Hesperian Health Guides

Dawa za mshituko wa moyo

Kama unahisi mtu anapatwa na mshituko wa moyo, mpe kidonge 1 cha aspirini mara moja (miligramu 300 hadi 325). Mwambie mgonjwa kukitafuna kidonge na kumeza kwa maji. Hata kama huna uhakika kwamba mtu ana mshituko wa moyo, asprini haitasababisha madhara yoyote. Mkiwa njiani kuelekea hospitalini, unaweza kumpa nitrogliserini (nitroglycerin) kama unayo.

Unaweza pia kumpa mofini (morphine) kusaidia kupunguza maumivu na wasiwasi, na kuurahisishia moyo kusukuma damu.

Nitrogliserini (nitroglycerine/glyceryl trinitrate)


Nitrogliserini hutumika kutibu maumivu kifuani kutokana na mshituko wa moyo. Husaidia kupanua mishipa ya damu na kurahisisha moyo kusukuma damu.

MuhimuNBgrnimportant.png

Usitoe nitrogliserini kwa mtu mwenye shinikizo la damu la chini au ambaye ametumia dawa ya Viagra ndani ya saa 24 zilizopita. Muunganiko wa dawa hizi unaweza kusababisha shinikizo la damu kushuka sana, na kusababisha mauti.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Inaweza kusababisha maumivu ya kichwa, kusikia joto au kizunguzungu.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png

Mpe ½ miligramu (0.5 miligramu) iyeyushwe chini ya ulimi, kila dakika 5. Lakini usitoe zaidi ya mara 3 ndani ya dakika 15.