Hesperian Health Guides

Kufanya maji yawe salama kwa ajili ya kunywa

Katika sura hii:

Ni bora kutunza na kutumia chanzo salama cha maji, kama vile chemchemi au kisima kilichojengwa kuliko kutibu na kutumia maji ambayo yametoka kwenye chanzo kilichochafuliwa, kama vile mto au kisima cha asili. Lakini maji kutoka chanzo chochote yanahitaji kutibiwa kama yamechafuliwa na iwapo watu wanaweza kukataa kuyanywa kutokana na rangi au ladha yake, au kama yamechotwa na kuhifadhiwa nyumbani. Hata maji kutoka kwenye bomba, tenki na visima yatahitaji kutibiwa kabla ya kunywa endapo yamechafuliwa.

Njia utakayoichagua kwa ajili ya kutibu maji itategemea:

 • kiasi cha maji unayohitaji,
 • yamechafuliwa na nini,
 • jinsi gani utayatunza baada ya kuyatibu, na
 • ni vifaa na rasilimali gani nyingine ulizonazo.


Bila kuzingatia njia gani utatumia kuyatibu, la msingi ni kuruhusu maji yakatulia ndipo baadaye kumimina kwenye chombo kingine, au kuyachuja kabla ya kuyatibu. Hii itasaidia kuondoa uchafu, hali ambayo hurahisisha na kuchangia tiba kamili.

Njia zinazoelezewa hapa hazikidhi kusafisha maji yenye kemikali za sumu. Maji yenye kemikali zenye sumu hayawezi kuwa salama kwa ajili ya kunywa, kuoga au hata kufulia nguo. Yanaweza kusababisha saratani, magonjwa ya ngozi, mimba kuharibika na matatizo mengine ya kiafya.

Ili kufanya maji yawe salama kutokana na vijidudu vya magonjwa, unaweza kutumia njia mbili zifuatazo - kwanza chuja maji hayo, halafu yatibu.

1. Acha maji yatulie kwa saa chache na kisha mimina katika chombo safi au yachuje.

EHB Ch6 Page 92-1.png

Chujio la kitambaa
…au…
EHB Ch6 Page 92-2.png
Chujio la mkaa
Mchanga
Mkaa
Mchanga wenye punje kubwa
Maji yaliyochujwa


2. Baada ya uchujaji, tibu maji hayo kwa kutumia moja ya njia zifuatazo:

EHB Ch6 Page 92-3.png
EHB Ch6 Page 92-4.png
EHB Ch6 Page 92-5.png
EHB Ch6 Page 92-6.png
Kuchemsha maji au… Kutumia klorini au… Kutumia mionzi ya jua au… Kuchanganya na maji ya matunda ya limao


Ruhusu maji yatulie

Maji yanapotulia huruhusu uchafu, vitu, vijidudu na minyoo isababishayo magonjwa kushuka na kutua chini kwenye chombo. Pia kuhifadhi maji kwa siku 5 hadi 6 hupunguza kiwango cha vimelea kwenye maji. Lakini baadhi ya vimelea havifi kwa njia hii. Hivyo tumia njia nyingine ya kutibu maji hayo baada ya maji kutulia, kwa mfano kuchuja, kutumia klorini, njia ya mionzi ya jua au kuchemsha.

Njia ya vyombo vitatu

Njia ya vyombo vitatu vya maji huwezesha maji kutulia na vimelea pamoja na uchafu mwingine kushuka chini. Njia hii ni salama zaidi kuliko ile ya kutumia chombo kimoja. Hata hivyo, njia hii haitoi uhakika wa usalama wa maji. Njia hii ya kutumia vyombo vitatu inapaswa kufuatiwa na tiba ya maji kwa dawa.

EHB Ch6 Page 93-1.png
EHB Ch6 Page 93-2.png
EHB Ch6 Page 93-3.png

Siku ya kwanza asubuhi: Jaza maji chombo kimoja. Funika na kuacha yatulie kwa muda wa siku mbili.

