Hesperian Health Guides

Lishe bora hutengeneza afya bora

HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Lishe bora hutengeneza afya bora

Katika sura hii:

Watu wazima 4, kijana na mtoto wakila mlo pamoja
Chakula hurutubisha miili na pia mahusiano yetu. Chakula huziweka familia na marafiki pamoja, na kuendeleza uhai wa tamaduni zetu
Kundi la wanawake wakiongea wakati wakipata chakula na vinywaji
Mvulana akimsaidia mtoto kula kutoka kwenye bakuli

Chakula cha kutosha na chenye virutubishi mbalimbali ni hitaji muhimu kwa afya bora. Chakula huipatia miili yetu nguvu na hutusaidia kujifunza na kufikiri vizuri. Chakula hutulinda dhidi ya maambukizi, huruhusu misuli yetu na viungo ndani ya miili yetu kufanya kazi vizuri, na huifanya ngozi yetu, nywele na meno kuonekana vizuri na kuwa imara.

Lakini siyo vyakula vyote hutufanya kuwa na afya bora zaidi. Vyakula ambavyo vimetengenezewa viwandani ambavyo wengi wetu hutegemea huwa na chumvi, mafuta na sukari nyingi kupita kiasi. Vyakula hivi ambavyo vimesindikwa kupita kiasi na hata kuchakachuliwa vinaweza kusababisha au kuchangia ongezeko la matatizo ya kiafya kama vile magonjwa ya moyo na kisukari.

Kuendelea kuwa na afya bora hutegemea kula chakula cha kutosha na mchanganyiko wa vyakula vyenye virutubishi