Hesperian Health Guides

Sehemu ya pili: Utunzaji wa huduma ya maji ya jamii

HealthWiki > Mwongozo wa jamii juu ya afya ya mazingira > Sehemu ya pili: Utunzaji wa huduma ya maji ya jamii

Katika sura hii:

EHB Ch9 Page 161-1.png


Maji ni muhimu sana kwa uhai. Binadamu, wanyama na mimea vyote vinahitaji maji ili kuishi na kukua. Hata hivyo, katika sehemu nyingi watu hawana maji ya kutosha. Watu wengi hulazimika kutembea umbali mrefu ili kupata maji. Na mara nyingi, maji yanayopatikana siyo salama kwa ajili ya kunywa.

Baada ya kusoma sehemu ya pili, utakuwa umejifunza:
  1. Jinsi ya kuboresha, kuhifadhi na kutunza chanzo cha maji - kisima, chemchemi, bomba na maji ya mvua.
  2. Njia mbalimbali za kutibu na kusafisha maji.


Jamii inapokuwa na chanzo cha maji ambacho ni salama na karibu na watu, kila mtu ana fursa nzuri ya kuwa na afya njema. Iwapo wanawake na wasichana wataepushwa na kazi ngumu ya kubeba maji kila siku na shughuli za kuhakikisha kuwa maji hayo ni safi na salama, watapata muda zaidi wa kujiendeleza kielimu, kujumuika katika shughuli mbalimbali za jamii zao, na hata kupumzika. Hali hii itasaidia ustawi wa jamii kwa ujumla.

Jamii ikiwa na maji salama ya kutosha, hatari ya magonjwa yanayohusiana na maji yaliyochafuliwa itapungua.


Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Jan 2024