Hesperian Health Guides

Vyoo vya kiikolojia

Katika sura hii:

Vyoo vya kiikolojia hugeuza kinyesi na mkojo kuwa kirutubisho na mbolea kwa udongo. Utaratibu huu huboresha afya ya watu na mazingira kwa kuzuia ueneaji wa vijidudu na kubadili taka hatari kuwa rasilimali muhimu.

Vyoo vya kiikolojia pia hulinda na kutunza maji kwa sababu hakuna maji yanayohitajika kwa ajili ya matumizi yake, isipokuwa maji ya kunawa. Vyoo hivi ni salama zaidi kwa maji yaliyoko chini ya ardhi kuliko vyoo vingine kwa sababu hujengwa juu ya ardhi, au hutumia mashimo mafupi.

Vyoo vya kiikolojia vinaweza kujengwa katika maeneo ya mjini na hata vijijini. Kawaida huhitaji matunzo zaidi kuliko vyoo vya kawaida vya shimo, lakini matumizi kidogo ukilinganisha na vyoo vya kumwaga maji kuondoa kinyesi. Ni muhimu kwa watu kufundishwa jinsi vinavyofanya kazi.

Kugeuza taka kuwa mbolea

Udongo mzuri wenye rutuba huhitaji mboji-ambayo ni mabaki ya mimea na viumbe hai vingine baada ya kufa na kuoza.

Illustration of the below: Arrows from an ear of corn, to a woman eating, to a person in a toilet shelter, to a woman farming, to a crop of corn.
Udongo wenye rutuba huzalisha mazao bora
Mbolea hurutubisha udongo
Mazao huwa chakula
Kinyesi kinaweza kugeuzwa kuwa mbolea
Chakula hugeuka kuwa taka kutoka mwilini (kinyesi)
Choo cha kiikolojia hugeuza kinyesi kuwa rasilimali.

Wakulima hutengeneza mboji kutokana na mabaki ya chakula na kinyesi cha mifugo na kuiweka kwenye udongo mashambani. Hii husaidia udongo kuwa na virutubisho vya kutosha kwa ajili ya kuotesha mazao. Kama vile watu wanavyohitaji virutubisho kutokana na chakula ili kuwa na nguvu na afya, mimea pia inahitaji virutubisho kwenye udongo ili kukua na kutoa matunda.

Mbolea inaweza pia kutengenezwa kutokana na kinyesi cha binadamu. Kinyesi cha binadamu kina virutubisho ambavyo vinaweza kutumika kuboresha udongo. Lakini kinyesi pia kina vijidudu ambavyo vinaweza kusababisha magonjwa.

Kwa sababu hii, utengenezaji wa mbolea kutokana na kinyesi cha binadamu huhitaji uangalifu zaidi kuliko utengenezaji wa mbolea kutokana na kinyesi cha mifugo, mabaki ya vyakula, mimea na vitu vya asili ya kijani.

Kinyesi kamwe kisitumike kingali kibichi. Lakini baada ya kufanyika kuwa mbolea, kinaweza kutumika kuotesha chakula, miti, na mazao mengine bila nyongeza ya mbolea zenye kemikali.

Mkojo una vijidudu kiasi ukilinganisha na kinyesi lakini una virutubisho zaidi kuliko kinyesi. Hali hii huufanya kuwa salama zaidi kushughulikia, na muhimu zaidi kama mbolea. Lakini mkojo ni mkali mno kutumika moja kwa moja kwenye mimea kama mbolea. Huhitaji kushughulikiwa kwanza kwa utaratibu maalum kama ilivyoelezwa chini ya mbolea kutokana na mkojo.

Vyoo vyenye mfumo wa kutengeneza mbolea na vyoo kavu vyenye mfumo wa kuchepusha mkojo

Kuna aina kuu mbili za vyoo vya kiikolojia: vyoo vya kutengeneza mbolea kutokana na kinyesi na vyoo kavu vinavyochepusha mkojo. Vyoo hivi vyote vinaweza kutengeneza mbolea salama na watu wengi huvichukulia kuwa vya aina moja tu - vyoo vya kutengeneza mboji. Hata hivyo vinatofautiana kwa njia kuu kadha:

Vyoo vya kutengeneza mbolea kutokana na kinyesi

  • Kinyesi na mkojo huenda kwenye chombo, kama vile shimo fupi au tanki kubwa la zege ambalo haliwezi kuvuja na kuchafua maji yaliyo chini ya ardhi.
  • Mtumiaji huongeza mchanganyiko wa vitu vikavu kama vile majani, vumbi la mbao, maranda, udongo na jivu kila mara anapomaliza kujisaidia. Hii hupunguza harufu mbaya na kurahisisha mchanganyiko wa taka kuvunda na kutengeneza mbolea.
  • Vijidudu vya magonjwa na mayai ya minyoo vitakufa baada ya miezi kadhaa.
  • Baada ya mchanganyiko kukaa muda wa kutosha wa kuweza kuua vijidudu katika kinyesi (wastani mwaka mmoja), mabaki makavu hupakuliwa kwa ajili ya matumizi kama mbolea.

Vyoo kavu

  • Mkojo huhifadhiwa katika sehemu tofauti na kinyesi. Hukusanywa, kutengenezwa na kutumika kama mbolea.
  • Kinyesi huelekezwa kwenye chombo, kama vile tanki la zege au chombo cha plastiki nzito ambacho hakiwezi kuvuja na kuchafua maji chini ya ardhi.
  • Mtumiaji huongeza udongo ukiwa umechanganyika na majani makavu na majivu` kwenye shimo kila baada ya kujisaidia. Hii husaidia kupunguza harufu na kinyesi kukauka haraka.
  • Kinyesi kamwe hakichanganyiki na maji. Mchanganyiko mkavu utaua sehemu kubwa ya vijidudu, yakiwemo mayai ya minyoo.
  • Kinyesi huhifadhiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, hadi kitakapokuwa kama udongo uliokauka.

Kwa aina zote mbili za vyoo, mchanganyiko wa kinyesi utakuwa tayari kupangwa katika marundo ya mbolea, kupandia mti, au kuchanganywa kwenye udongo shambani kwa ajili ya kuoteshea mazao.

Choo cha kawaida cha kutengeneza mbolea kwa ajili ya kupandia mti

Choo kiki hutengeneza mbolea kwa ajili ya kupanda miti. Ni rahisi kujenga, na huwa na kijumba ambacho kinaweza kutolewa kinapojaa.

Choo hiki kinafaa sana katika sehemu zenye nafasi ya kutosha na mahali ambapo watu wana nia ya kupanda miti. Pia ni muhimu mahali ambapo kuna tabaka maji la karibu na usawa wa ardhi kwa sababu shimo lake huwa ni fupi. Kufukia choo kilichojaa na udongo na kupanda mti hapo husaidia mchakato wa kinyesi kutengeneza mbolea.

Hii ni njia nzuri ya kuanzisha bustani ya miti ya matunda au miti mingine yenye faida. Hata hivyo, kama hutarajii kupanda miti, unaweza kuchagua aina nyingine ya choo.

A woman plants a small tree between a toilet shelter and some larger trees.

Jinsi ya kujenga choo rahisi kwa ajili ya kupanda mti

Safisha eneo na kulaza bimu la zege mahali unapotaka kukiweka choo. Ndani ya bimu, chimba shimo la kina cha mita 1. Weka vizuri bimu hiyo mahali pake. Tengeneza jukwaa na kuliweka juu ya shimo na bimu. Jenga kijumba au kibanda chepesi kwa ajili ya kumstiri mtumiaji, ambacho ni rahisi kuhamishiwa sehemu nyingine pale shimo litakapojaa.

Matumizi na utunzaji

Women work together to move a toilet shelter over a platform and pit.
  • Kabla ya kutumia, weka ndani ya shimo majani makavu. Hii itasaidia kuharakisha mabadiliko ya kinyesi kuwa mbolea.
  • Mwaga kiganja kimoja cha udongo uliochanganywa na majivu au majani makavu kila mara baada ya kutumia.
  • Rundo ndani ya shimo linapokuwa kubwa sana, koroga au sambaza kwa kutumia mti.
  • Fagia na kusafisha jukwaa au sakafu mara kwa mara. Kuwa mwangalifu maji mengi yasiingie kwenye shimo.
  • Shimo linapokaribia kujaa, ondoa kijumba, jukwaa au sakafu na bimu.
  • Jaza shimo na tabaka la sentimeta 15 za udongo uliochanganywa na mimea.
  • Baada ya wiki kadhaa, taka hizo zitatulia. Ongeza udongo zaidi na mimea, maji na kupanda mti. Miti ya matunda huota vizuri na kuzaa matunda mengi.
EHB Ch7 page 128-1.png
1 mita
30 cm
1 mita

Vyoo vya kutengeneza mbolea vyenye matundu mawili

Choo chenye matundu mawili cha kutengeneza mbolea kinafanana na choo cha kawaida cha kutengeneza mbolea kwa ajili ya kupanda mti. Lakini badala ya kupanda mti kwenye shimo hilo, mbolea hiyo hupakuliwa na kutumika bustanini au shambani.

