ya kunywa

Kuyafanya maji kuwa salama kwa ajili ya kunywa ni njia bora zaidi mojawapo ya kuzuia kuharisha na magonjwa. Maji kutoka chanzo chochote kile yatahitaji kutibiwa kama kutakuwa na vijidudu. Hata kama maji yatakuwa yanaonekana safi kwa macho na kutiririka kutoka bombani, kwenye matenki, au visimani, hii haimaanishi kuwa hayajafuliwa au hayahitaji kutibiwa.

Katika kuamua njia gani ya kutibu maji itumike, fikiria juu ya kiasi cha maji unachohitaji., yamechafuliwa na nini, na rasilimali zilizopo kwa ajili ya kazi ya kuyatibu. Chati ifuatayo inaweza kukusaidia kuamua njia gani itumike kama unajua tatizo kubwa linaloathiri maji eneo lako. Njia utakapotumia itategemea msimu au mahali ulipo. Kwa mfano, unaweza kutumia njia moja unapokuwa nyumbani na njia nyingine unapokuwa unafanya kazi shambani.


Tatizo Njia za kuchuja maji Njia za kutibu maji
Chujio la kitambaa Chujio la mkaa Chemsha Klorini Joto la jua Ndimo au juisi ya laimu
Virusi (kama vile homa ya manjano na homa ya matumbo)
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
Bakteria (kama vile shigella na e. coli)
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
Amebas
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
Giardia
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
Cryptosporidia
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
Kipindupindu
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
NWTND was Page 19-1.png
Chati inaonesha vijidudu na vimelea gani ambavyo hudhibitiwa na njia mbalimbali. Tone la maji linamaanisha kuwa njia hiyo inafaa kuangamiza kijidudu husika.


Kama kuna zaidi ya sababu moja ya ugonjwa unaoenezwa kupitia majimahali unapoishi (ambalo ndiyo hali inayojitokeza mara nyingi), ufumbuzi bora unaweza kuwa ni kuunganisha njia 2: kuchuja na kutibu.

Kuchuja maji

Kuna njia nyingi za kuchuja maji ili kuyafanya yawe salama zaidi. Chujio za kitambaa na mkaa zinaelezewa katika sehemu ifuatayo.

Kama maji yako yana uchafu, kwanza ruhusu yatulie kwenye chombo kwa saa kadhaa ili uchafu, na vijidudu vya magonjwa viweze kusuka chini ya chombo. Mwaga maji yaliyotulia kwenye chujio. Usijaribu kutikisa uchafu uliotulia chini ya chombo. Halafu safisha chombo.

Chujio za kitambaa

Katika nchi za Bangladesh na India, watu hutumia chujio iliyotengenezwa kutokana na kitambaa chenye nyuzi zilizoshonwa vizuri kwa karibu kuondoa vijidudu vya kipindupindu kwenye maji. Vijidudu vya kipindupindu mara nyingi hujibanza kwenye mnyama mdogo yoyote aishiye majini, na zoezi la kuchuja na kuwatoa nje wanyama hao pia huondoa vijidudu vingi vya kipindupindu. Unaweza kutengeneza chujio la kitambaa kutokana na vitambaa vya mkononi, vitambaa vya pamba na vitambaa vingine vyenye nyuzi zilizofungamana vizuri. Nguo zilizowahi kutumika hufanya kazi vizuri kwa sababu nafasi katika nyuzi za nguo zilizotumika huwa zinakuwa zimepungua sana na hivyo kuchuja vizuri.

wanawake wawili wakichuja maji kwa kutumia kitambaa na kuyakusanya kwenye jagi
  1. Ruhusu maji yatulie kwenye chombo ili uchafu utue chini.
  2. Kunja kitambaa mara 4,tanua au funga juu mdomo wa chombo kingine au jagi.
  3. Mwaga maji polepole kutoka kwenye chombo cha kwanza kwenda chombo kingine kupitia chujio la kitambaa. Kila mara tumia upande mmoja wa kitambaa, au vijidudu vitaingia kwenye maji.
  4. Baada ya kutumia kitambaa, fua na kukausha juani. Hii huua vijidudu ambavyo vinaweza kuwa vilibaki kwenye kitambaa.Wakati wa msimu wa mvua, tibu kitambaa kwa kutumia dawa maalum ya kuwa vijidudu (bleach).