Siku ya pili asubuhi: Jaza chombo cha pili na maji, funika na acha yatulie kwa siku mbili. Uchafu katika chombo cha kwanza utakuwa umeanza kutulia chini.

Siku ya tatu asubuhi: Mimina maji kutoka katika chombo cha kwanza kwenda chombo cha tatu ambacho hakina kitu, huku ukiacha uchafu ulio chini ya maji. Maji katika chombo cha tatu sasa yako tayari kwa ajili ya kutiwa dawa. Uchafu ulio katika chombo cha kwanza sasa unaweza kumwagwa. Safisha chombo cha kwanza na kijaze tena maji. Kifunike na ukiache kwa muda wa siku 2 (Maji haya yatatolewa yakiwa tayari kutiwa dawa siku ya 5).

Siku ya nne asubuhi: Ondoa maji yaliyotulia kutoka chombo 2 kwenda chombo cha 3 kwa ajili ya kutibiwa. Safisha chombo cha pili na kijaze tena maji.

Kila baada ya siku chache safisha vizuri chombo cha 3 kwa maji ya moto. Kuwa mwangalifu katika kumimina maji kutoka chombo kimoja hadi kingine ili kutovuruga tena uchafu uliotulia chini.

Kuchuja maji

Kuna njia nyingi za kuchuja maji ili yaweze kuwa salama zaidi. Baadhi ya njia hizo huhitaji vifaa maalum. Njia zingine zinahitaji vifaa vya kawaida vyenye uwezo wa kuchuja kwa urahisi kiasi cha maji kidogo au kikubwa kabla ya kutibiwa.

Chujio la kitambaa

2 women wearing saris filter water through a cloth into a container.

Nchini India na Bangladesh, kitambaa chenye nyuzi zilizofumwa kwa karibu hutumika kuchuja maji na kuondoa vijidudu vya kipindupindu. Kwa sababu vijidudu vya kipindupindu kawaida hujibanza kwenye vimelea vidogo viishivyo kwenye maji, kuchuja maji na kuondoa vimelea hivyo vilevile huondoa sehemu kubwa ya vijidudu vya kipindupindu. Njia hii pia huondoa aina ya minyoo ambayo hujulikana kama guinea worms.

Unaweza kutengeneza chujio la kitambaa kutokana na kitambaa cha kawaida kitambaa kilichotengenezwa kutokana na pamba, au kitambaa kingine kinachofaa. Ili kutumia chujio la kitambaa:

 1. Acha maji yatulie kwenye chombo ili uchafu uzame chini.
 2. Kunja kitambaa mara 4 na kinyooshe au kifunike mdomo wa chombo cha maji au birika.
 3. Mimina maji polepole kutoka kwenye chombo cha kwanza kupitia kitambaa kwenda kwenye chombo cha pili.

Tumia upande huo huo wa kitambaa au vinginevyo vimelea vitaingia kwenye maji. Baada ya kutumia kitambaa, kisafishe na kuacha kikauke juani. Mionzi ya jua itaua vimelea ambavyo vinaweza kuwa vimebaki kwenye kitambaa. Wakati wa msimu wa mvua, takasa kitambaa kwa dawa isiyo na madhara ya kuua wadudu, au piga pasi. Hakikisha usafi wa chombo unachotumia kuhifadhia maji yaliyochujwa angalau kila baada ya wiki 2.

Chujio la seramiki

Chujio la seramiki linaweza kutengenezwa kutokana na udongo wa mfinyanzi uliokandwa na kuchomwa kwa moto, na kupakwa utando wa madini ya chuma yenye uwezo wa kuua wadudu. Chujio hili linaweza kutengenezwa na mfinyanzi yoyote aliyepitia mafunzo ya msingi.

EHB Ch6 Page 94-2.png
Mfuniko wa plastiki
Chujio la seramiki lenye utando wa madini ya chuma ndani yake
Ndoo ya plastiki
Koki ya plastiki
Chujio la seramiki ndani ya ndoo ya plastiki


Jinsi ya kutengeneza chujio la maji linalotumia mkaa

Chujio hili linaweza kutengenezwa kwa urahisi na huondoa karibu vijidudu vyote vya magonjwa katika kiasi kidogo cha maji.