Choo hiki huwa ni salama zaidi kwa maji yaliyoko chini ya ardhi kuliko choo cha kawaida cha shimo kwa sababu kinyesi huchanganyika na udongo kwenye shimo fupi, huruhusiwa kukauka na kuua vijidudu vya magonjwa, na baadaye kuondolewa.

Kujenga choo cha kutengeneza mbolea chenye matundu mawili

Chimba mashimo 2 yenye kina cha mita 1 hadi 1.5, mita 1 upana na sentimeta 30 kati ya mashimo hayo. Jenga bimu kwenye mashimo yote mawili. Weka jukwaa au sakafu na kijumba chepesi juu ya shimo moja, na mfuniko wa zege au mbao juu ya shimo la pili. Tumia shimo la kwanza hadi litakapokaribia kujaa. Familia yenye watu 6 itajaza shimo hilo katika kipindi cha mwaka mmoja kwa wastani.

  1. Shimo la kwanza litakapokaribia kujaa, jazia na sentimeta 30 za udongo na kufunika kwa mfuniko wa mbao au zege. Hamisha jukwaa na kijumba kwenye shimo la pili. Tumia hadi litakapokaribia kujaa.
  2. Woman shoveling compost into a wheelbarrow.
    Baada ya mwaka mmoja, taka kwenye choo cha kutengeneza mbolea chenye matundu mawili zinafaa kuwa tayari kuchanganya na udongo shambani kama mbolea. Lakini bado ni muhimu kuvaa mipira ya mikononi na viatu wakati wa kushughulikia mbolea hiyo.
  3. Acha shimo la kwanza likae tu. Au baada ya kukaa kwa miezi miwili, ongeza udongo na kupanda mbogamboga za msimu kama vile nyanya kwenye shimo. Kwa sababu mchakato wa ubadilishaji taka ndani ya shimo kutengeneza mboji bado unaendelea, ni muhimu kuepuka mazao ambayo huota chini ya ardhi kama vile karoti na viazi.
  4. Baada ya shimo la pili kujaa, pakua shimo la kwanza kwa kutumia chepe. Vaa mipira ya mikononi na kunawa mikono baada ya kushughulika na mbolea hiyo.
  5. Tunza mbolea kavu hiyo kwenye mifuko iliyo wazi na ndoo kwa ajili ya matumizi ya baadaye, au rundika sehemu moja, au tumia shambani. Ili kujua iwapo mbolea hiyo ni tayari kutumika, inapaswa kuwa imekaa sehemu kavu kwenye shimo au sehemu nyingine iliyotengwa angalau kwa mwaka mmoja. Inatakiwa kuwa imekauka vizuri, na haitoi harufu kali.

Utunzaji wa choo cha kutengeneza mboji chenye matundu mawili

  • Weka ndoo yenye udongo uliyochanganywa na majani makavu au vumbi la mbao kwenye kijumba cha choo. Kila baada ya kutumia choo, mwaga angalau kiganya kimoja ndani ya tundu.
  • Shimo linapokaribia kujaa, sambaza kwa kutumia mti.
  • Fagia na kusafisha jukwaa mara kwa mara. Kuwa mwangalifu ili usiruhusu maji mengi kuingia kwenye shimo.

Vyoo vya kuchepusha mkojo

Vyoo vikavu havihitaji mashimo ila hujengwa juu ya ardhi kurahisisha upakuaji wa mbolea iliyoko ndani. Pia vina chombo mahali pa kujisaidia chenye sehemu mbili ambazo hutenganisha kinyesi na mkojo. Hali hii huruhusu taka kwenye choo kubaki kavu, vijidudu vya magonjwa kufa na harufu kupungua. Pia huruhusu mkojo kutumika kama mbolea. Kwa sababu hujengwa juu ya ardhi na chini yake kimesakafiwa, choo kikavu ambacho kimejengwa vizuri hakichafui maji yaliyoko ardhini.

