Hesperian Health Guides

Aina ya vyoo

Katika sura hii:

Hakuna aina moja ya choo ambayo inafaa kwa kila jamii na kila kaya. Hivyo ni muhimu kuelewa faida ya kila aina ya choo. Vyoo vilivyounganishwa kwenye mifumo ya maji taka kwa ajili ya kinyesi ni vigumu kujenga. Kwa sababu hiyo, moduli hii inaelezea tu vyoo ambavyo vinatumia maji kidogo au havitumii maji kabisa.

Vyoo ambavyo hutumia maji kidogo au havitumii maji kabisa

EHB Ch7 page 118-1.png
EHB Ch7 page 118-2.png
EHB Ch7 page 118-3.png
Vyoo vya kawaida vyenye uwezo wa kutengeneza mboji kwa ajili ya kupandia miti:
Vyoo hivi vinafaa mahali ambapo watu wanataka kupanda miti na wanaweza kumudu choo kinachohamishika.
Choo kinachotenganisha mkojo na kinyesi:
Choo hiki kinafaa zaidi mahali ambapo watu wako tayari kutumia mbolea inayotokana na kinyesi cha binadamu, na mahali ambapo tabaka maji ipo karibu na usawa wa ardhi, au eneo linaloathiriwa sana na mafuriko.
Choo cha kutengeneza mbolea kutokana na kinyesi chenye chemba mbili
Hiki nacho kinafaa mahali ambapo watu wako tayari kutumia mbolea inayotokana na kinyesi.
EHB Ch7 page 118-4.png
EHB Ch7 page 118-5.png
EHB Ch7 page 118-6.png
Choo cha kumwaga maji kuondoa kinyesi:
Hiki kinafaa zaidi mahali ambapo tabaka maji ipo chini sana ardhini, na mahali ambapo watu hutumia maji kutawazia.
Choo cha shimo chenye bomba la kutolea harufuchoo cha VIP<br? Kinafaa zaidi katika maeneo yenye tabaka maji ikiwa mbali na usawa wa ardhi na maeneo yasioathiriwa na mafuriko. Choo cha kawaida kilichofunikwa
Choo hiki kinafaa zaidi mahali tabaka maji ipo mbali na usawa wa ardhi.

Angalizo: Michoro hii inaonyesha vyoo bila milango na bila mifuniko kwenye matundu ili msomaji uweze kuona ndani vikoje. Vyoo vyote vinapaswa kuwa na milango na matundu ya vyoo yafunikwe wakati yanapokuwa hayatumiki. Vile vile, vyoo vinapaswa kutengenezwa kwa njia inayorahisisha kila mtu katika jamii kuvitumia.

Mahali panapofaa kujenga choo

 Illustration of the below: Toilet shelter with arrows showing distance to river, spring box and well.
zaidi ya mita 20 kutoka kwenye mto
zaidi ya mita 20 kutoka kwenye chemchemi iliyoboreshwa
zaidi ya mita 20 kutoka kwenye kisima

Wakati wa kufanya maamuzi ya kujenga choo, hakikisha kwamba hutachafua visima au maji yaliyopo ardhini. Hatari ya maji ya ardhini kuchafuliwa inategemea na hali ya mahali husika, mfano aina ya udongo, hali ya unyevunyevu na umbali wa tabaka maji kutoka usawa wa ardhi.

Lakini maelekezo ya msingi yafuatayo yanaweza kusaidia kuhakikisha usalama:

  • Kina cha shimo kama ni choo cha kawaida, au chenye chemba ya kubadili kinyesi kutengeneza mbolea, kinapaswa kuwa angalau mita mbili na nusu juu ya tabaka maji.
  • Kama wakati wa kuchimba shimo la choo utakuta ardhi ina maji maji, au kama shimo litajaa maji, hivi ni viashiria kuwa sehemu hiyo haifai kuchimba choo.
  • Kumbuka kuwa wakati wa msimu wa mvua, tabaka maji huwa juu kuliko wakati wa kiangazi. Usijenge vyoo sehemu ambayo kawaida hukumbwa na mafuriko.
  • Kama kuna uwezekano wa kuchafua maji yaliyoko chini ya ardhi kutokana na choo, unaweza kujenga choo kilichoinuliwa juu ya ardhi.
  • Kawaida maji ya chini ya ardhi hutiririka kutoka eneo lenye usawa wa juu kuelekea usawa wa chini. Iwapo utalazimika kujenga choo mahali penye hatari ya kuchafua maji chini ya ardhi, basi choo kijengwe chini ya mwinuko kutoka kwenye visima vilivyopo karibu.
Village with arrows showing placement of pit toilet and well.
Taka zenye kinyesi zikiingia kwenye mkondo wa maji chini ya ardhi kutoka shimo la choo
Maji ya kisima kwa ajili ya kunywa
Visima vinapaswa kujengwa kwenye miinuko na vyoo chini yake kwa sababu maji chini ya ardhi hutiririka kutoka miinuko kwenda chini yake.

