Hesperian Health Guides
Huduma ya vyoo katika hali ya dharura
HealthWiki > Mwongozo wa jamii juu ya afya ya mazingira > Sehemu ya kwanza: Ujenzi wa vyoo na matumizi yake > Huduma ya vyoo katika hali ya dharura
Katika sura hii:
Watu wengi hulazimika kuishi katika mazingira ya dharura kutokana na vita, majanga ya asili (mfano mafuriko na kimbunga) na sababu nyingine zinazowalazimisha kuyahama makazi yao kwa muda. Katika makazi ya dharura kama vile makazi ya wakimbizi, huduma ya vyoo inapaswa kupewa kipaumbele sawa na huduma zingine za msingi.
Choo rahisi cha handaki
Handaki za kawaida zinaweza kutengenezwa kwa kutumia vifaa vilivyopo. Handaki moja iliyozungushiwa ua au uzio, kwa ajili ya familia moja au kundi dogo la familia itakidhi haja katika mazingira hayo.
Vyoo vya handaki vinatakiwa kujengwa chini ya miinuko na mbali na vyanzo vya maji, lakini karibu na makazi ya familia ili watu wasitembee muda mrefu kufuata huduma hiyo.
Choo cha handaki huwekewa ngazi kwa ajili ya kuweka miguu. Choo kinaweza kuwa na kina cha karibu mita 2 au zaidi, ingawa kinaweza kupungua kama hakuna nguvu kazi. Kila mtumiaji amalizapo humwaga udongo kidogo juu ya kinyesi chake. Handaki inapokaribia kujaa, hufukiwa kabisa na udongo. Miti na mimea hufaidi kutokana na udongo weye rutuba.
Kijumba au kibanda chepesi kinachohamishika kinaweza kuwekwa juu ya handaki ili kutoa faragha na kukinga watumiaji dhidi ya mvua na jua. Badala ya milango, pazia zinaweza kutengenezwa kutokana na kitambaa, mijeledi, au vifaa vingine vilivyopo. Hata hivyo, juhudi zaidi zifanyike kuhakikisha kwamba vyoo hivi ni salama kwa wanawake na watoto.