Chujio za mkaa

Kutengeneza chujio la mkaa, utahitaji ndoo safi 2 za chuma na plastiki, nyundo,msumari 1 au 2, ndoo iliyojaa mchanga ambao haujapembuliwa, na ¼ ndoo ya mkaa.

  1. Toboa matundu kwenye ndoo moja wapo. Osha ndoo. Hii ndiyo itakuwa ndoo ya kuchujia.
  2. Safisha mchanga kwa kuuloweka kwenye maji mara kadhaa na kuyaondoa hadi yatakapoonekana safi.
  3. Weka safu ya mchanga uliooshwa yenye sentimeta 5 kwenye ndoo ya kuchujia na kumwaga maji juu yake. Maji yanapaswa kupita kwenye matundu. Kama hakuna maji yanayopita, panua matundu hayo. Kama mchanga utapita, hii ina maana matundu ni makubwa kupita kiasi. Kama hii itatokea, ondoa mchanga, weka kitambaa chepesi juu ya matundu yale, na kubadilisha mchanga.
  4. Saga mkaa kupata vipande vidogo vidogo. Mkaa wa kawaida unafaa kwa kazi hii. Kamwe usitumie mkaa kutokana na taka kwani ni sumu!
  5. Weka safu ya mkaa uliosagwa yenye ukubwa wa sentimeta 8 juu ya mchanga. Halafu jaza ndoo na machanga zaidi ambao umeoshwa hadi kufikia sentimeta 10 kutoka ncha ya juu ya ndoo.
  6. Weka vijiti 2 juu ya ndoo ya pili na kukalisha ndoo yenye chujio kwenye vijiti hivi. Mwaga maji safi kupitia ndoo yenye chujio. Kama maji yanaoingia kwenye ndoo ya pili yanonekana safi, basi chujio liko tayari kuanza kutumika.
  7. Ruhusu maji kutulia kabla ya kumwaga kupitia kwenye chujio.
maji yakimwagwa kwenye chujio la mkaa
Ndoo yenye chujio
Sentimeta 10
Mchanga
Sentimeta 8 mkaa
Sentimeta 5 mchanga
Vijiti vya kubeba ndoo
Ndoo safi ya kukusanya maji


Kwa sababu vijidudu vya magonjwa ambavyo vimechujwa vitaota kwenye mkaa, ni muhimu kuondoa na kuusafisha mkaa baada ya kila wiki kadhaa iwapo chujio litakuwa likitumika kila siku, au wakati wote chujio likibaki bila kutumika kwa siku chache. Kuusafisha mkaa, toa kwenye chujio na kutiririsha maji juu yake. Ruhusu ukauke, ikiwezekana chini ya jua kali. Halafu rudisha mkaa kwenye chujio.

Ni salama zaidi pia kutibu maji baada ya kuchuja kwa kuchemsha, kuongeza klorini, au kwa joto la jua.

Kutibu maji

NWTND was Page 23-1.png
Kuchemsha maji kwa dakika 1 huua vijidudu vya magonjwa na kuyafanya kuwa salama kwa ajili ya kunywa.

Kuchemsha maji

Wezesha maji kuchemka haraka. Endelea kuchemsha kwa dakika 1 kabla ya kuepua chombo kutoka kwenye moto ili yaweze kupoa. Katika sehemu za juu milimani, maji yachemke kwa dakika 3.

Uchemshaji unaweza kubadili ladha ya maji, hasa iwapo yatachemshwa kwenye moto wa kuni. Iwapo ladhaa yake hairidhishi, mimina maji hayo ambayo yamepoa kwenye chupa na kuitikisha. Kutikisha chupa huongeza hewa kwenye maji na kuboresha ladha.

Kuchemsha maji baada ya kuivisha chakula, lakini kabla moto haujafifia, ni njia moja ya kubana matumizi ya mkaa.