Vyoo vya shimo vilivyofunikwa

A shelter over a closed pit toilet.

Choo cha aina hii kina jukwaa lenye tundu na mfuniko wa kufunikia pale linapokuwa halitumiki. Jukwaa linaweza kutengenezwa kwa mbao, kokoto au magogo yaliyofunikwa kwa udongo. Jukwaa zilizotengenezwa kwa kokoto na saruji huzuia maji kupenya na hudumu kwa miaka mingi. Choo cha shimo kilichofunikwa kinahitaji kufungwa bimu au kuwekewa kingo za kuzuia jukwa lisibomoke na kuzama shimoni. Soma “Jinsi ya kutengeneza jukwaa imara la choo”.

Choo cha shimo kilichoboreshwa na bomba la kutolea harufu, kwa jina maarufu VIP, hutumia bomba la kupitishia hewa kupunguza harufu na nzi.

Tatizo la choo cha shimo ni kwamba pale kinapojaa, hakiwezi kutumika tena. Ili kutumia vizuri shimo lililojaa mbolea inayotokana na kinyesi, inashauriwa kupanda mti mahali hapo. Kabla ya kuupanda mti, ondoa jukwaa au sakafu, bimu na ukingo uliotumika kwa ajili ya uimarishaji, pamoja na kijumba chake. Halafu funika kinyesi kwa udongo, kiasi cha sentimita 30, uliochanganywa na mabaki makavu ya mimea. Iache sehemu hiyo kwa miezi kuruhusu taka hizo kutulia. Baada ya hapo, ongeza udongo zaidi na kupanda mti.

Njia nyingine ni kuongeza udongo mara kwa mara wakati choo kinaendelea kutumika na kukiacha kwa miaka 2 ili kinyesi kiweze kubadilika kuwa mbolea. Baadaye toa mbolea hiyo, na endelea kutumia choo kama kawaida. Kila mara nawa mikono yako kwa sabuni baada ya kushika na kuchimba udongo kwenye vyoo au karibu yake.

Kutengeneza choo cha shimo kilichofunikwa

1. Chimba shimo mita 1 upana na angalau mita 2 kwenda chini.
EHB Ch7 page 120-2.png
2. Panga na kujenga matofali, mawe, kokoto au malighafi nyingine inayofaa juu ya shimo la choo ili kutoa msingi imara kwa ajili ya jukwaa na kulinda shimo lisibomoke. Bimu ya kokoto iliyosukwa inaweza kufaa zaidi.
EHB Ch7 page 120-3.png
3. Tengeneza jukwaa na kijumba cha kuweka juu ya shimo. Jukwa la saruji na kokoto au mawe ni imara zaidi lakini unaweza kutumia vifaa vyovyote vilivyopo kama magogo, mabanzi na udongo. Ukiamua kutengeneza jukwa la magogo, tumia miti ambayo haiozi haraka.
EHB Ch7 page 120-4.png


Jinsi ya kutengeneza jukwaa imara la choo

Jukwaa imara la choo litadumu miaka mingi. Mfuko mmoja wa saruji wa kilo 50 unaweza kutengeneza majukwaa 4 ya vyoo, au 2 na bimu za mzunguko 2. Pia utahitaji waya za kusuka bimu na jukwaa, matofali na mbao pana kwa ajili ya kujenga bimu na kubeba zege. Utahitaji pia kifaa cha mbao kilichotengenezwa kwa umbo la tundu la ufunguo kwa ajili ya tundu la choo. Majukwaa yanaweza kuwa na muundo wa pembe nne zinazolingana, au muundo wa mduara.

1. Tandaza chini sehemu tambarare shuka la plastiki au mifuko ya saruji iliyotumika. Juu yake, tengeneza ukingo wa matofali au mbao wenye sentimeta 120 urefu, sentimeta 90 upana na setimeta 6 kina.
EHB Ch7 page 121-1.png
2. Weka kile kifaa cha mbao chenye m u u n d o wa tundu la ufunguo katikati ili kulipa sura tundu la choo. Unaweza pia kutumia matofali kuziba tundu, na kutengeneza muundo wa tundu baada ya kumwaga zege.
EHB Ch7 page 121-2.png
3. Tengeneza zege kwa kuchanganya kipimo kimoja cha saruji, vipimo kama hivyo 2 vya mchanga, na maji ya kutosha kulainisha zege liweze kushikamana vizuri. Mwaga zege kwenye sehemu ya jukwaa iliyotengenezwa hadi ijae nusu.
EHB Ch7 page 121-3.png
4. Weka waya zenye unene wa milimita 3 juu ya zege ambalo bado laini. Tumia waya 4 hadi sita zikitanda kila sehemu ya zege hiyo. Tengeneza vishikizio vya waya zenye unene wa milimita 8 hadi 10, na kuvifunga kwenye zege karibu na kona zote.
EHB Ch7 page 121-4.png
5. Mwaga zege lililobaki na kusawazisha kwa kutumia ubao.
EHB Ch7 page 121-5.png
6. Ondoa kifaa chenye umbo la tundu la ufunguo pale zege litakapoanza kukauka (baada ya saa 3). Kama ulitumia kifaa cha tofali, ondoa matofali na kutengeneza shimo la umbo la tundu la ufunguo. Funika zege na magunia yaliyoloweshwa na maji, au kitambaa kilicholowa au hata shuka la plastiki usiku mzima hadi kesho yake. Lowesha jukwaa hilo kila siku, kwa siku saba ili liweze kuimarika taratibu hadi litakapokuwa imara kabisa.
7. Baada ya zege kukauka na kuwa imara kabisa, weka jukwaa juu ya shimo. Ili kuimarisha zaidi shimo hilo, zungushia bimu. 8. Tengeneza mfuniko kwa ajili ya tundu la choo kwa kutumia zege au mbao. Mfuniko unaweza kuwa na kishikio, au unaweza kusogezwa kwa mguu ili kuepuka kuchafua mikono na vijidudu vya magonjwa.