Gharama ya kujenga choo kikavu ni kubwa zaidi kuliko choo cha shimo la kawaida. Matumizi yake sahihi pia yanahitaji mafunzo kwa sababu hufanya kazi kwa njia tofauti na vyoo vya shimo vya kawaida, au vyoo vya kumwaga maji. Pia matunzo yake mazuri yanahitaji juhudi kubwa. Lakini ni muhimu sana kwa watu ambao wanataka kutengeneza mbolea kutokana na taka zao. Pia aina hii ya vyoo ndiyo inayofaa zaidi katika maeneo yenye:

  • Tabaka maji ikiwa karibu sana na hivyo kutofaa vyoo vya shimo.
  • Kukumbwa na mafuriko mara kwa mara.


  • Mwamba au udongo mgumu kwa ajili ya uchimbaji wa vyoo vya kawaida.
  • Mahitaji ya choo cha kudumu ndani au karibu na nyumba.

Vyoo vikavu vyenye chemba mbili

Aina hii ya choo kikavu ina sehemu (chemba) mbili mahali ambapo kinyesi hubadilika na kuwa mbolea salama. Sehemu moja hutumika kama choo wakati kinyesi kinabadilika na kukauka katika sehemu ya pili. Chombo maalum mahali pa kujisaidia hutenganisha mkojo na kinyesi. Mkojo hupita kwenye mpira kuelekea kwenye chombo maalum nje ya choo. Baada ya mwaka mmoja, mbolea kavu huondolewa na kurundikwa sehemu moja, au hutumiwa, moja kwa moja, bustanini au shambani. Mkojo uliokusanywa unaweza kuchanganywa na maji na kutumika kama mbolea.

Sehemu za choo kikavu chenye chemba mbili

EHB Ch7 page 129-1.png
Mbele ya choo
Nyuma ya choo
Kibanda au kijumba juu ya choo kwa ajili ya faragha na kutunza choo kikiwa kavu.
Chombo cha mkojo mahali mkojo hukusanyika kutoka chooni na kwenye sehemu ya haja ndogo.
Chemba mbili ambazo zimetengenezwa kutokana na matofali, kokoto au rasilimali nyingine ngumu. Wakati chemba moja inatumika kama choo, nyingine itakuwa inatumika kwa ajili ya kubadilisha kinyesi kuwa mbolea.
Sehemu ya haja ndogo
Chombo kwa ajili ya kujisaidia ambacho hutenganisha mkojo na kinyesi. Chombo hiki kinaweza kutengenezewa nyumbani na kufanya kazi vizuri
Milango midogo ya nyuma kwa ajili ya kuondoa kinyesi kilichokauka.
Mpira wa kuchepusha mkojo kutoka kwenye chombo cha haja ndogo cha wanaume na chombo cha wanawake kuelekea kwenye dumu au chombo kingine cha kuuhifadhi.
Njia tatu za kujenga choo kikavu

Njia zote 3 zinahusisha sehemu ya msingi ambayo imejengwa kwa kokoto, matofali, au rasilimali yoyote nyingine isiyopenya maji. Sehemu ya msingi ina sehemu zingine zifuatazo:

EHB Ch7 Page 130-1.png
Chemba mbili
Milango miwili midogo
Bomba la kutolea harufu
Tundu kwenye bomba
Tundu kila upande au mbele kwa ajili ya mpira wa kuchepusha mkojo ukitokea kwenye chemba.
Katika njia zote 3, jenga kijumba au kibanda na ngazi. Funga milango nyuma. Funga mpira wa kuchepusha mkojo kupitia tundu kwenye sehemu ya msingi hadi kwenye chombo, shimo, au bustanini kurutubisha udongo.
AINA YA VYOO: 1. Kwa ajili ya kuchuchumaa
EHB Ch7 Page 130-2.png
2. Kwa ajili ya kukaa kama vile kwenye dawati
EHB Ch7 Page 130-7.png
3. Au kwa ajili ya kukaa kwenye kikalio kama vile kwenye vyoo vinavyotumia maji
EHB Ch7 Page 130-12.png
KUJENGA CHEMBA ZA MSINGI
EHB Ch7 Page 130-3.png
EHB Ch7 Page 130-8.png
EHB Ch7 Page 130-8.png
Acha nafasi katika ukuta unaotenganisha kwa ajili ya kuweka chombo cha kukusanyia mkojo kutoka sehemu zote mbili. Funika chemba la msingi na mfuniko wa mbao au zege kukiwa na tundu juu ya kila chemba Funika chemba la msingi na mfuniko wa mbao au zege kukiwa na tundu juu ya kila chemba
KUCHEPUSHA MKOJO
EHB Ch7 Page 130-4.png
EHB Ch7 Page 130-09.png
EHB Ch7 Page 131-13.png
Kata kitako cha dumu la lita 20. Funga kwa kulipindua juu -chini katika nafasi ilioachwa inayotenganisha chemba hizo mbili. Funga bomba kwa ajili ya kuchepusha mkojo, ukihakikisha hakuna mvujo kati ya dumu na bomba. Weka wavu juu ya dumu kuzuia kinyesi na vitu vingine kuingia ndani Kata kitako cha dumu. Funga bomba kwenye mdomo wa dumu kuchepusha mkojo. Weka wavu juu ya dumu ili kuzuia kinyesi na vitu vingine kuingia. Vikalio vya choo kinachochepusha mkojo vinaweza kujengwa au kununuliwa kutoka baadhi ya maduka ya vifaa vya ujenzi. Vikipatikana, ni rahisi kufunga na kutumiwa.
KUKAMILISHA CHEMBA LA MSINGI
EHB Ch7 Page 131-5.png
EHB Ch7 Page 131-10.png
EHB Ch7 Page 131-14.png
Kata tundu refu kwa ajili ya kuchuchumaa kwenye sakafu au jukwaa, na dumu lililofungwa juu - chini likiwa katikati. Mkojo utakwenda kwenye dumu na kinyesi kwenye chemba chini ya kila mwisho wa tundu. Funika nusu ya shimo, juu ya chemba ambayo haitumiki. Funga kichepusha mkojo mbele ya kila tundu. Weka vikalio juu ya matundu hayo. Weka kikalio cha kuchepusha mkojo juu ya tundu moja wapo na kufunika tundu lingine hadi litakapokuwa tayari kutumika.
KUJENGA KIJUMBA/ KIBANDA
EHB Ch7 page 131-6.png
jagi
EHB Ch7 page 131-11.png
bomba
EHB Ch7 Page 130-15.png
Mko hukusanywa kwenye chombo na kutumika kama mbolea...au kupitishwa kwenye bomba na kuelekezwa kwenye shimo maalum la kunyonya maji taka.

Jinsi ya kutumia na kutunza choo kikavu chenye chemba mbili

EHB Ch7 page 132-1.png
Bandika taarifa za kuwasaidia watu kutumia choo kwa usahihi na jinsi ya kukitunza.
Mwaga maji kidogo kwenye chombo cha haja ndogo na kichepusha mkojo kila baada ya kujisaidia ili kudhibiti harufu.
Chemba ambayo haitumiki ifunikwe.
Chombo mahali pa kujisaidia haja ndogo kinaweza kutengenezwa kutokana na dumu au jagi la plastiki, na kuunganishwa na bomba la kupeleka mkojo kwenye chombo maalum au shimoni.
Karatasi
Kichepusha mkojo kitunzwe kwa usafi. Iwapo kimeziba, kiondoe, ukisafishe na kukirudisha.
Iwepo ndoo yenye mchanganyiko wa udongo, jivu na majani makavu. Kila baada ya kujisaidia, mwaga viganja viwili ndani ya tundu kavu la choo. Halafu rudishia mfuniko.


  • Hakikisha hakuna maji yanayoingia katika sehemu ya chemba inayohifadhi kinyesi.
  • Iwapo taka ndani ya choo zitaloa, mwaga majani makavu.
  • Iwapo choo kinatoa harufu kali, ongeza majani na mimea mingine mikavu, na kuhakikisha bomba la kutolea harufu halijaziba.
  • Iwapo rundo la kinyesi litakuwa kubwa sana, tumia mti kukirudisha chini.
  • Chombo cha kukusanyia mkojo kinapojaa, uondoe na kuutumia kutengeneza mbolea.
  • Chemba moja inapojaa, tumia chemba nyingine. Kumbuka kufunika chemba ambayo haitumiki.
  • Ni bora kuruhusu kinyesi kukaa na kutulia kwa mwaka mmoja kabla ya kukiondoa. Baada ya mwaka mmoja, au baada ya chemba ya pili kujaa, ondoa mabaki yote kwenye chemba ya kwanza na kurudia utaratibu.