Klorini

Kiasi cha klorini ambacho kinahitajika kutibu maji hutegemea kwa kiwango gani maji hayo yalivyochafuliwa. Wingi wa vijidudu kwenye maji, ni kiashiria cha wingi wa dawa ya klorini inayohitajika kuwaangamiza. Kiwango sahihi kinapotumika, maji kwa umbali yatakuwa na harufu na ladha ya klorini. Hii ni ishara kwamba maji hayo ni salama kwa ajili ya kunywa. Kama kiwango kikubwa cha kilorini kimetumika, harufu na ladha itakuwa kali na isiyopendeza.

Klorini huuzwa katika viwango tofauti vya kukolezwa. Viwango ambavyo vimeorodheswha katika sehemu inayofuata vinaonesha jinsi ya kutibu maji kwa kutumia dawa ya yenye asilimia 5 ya klorini (sodium hypochlorite). Soma kibandiko kwenye dawa kujua ni aslimia ngapi ya klorini iliyopo kwenye dawa hiyo.Kama dawa ina asilimia 3 za klorini, utahitaji kutumia zaidi. Kama kibandiko kinajumwisha maelekezo ya kutibu maji, fuata maelekezo hayo. Usitumie dawa ambayo ina sabuni au manukato ndani yake.

Kama maji yatakuwa na uchafu unaoelea au vipande vya uchafu ndani yake, chuja maji kabla ya kuyatibu na klorini.

Maji Ongeza dawa (bleach 5%)
Kwa lita 1
NWTND was Page 23-2.png
NWTND was Page 23-3.png Matone 2
Kwa galoni 1 au lita 4
NWTND was Page 23-4.png
NWTND was Page 23-5.png Matone 8
Kwa galoni 5 au lita 20
NWTND was Page 23-6.png
NWTND was Page 23-7.png Kijiko cha chai ½
Kwa pipa la lita 200
NWTND was Page 23-8.png
NWTND was Page 23-9.png Vijiko vya chai 5

Baada ya kuongeza kiwango sahihi cha klorini, koroga vizuri na kusubiri angalau dakika 30 kabla ya kunywa. Kama maji hayana harufu au ladha ya klorini kwa mbali baada ya kuongeza kiwango kilichooneshwa, ongeza kiwango hicho hicho tena. Changanya na kusubiri kabla ya kunywa.

NWTND was Page 24-1.png

Jua

Kutibu maji kwa joto la jua hufanya kazi vizuri zaidi katika maeneo yaliyopo karibu na ikweta, kwa sababu jua ni kali zaidi eneo hilo. Unapokwenda kasikazini au kusini zaidi ya Ikweta, muda zaidi utahitajika kwa ajili ya jua kutibu maji vizuri.

Maji yanapochujwa kwanza ili yawe safi zaidi husaidia kutibiwa haraka zaidi. Safisha chupa ya plastiki au glasi, au mfuko wa plastiki. Chupa za soda za plastiki ndiyo bora zaidi kutumia. Jaza chupa nusu, halafu tikisa kwa zaidi ya sekunde 20. Hii huongeza viputo vidogo vya hewa ndani ya maji ambavyo husaidia maji kutibika haraka. Halafu jaza chupa hadi juu. Weka chupa kwenye jua, mahali ambapo watu na wanyama hawatafikia, kama vile juu ya paa la nyumba. Acha chupa ibaki kwenye jua kali angalau kwa saa 6, au kwa siku 2 kama kuna mawingu.

“vipande 2 vya limau na chupa ya lita ya maji
Tumia limau 1 kwa ajili ya kila lita ya maji

Limau au maji ya limau

Ongeza juisi ya limau kwenye lita 1 ya maji ya kunywa na kuruhusu kutulia kwa dakika 30. Asidi kutoka kwenye juisi itaua vijidudu vingi vya kipindupindu na vingineo. Njia hii siyo nzuri sana kwa sababu vijidudu vingi vinaweza kubaki kwenye maji, lakini ni bora kuliko kutotibiwa kabisa, hasa kwa maeneo yenye kipindupindu.

