Hesperian Health Guides

Dawa za vidonda kutokana na kuungua

Huduma ya kwanza: Madawa

Vidonda kutokana na kuungua vinauma sana. Mpe dawa ya kupunguza maumivu yenye nguvu kama vile kodeini (codeine) AU mofini (morphine), hasa kabla ya kukisafisha kidonda au kubadilisha pamba au bandeji au vifaa vilivyofunga kidonda.

Majeraha ya kuungua yanaweza kupata maambukizi. Hivyo toa antibiotiki kama vile dikloksasilini (dicloxacillin), kilindamaisini (clindamycin), sefaleksini (cephalexin), AU sipro (ciprofloxacin) kama kuna dalili ya maambukizi.

Kadri kidonda kinavyoendelea kupona, mpe dawa kutoka kundi la antihistamini kama vile klorofeniramini (chlorpheniramine) AU difenhidramini (diphenhydramine) kupunguza mwasho.

Mpe chanjo ya tetanasi kama ratiba yake ya chanjo za tetanasi siyo kamilifu (angalia Chanjo – inaandaliwa).

Kama mtu alikuwa kwenye moto na kumeza moshi mwingi, dawa ya salbutamo (salbutamol) inaweza kumsaidia aweze kupumua vizuri.