Hesperian Health Guides

Kuchagua aina ya choo inayokufaa

Katika sura hii:


Kuchagua aina ya choo inayokufaa

Hakuna aina moja ya choo inayofaa sehemu zote, na kila aina ya choo ina nafasi ya kuboreshwa zaidi. Lengo la zoezi hili ni kusaidia watu kutafakari juu ya aina za vyoo zilizopo na kuchagua ipi inayowafaa.

EHB Ch7 page 138-1.png

Muda: Saa 1 hadi 2.

Vifaa: Karatasi ndogo za kuchorea, karatasi kubwa za kuchorea, kalamu za rangi au kalamu za wino mzito na gundi ya karatasi.

 1. Wezesha watu kuingia katika vikundi vidogo, kila kikundi watu 5 au 6. Kila mtu achore picha ya kila aina ya choo au njia ya kujisaidia wanayojua. Wachore vyoo vyao wenyewe, vingine ambavyo wamewahi kuona, na hata picha njia ambazo watu hutumia mahali ambapo hakuna vyoo. Lengo ni kuchora vyoo vyote vilivyopo, kuanzia vile ambavyo ni rahisi zaidi hadi vyoo vya kisasa zaidi.

 2. Picha zinapokuwa tayari, kila kikundi kipange picha zake kwa utaratibu wakianza na njia za kujisitiri ambazo ni mbaya zaidi hadi njia ambazo wanadhani ni bora zaidi. Picha zote zibandikwe kwenye katarasi pana kwa kutumia gundi.

 3. Kila kikundi kionyeshe picha zake na kueleza sababu za mpangilio waliouchagua. Mambo gani yanafanya mfumo mmoja kuwa bora zaidi au mbaya? Kila mwana kikundi pia aeleze mfumo gani anaoutumia nyumbani na upi angetamani kuwa nao?

 4. Baada ya kila mtu kuonyesha picha zake, kikundi kijadili tofauti kati ya njia zote. Uliza maswali kama vile:
  • Je, watu wote wanakubaliana juu ya mfumo ambao ni mbaya zaidi na upi ni bora zaidi?
  • Je, upo mfumo ambao unaonekana kumfaa kila mtu? Ni kwa sababu za kiafya, gharama, au sababu yoyote nyingine?
  • Je, ipo mifumo ya vyoo ambayo hakuna mtu yoyote ndani ya kikundi anayeitumia? Kwa nini?
  Hii inaweza kuelekeza kwenye mjadala juu ya sababu za upendeleo wa watu wa mifumo Fulani ya vyoo.
  • Je, ni manufaa gani ya kiafya ambayo ni muhimu zaidi?
  • Manufaa gani ya kimazingira ni muhimu zaidi?
  • Maboresho ambayo watu wanataka yatahitaji mabadiliko yoyote katika kaya au jamii, au watu wanafikiria nini juu ya usafi kuhusiana na huduma ya vyoo? Je yapo mambo rahisi ambayo yanaweza kufanyika kuboresha mifumo iliyopo?
  • Kama kikundi kinajumuisha wanawake na wanaume, je majibu yao ni tofauti?

 5. Sw EHB Ch7 page 139-1.png
 6. Tambulisha vyoo vingine ambayo huenda watu hawajui.Hii inaweza kujumuisha mabadiliko madogo kwa vyoo vyao vya sasa kama vile mabomba ya kutolea harufu, au aina mpya ya choo (inaweza kujumuisha mifano ambayo imetolewa katika moduli hii, na mingine ambayo unaweza kuwa unaijua). Kikundi kijadili mawazo hayo mapya.
 7. Sw EHB Ch7 page 139-2.png


 8. Wezesha mjadala juu ya njia hizo mbalimbali, ukiwaomba wanakikundi kutafakari maswali kwenye jedwali. Kila mtu atoe mawazo yake juu ya manufaa na mapungufu ya kila choo, kwa kutumia tarakimu kuonyesha nguvu ya azma yake. Kwa mfano, 5 kumaanisha bora na 0 mbaya zaidi. Andika alama ambazo kila mtu anatoa kwenye jedwali na hesabu ili kujua njia ambayo inachukuliwa kuwa bora zaidi.
 9. a group of men and women sit and talk.
  Mawasiliano kati ya wanawake na wanaume ni sehemu muhimu ya mchakato wa kuchagua vyoo salama ambavyo vinakidhi pia kanuni za afya.


 10. Kikundi kichore picha mpya kulingana na matokeo ya majadiliano juu ya manufaa na njia mpya ambazo wamejifunza. Wabandike picha mpya na za zamani kwenye karatasi pana kwa mpangilio wakianza na mifumo mibaya zaidi kuelekea mifumo bora zaidi. Hatimaye, walinganishe mpangilio mpya na wa zamani.
  • Kuna tofauti gani?
  • Ni mawazo au taarifa gani ambazo zilisababisha watu kubadili msimamo wao juu vyoo vibaya zaidi na vyoo bora zaidi?
  Kwa msingi wa mjadala huu, kikundi kinaweza kuamua juu ya choo au maboresho gani ambayo yanawafaa zaidi.Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Juni 2022