Hesperian Health Guides

Baadhi ya tabia za msingi ambazo huchangia maambukizi ya magonjwa yanayohusiana na kinyesi

Katika sura hii:

  • Kunywa maji yasiyochemshwa
  • Kula chakula (yakiwemo matunda) kilichoandaliwa katika mazingira machafu ambacho kinaweza kuwa kimechafuliwa na vimelea vya magonjwa hayo.
  • Kutembea pekupeku.
  • Kutonawa mikono kwa sabuni kila baada ya kutoka chooni
  • Kula au kugusa chakula bila kunawa mikono kwa maji safi na sabuni.
  • Kujisaidia hovyonje ya choo, karibu na vyanzo vya maji na visima, na utupaji vinyesi hovyo.


Sw EHB Ch7 page 144-1.png


Kinga ni bora kuliko tiba. Hivyo, ni wajibu wa kila mtu kutumia choo kwa usahihi, kunawa mikono kwa maji safi na sabuni baada ya kutumia choo, na kuzingatia kanuni za afya na usafi kwa ujumla ili kulinda afya yake na ya wengine.



Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Juni 2022