Hesperian Health Guides
Lishe bora hutengeneza afya bora: Madawa
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Lishe bora hutengeneza afya bora > Dawa za minyoo
Yaliyomo
Dawa za minyoo
Mebendazo
Mebendazo hufanya kazi dhidi ya safura, askarisi, mchangokiboko (trichuris au whipworm), na mchangouzi (pinworm au threadworm). Pia husaidia dhidi ya trikinosisi (trichinosis) lakini siyo sana. Ingawa kawaida haina madhara ya pembeni, mara chache huenda kukawa na maumivu tumboni au kuharisha iwapo mgonjwa ana minyoo mingi mwilini.
Epuka mebendazo wakati wa miezi 3 ya kwanza ya ujauzito kwa sababu inaweza kumuathiri mtoto aliyeko tumboni. Usitoe kwa mtoto mwenye umri chini ya mwaka 1.
Kutibu askarisi, mchangokiboko (whipworm au Trichuris) na safura (hookworm)
toa kidonge 1 cha miligramu 500, mara moja tu.
Kuzuia askarisi (roundworm) mahali ambapo imeenea
Kwa ajili ya trikinosisi (trichinosis)
Albendazo
Albendazo inafanana na mebendazo, lakini huwa ni ghali zaidi. Hufanya kazi dhidi ya safura, askarisi, trikinosisi, mchangokiboko (whipworm), na mchangouzi (pinworm au threadworm). Madhara ya pembeni ni nadra sana.
Epuka albendazo katika miezi 3 ya kwanza ya ujauzito kwani inaweza kumuathiri mtoto aliyeko tumboni. Usitoe kwa watoto chini ya mwaka 1.
Zaidi ya miaka 2: toa miligramu 400, mara 1. Rudia ndani ya wiki 2 kama itahitajika.
Kwa ajili ya trikinosisi (trichinosis)
Pamoti pirante (pyrantel pamoate), emboneti pirante (pyrantel embonate)
Pirante (pyrantel) hufanya kazi dhidi ya mchangouzi,safura,na askarisi, lakini inaweza kuwa ghali. Mara chache husababisha kutapika, kizunguzungu, au maumivu ya kichwa. Usitoe kwa mtu yeyote ambaye pia anatumia piperazini (piperazine)- dawa nyingine ya minyoo.
Kwa ajili ya safura na askarisi: toa dozi 1 tu.
Kwa ajili ya mchangouzi: toa dozi 1, subiri wiki 2, halafu toa dozi nyingine. Toa miligramu 10 kwa kila kilo. Kama huwezi kumpima mtu toa dozi kwa kuzingatia umri kama ifuatavyo:
Miaka hadi 5: toa miligramu 125 (½ kidonge cha miligramu 250).
Miaka 6 hadi 9: toa miligramu 250 (kidonge 1 cha miligramu 250 mg).
Miaka 10 hadi 14: toa miligramu 500 (vidonge 2 vya miligramu 250).
Zaidi ya miaka 14: toa miligramu 750 (vidonge 3 vya miligramu 250).
Kutibu mchangokamba (tapeworm)
Dawa ya praziquantel or niclosamide hutibu aina yote ya minyoo katika kundi la chango.Kama maambukizi ya mchangokamba yatakuwa yameufikia ubongo na kusababisha mashambulio, mgonjwa atahitaji albendazo na dawa za kudhibiti mashambulio, na msaada wa haraka.
Praziquantel
Praziquantel inaweza kusababisha uchovu, kizunguzungu,maumivu ya kichwa, kukosa hamu ya kula, na kichefuchefu, lakini madhara haya ni nadra pale dozi ndogo inapotumika kutibu mchangokamba.
Miaka 4 hadi 7: toa miligramu 150 (¼ kidonge), mara moja tu.
Miaka 8 hadi 12: toa miligramu 300, mara 1 tu.
Zaidi ya miaka 12: toa miligramu 600, mara 1 tu.
Kutibu mchangokamba fupi (H. nana)
Miaka 4 hadi 7: toa miligramu 300 hadi 600 (½ kidonge hadi kidonge 1) kwa kila dozi.
Miaka 8 hadi 12: toa miligramu 600 hadi 1200 kwa akila dozi.
Zaidi ya miaka 12: toa miligramu 1500 kwa kila dozi.
Niklosamaidi (niclosamide)
Dawa ya niclosamide hutibu maambukizi ya mchangokamba kwenye utumbo, lakini siyo vifuko vyenye viluwiluwi vya minyoo hiyo nje ya utumbo.
Tumia niclosamide baada ya kula mlo mdogo asubuhi. Vidonge vinapaswa kumumunywa vizuri na kumezwa. Dozi inaweza kutofautiana na aina ya mchangokamba. Hivyo, tafuta ushauri kutoka kituo cha afya eneo lako au kama hili haliwezekani tumia dozi ifuatayo:
Mumunya vizuri na kumeza dozi zifuatazo. Kama mtoto mdogo hawezi kumumunya, saga kidonge na kuchangaya na maziwa ya mama kidogo au chakula.
Miaka 2 hadi 6: toa gramu 1 (miligramu 1000), mara 1 tu.
Zaidi ya miaka 6: toa gramu 2, mara 1 tu.