Usiweke taka zozote zingine kwenye choo

EHB Ch7 page 133-1.png
Usitumbukize taka chooni

Ili vyoo vya kiikolojia viweze kufanya kazi vizuri, vinapaswa kutumika tu kwa ajili ya taka zinazotoka kwenye mwili wa binadamu. Wanawake katika hedhi wanaweza kutumia vyoo vya kiikolojia kwa usalama. Hata hivyo, vitambaa vya hedhi na bidhaa zingine wanazotumia hazipaswi kutumbukizwa kwenye vyoo.

Vyoo vya kiikolojia haviwezi kutengeneza mbolea kutokana na bidhaa ambazo haziwezi kuoza, kama vile makopo, chupa, plastiki, vitambaa vya nailoni au kiasi kikubwa cha karatasi. Ni sahihi kutumia kiasi kidogo cha karatasi, majani, vumbi la mbao, na mabaki ya mimea mengine, kwa sababu vitu hivi huoza ndani ya udongo.

Lini mbolea kutokana na kinyesi itakuwa tayari kutumika?

Mabaki ndani ya choo kavu yatakuwa tayari kutolewa baada ya kukauka na harufu kupungua sana au kupotea kabisa. Ili kufikia hatua hii, mabaki ndani ya choo yanapaswa kutunzwa kwa ukavu ndani ya chemba ya choo kwa mwaka mmoja.

Kama unafikiri kuwa mabaki hayo yako tayari kutolewa, fungua chemba. Kama rundo bado lina unyevunyevu, ongeza majani makavu au udongo uliochanganywa na jivu na kuruhusu mabaki yakae kwa wiki kadhaa. Iwapo rundo ni kavu na hakuna harufu kali, sasa tayari kutumika kama mbolea. Pakua kwa kutumia chepe.

EHB Ch7 page 133-2.png
Ondoa mabaki yaliokauka kwa ajili ya matumizi kama mbolea.
EHB Ch7 page 133-3.png
Ni muhimu kuvaa mipira ya mkononi na viatu wakati unaposhughulikia taka kutoka mwili wa binadamu, na kunawa vizuri na sabuni baada ya kupakua chemba ya choo.

Baada ya kukauka kwa mwaka mmoja, sehemu kubwa ya vijidudu vya magonjwa vitakuwa vimekufa na rasilimali hiyo itakuwa tayari kuchanganya na udongo shambani kama mbolea. Lakini kama kuna walakini, rasilimali hiyo inaweza kuhifadhiwa kwanza katika viroba au ndoo zikiwa wazi kwenye sehemu kavu.

Mbolea kutokana na mkojo

Baadhi ya wakulima hutumia mkojo uliochanganywa na maji kama mbolea kwa sababu mkojo una virutubisho kama vile nitrojeni na fosforasi ambavyo husaidia mimea kuota vizuri. Mkojo ni salama zaidi kushughulikia kuliko kinyesi. Lakini vile virutubisho muhimu ambavyo huupa sifa ya kuwa mbolea nzuri ndivyo huweza kuchafua vyanzo vya maji.

Pia mkojo unaweza kuwa na vijidudu vya minyoo ya damu. Kwa sababu hii, ni muhimu kuepuka kuingiza mkojo kwenye vyanzo vya maji.

Kutengeneza mbolea ya kawaida kutokana na mkoj

Hifadhi mkojo kwenye chombo kilichofunikwa kwa siku kadhaa. Hii itaua vijidudu vyote kwenye mkojo, na kuzuia virutubisho kutorokea hewani.

Ili kutengeneza mbolea, changanya vipimo vitatu vya maji na kipimo kimoja cha mkojo. Unaweza kutumia mbolea hii kwa mimea angalau mara 3 kwa wiki

Sw EHB Ch7 page 134-1.png
Jagi 2 za maji + jagi 1 ya mkojo = mbolea salama

Mimea iliyorutubishwa na mbolea ya mkojo inaweza kustawi vizuri kama vile mimea iliyotumia mbolea ya kemikali ya viwandani. Mimea inayotoa majani yanayoliwa kama vile spinachi, mchicha, matembele na mbogamboga nyingine za kijani huota vizuri zaidi kwa mbolea inayotokana na mkojo. Kila mara nawa mikono yako kwa maji na sabuni baada ya kugusa mkojo.