Hifadhi maji kwa usalama

Baada ya maji kuchujwa au kutibiwa, yanapaswa kuhifadhiwa vizuri. Kinyume na hayo yanaweza kuchafuliwa tena. Maji yanayohifadiwa katika matenki yenye mipasuko katika kuta zake yanaweza kutokuwa salama. Vivyo hivyo, vyombo vyenye mifuniko ambayo haijakaza, iliyotengenezwa vibaya au bila mifuniko kabisa haviwezi kuzuia maji kutochafuliwa tena na vijidudu vya magonjwa.

Matenki yaliyofunikwa ni salama zaidi katika kuhifadhi maji kuliko tenki zilizowazi kwa sababu mbuu na konokono hawawezi kuishi ndani ya vyombo vilivyofunikwa. Weka chombo cha kuhifadhi maji karibu na mahali maji hayo yanahitajika kutumika.

Maji yaliyohifadhiwa yanaweza pia kutokuwa salama tena yanapoguswa na vikombe vichafu, mikono michafu, yanapomiminwa kwenye chombo kichafu, au uchafu au vumbi vinapoingia kwenye maji hayo.

Ili kuzuia maji kutochafuliwa wakati yanapokuwa yamehifadhiwa:

chombo cha maji na kichoteo chenye mkono mrefu
  • Mimina maji nje bila kugusa mdomo wa chombo, au tumia kichoteo kisafi, chenye mkono mrefu kuchota maji hayo kutoka kwenye chombo.Usiruhusu kichoteo kugusa kitu chochote kingine, au kitachafua maji safi kitakapotumika tena.
  • Toa maji yote kwenye chombo na kusafisha na maji ya moto kila baada ya wiki 2 au 3.
  • Vyombo vitunzwe vikiwa vimefunikwa wakati wote.
  • Vyombo vya kunywea maji vitunzwe katika hali ya usafi wakati wote.
  • Kamwe usihifadhi maji kwenye vyombo ambavyo vimewahi kutumika kwa ajili ya viuatilifu au kemikali zenye sumu.
  • Usitibu kiasi kikubwa cha maji kuliko kiasi ambacho unahitaji kwa matumizi ya muda mfupi, pale inapowezekana. Kwa ajili ya kunywa na kuandaa chakula, mara nyingi zinahitajika angalau lita 5 kwa kila mtu kila siku.
NWTND was Page 25-2.png Vyombo vyenye mdomo mfinyu vinaweza kuzuia zaidi vijidudu vya magonjwa kuingia, na ndiyo salama zaidi kwa ajili ya kuhifadhi maji.

Maji safi, salama na ya kutosha kwa kila mtu

Afya njema hutegemea upatikanaji wa maji safi, salama naya kutosha. Hii inamaanisha kuwa haki yetu ya afya hutegemea hali yetu ya kupata maji. Japokuwa tunaweza kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti vyanzo vya maji, na kutibu maji ili yawe salama, afya yetu bado iko hatarini kama uchimbaji madini, michuruziko kutoa kwenye mbolea za kemikali na viuatilifu, au viwandani vitaendelea kuchafua vyanzo vyetu vya maji.

Serikali na jamii lazima zifanye kazi kwa pamoja kulinda, kuboresha, na kupanua mifumo ya ugavi wa maji ili kutoa maji safi, salama na ya kutosha kwa watu. Sekta binafsi huwa na hoja kwamba ikipewa mamlaka kamili ya kutoa huduma zote za maji, inaweza kutoa huduma bora kuliko serikali na kutengeneza faida pia. Huu ndiyo ubinafsishaji. Lakini mara nyingi kinachotokea ni kwamba baada ya kubinafsisha bei ya maji hupanda na kuwanyima watu wa kawaida haki ya maji yao. Hali hii huchangia matatizo makubwa ya kiafya, watu wanapolazimika kutumia maji kidogo kuliko mahitaji yao,au wanapolazimika kutafuta maji popote yanapoweza kupatikana bila malipo, pasipo kuzingatia usalama wake.

Kuhakikisha usalama wa afya ya watu na mazingira, tunahitaji mifumo ya maji kwa umaa ambayo inatoa maji safi, salama na ya kutosha kwa wote. Mifumo ya huduma ya maji inayodhibitiwa na jamii inaweza kusimamiwa kwa kuipa afya ya watu kipaumbele cha kwanza badala ya pesa.