EHB Ch7 page 121-6.png

Jinsi ya kuboresha jukwaa

Kwa sababu vijidudu na minyoo vinaweza kujikusanya karibu na tundu la choo, tengeneza sehemu mahsusi ya kukanyaga na miguu ili kupunguza matatizo ya kiafya.

Kama watu watapenda kukaa, tengeneza tundu la mduara na sehemu ya kukalia ya zege.

Vyoo vya shimo vyenye bomba la kutolea harufu na kuzuia nzi (vip)

EHB Ch7 page 123-1.png

Hiki ni choo cha kawaida cha shimo lililofunikwa lakini kimeboreshwa ili kupunguza harufu na nzi.

Jinsi choo cha VIP kinavyofanya kazi

Upepo hupita juu ya bomba la kupitishia hewa chafu na kuondoa harufu. Kijumba cha choo huleta giza ndani na kulazimisha nzi walioko chooni shimoni kuelekea kwenye mwanga juu ya bomba la kutolea harufu. Nzi hawa hunaswa kwenye wavu juu ya bomba na kufariki.

Jinsi ya kutengeneza choo cha VIP

  1. Chimba shimo lenye kina cha mita 2 na mita 1.5 upana. Jenga mdomo wake kwa matofali au bimu inayolingana na upana wa shimo. Iwapo kijumba chake kitakuwa kizito sana (chenye matofali, au mbao nzito), jengea shimo lote isipokuwa chini yake. Acha matobo au mianya katika kuta za matofali ili kuruhusu majimaji kutoka nje.
  2. EHB Ch7 page 123-2.png
    Tundu kwa ajili la bomba la kutolea harufu liwe na ukubwa unaolingana na bomba lenyewe.
  3. Tengeneza jukwaa au sakafu lenye mita 1.5 kwa mita 1, likiwa na matundu mawili. Tundu la pili likiwa pembezoni kwenye jukwaa ni kwa ajili ya bomba la kutolea harufu. Tundu la bomba hili liwe angalau sentimeta 11 kwa upana
  4. Jenga kijumba juu ya shimo na jukwaa lake
  5. Funga bomba la kutolea harufu kwenye tundu lake na kukaza vizuri. Bomba lipakwe rangi nyeusi ili liweze kufyonza joto na kuboresha upitishaji hewa. Funika mdomo wa bomba hilo kwa wavu wa kuzuia mbu (wavu wa alminiamu au chuma utadumu zaidi). Simamisha bomba kufikia urefu wa angalau sentimeta 50 juu ya paa la choo ili kuruhusu upepo kunyonya harufu hiyo mbaya.

Jinsi ya kutumia na kutunza choo cha VIP

EHB Ch7 page 123-3.png
Iwapo wavu juu ya bomba utachanika au kuchomoka, rudishia mara moja.
  • Funika tundu la choo wakati linapokuwa halitumiki.
  • Hakikisha chumba cha choo kinabaki na giza.
  • Tunza usafi wa choo na kusafisha sakafu mara kwa mara.


Iwapo bomba la kutolea harufu litaziba kutokana na utando wa buibui au na vitu vingine, mwaga na kupitisha maji ndani yake.

Matatizo ya vyoo vya VIP

Vyoo vya VIP vinaweza kuwa na matatizo haya:

  • Kama ndani ya kijumba hakutakuwa na giza, nzi hawataruka na kupanda ndani ya bomba la kutolea harufu wakifuata mwanga juu.
  • Iwapo kijumba hakitakuwa na paa, hakuna udhibiti wa nzi.
  • Iwapo wavu juu ya bomba utakuwa umechanika, hakutakuwa pia na udhibiti wa kutosha wa nzi.



Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Juni 2022