Kutengeneza mbolea chachu kutokana na mkojo

Kuchanganya mboji na mkojo na kuacha mchanganyiko huo kuoza na kuchachuka hutengeneza udongo mzuri kwa ajili ya mazao.

  1. Chukua mkojo kutoka kwenye vyoo kavu. Kwa kila lita ya mkojo, ongeza kijiko kimoja cha udongo au mboji.
  2. Acha mchanganyiko huo ukae wazi kwa wiki 4. Hii itatoa harufu mbaya, hivyo tengenezea mbali na watu. Mchanganyiko huo wa mkojo utachachuka na kugeuka rangi ya udongo.
  3. aza chombo kikubwa na mabaki ya mimea makavu, mfano majani makavu, vumbi la mbao, maranda nk. Tandaza chombo na plastiki ili kutoruhusu uvujaji wa maji kupitia chini ya chombo hicho.
  4. Jaza mkojo uliochachuka. Kiwango kizuri ni vipimo 7 vya majani kwa kipimo 1 cha mkojo.
  5. Funika kwa tabaka la udongo la sentimeta 10, halafu panda miche au mbegu.
  6. Mwagilia kila baada ya siku 2 na mchanganyiko wa kipimo 1 cha mkojo na vipimo10 vya maji. (Huo ni mchanganyiko dhaifu kwa sababu utatumika katika chombo kilichofunikwa, tofauti na bustani au shamba lililo wazi). Mabaki makavu ya mimea yatabadilika na kuwa udongo wenye rutuba katika kipindi cha miezi 10 hadi 12.

Udongo huo mpya unaweza kutumika kwa ajili ya kupandia mazao.

Vyoo vikavu vilivyoboreshwa na kurekebishwa kukidhi mazingira mapya

Vyoo katika moduli hii ni mifano michache tu ya vyoo vya kiikolojia. Vinaweza kuboreshwa na kurekebishwa kukidhi mahitaji ya jamii mbalimbali. Baadhi ya mambo ambayo yatasaidia choo kikavu kufanya kazi vizuri ni pamoja na:

EHB Ch7 page 135-1.png
  • Joto la jua - husaidia taka (kinyesi) kubadilika haraka. Jenga choo ili milango ya chemba iangalie jua, na paka milango yote rangi nyeusi. Hii itasaidia milango kupokea joto, kuboresha mzunguko wa hewa, na kuua vijidudu haraka.
  • Mzunguko zaidi wa hewa - pia utasaidia taka kubadilika haraka. Kutandaza miti na mabaki mengine ya mimea, kwa ndani chini ya chemba kabla ya kutumika, husaidia mzunguko wa hewa kupita kwenye kinyesi na hivyo kukauka haraka.

Choo chenye sehemu ya kunawia na bustani ya kunyonya maji taka

Watu wa India wamekifanyia choo kikavu marekebisho ili kuruhusu mkojo na maji taka, baada ya kunawa, kutiririka na kunyonywa na mimea katika eneo maalum la karibu.

EHB Ch7 page 135-2.png
Ndoo ya jivu
Unawaji hufanyika juu ya tundu ambalo huelekeza maji taka kwenye eneo lililopandwa majani.
Maji ya kunawa
Tundu kwa ajili ya kinyesi
Tundu kwa ajili ya mkojo
Eneo lililopandwa mimea mahali ambapo maji taka na mkojo hutiririkia. Eneo hilo hujazwa mchanga na kifusi na kupandwa mafunjo au majani mengine, na mimea isiyo ya kula. Mimea inapokua sana hupunguzwa na kutupwa chooni.
Chemba chini ya choo zimetandikwa na majani makavu kabla ya kuanza kutumika, ili kunyonya maji maji na kutengeneza mahali pazuri kwa ajili ya utengenezaji wa mbolea. Kila mara choo kinapotumika, kiganja 1 au 2 vya udongo au jivu humwagwa ndani. Kila baada ya muda, majani makavu pia huongezwa kusaidia ukaushaji na ubadilikaji wa kinyesi katika mchakato wa kutengeneza mbolea. Baada ya mwaka 1 wa matumizi, chemba ya kwanza hufunguliwa na mbolea kutolewa na kurundikwa, au kutumiwa moja kwa moja shambani kwa ajili ya kupandia mazao.


Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Juni 2022