Vifaa: Ndoo mbili za chuma au plastiki, nyundo na msumari mkubwa mmoja au miwili, ndoo ya mchanga wenye punje kubwa (siyo mchanga wa baharini) na robo ndoo ya mkaa wa kawaida.

 1. Toboa matundu chini ya ndoo moja na kuisafisha. Hii sasa ndiyo ndoo ya kuchujia.
 2. Safisha mchanga kwa kuuloweka na kuusuza kwenye maji; rudia na mwaga maji hadi maji yatakapoonekana safi.
 3. Saga mkaa wa kawaida kutokana na miti ili uwe vipande vidogo. Usitumie mkaa uliotengenezewa viwandani au kutokana na malighafi nyingine kwani mara nyingi una sumu ndani yake.
 4. EHB Ch6 Page 95-1.png
  Ndoo yenye chujio
  Uwazi sentimeta 10
  Mchanga
  Sentimeta 8 mkaa
  Sentimeta 5 mchanga wenye punje kubwa
  Vijiti kwa ajili ya ndoo kukalia
  Ndoo kwa ajili ya kupokea maji masafi yaliyochujwa
 5. Weka tabaka la mchanga uliosafishwa lenye kina cha sentimeta 5 ndani ya ndoo ya kuchujia na mimina maji juu yake. Kama maji hayatatiririka, panua zaidi matundu. Kama mchanga utapita, matundu ni makubwa sana. Na hii ikitokea ondoa mchanga, tandaza kitambaa laini juu ya matundu, halafu badilisha mchanga.
 6. Weka tabaka la mkaa uliopondwa la setimeta 8 juu ya mchanga. Halafu ongeza mchanga kwenye ndoo hadi ufikie sentimeta 10 kutoka usawa wa juu wa ndoo.
 7. Weka vibao viwili juu ya ndoo ya pili na kalisha ndoo yenye chujio juu ya vibao hivyo. Mimina maji safi kupitia ndoo ya kuchujia mara kadhaa hadi maji yanayoingia kwenye ndoo ya chini ya kukusanyia yatakapoonekana masafi. Sasa chujio liko tayari kutumia.
 8. Ili kutumia vizuri chujio hili, ruhusu maji uliyokusanya kutulia kwanza kabla ya kumiminwa ndani ya chujio. Maji ya kunywa hukusanywa kwenye ndoo safi ya chini. Kwa usalama zaidi, maji yaliyochujwa, yatibiwe kwa kutumia njia mojawapo iliyopendekezwa.


Kwa sababu vijidudu ambavyo vimechujwa vitaanza kuota kwenye mkaa, ni muhimu kuuondoa mkaa na kuusafisha kila baada ya chujio kutumika, au kama chujio limekaa siku kadhaa bila kutumika.

Chujio linalotumia mchanga

Chujio hili ni miongoni mwa njia salama, imara na yenye gharama nafuu ya kuchuja maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Chujio hili linaweza kusafisha maji ya kutosha kwa ajili ya familia ndogo (hadi lita 50 kwa siku).


Jinsi ya kutengeneza chujio la nyumbani kwa kutumia mchanga

 1. Safisha tenki, pipa au chombo cha lita 200 na baada ya hapo kutakasa kwa kutumia dawa salama. Hakikisha tenki hili halikuwahi kutumika kuhifadhi kemikali zenye sumu.
 2. Toboa tundu eneo la urefu wa theluthi tatu kutoka juu ya pipa kwenda chini kwa ajili ya kufunga koki. Tundu lazima litosheleze ukubwa wa koki itakayofungwa.)
 3. Funga koki kwenye tundu hilo na kukaza vizuri. Kama chombo au tenki ni ya matofali, basi saruji itumike kukazia vizuri koki kwenye tundu.
 4. Andaa bomba la mpira. Toboa matundu madogo madogo katika sentimeta 35 za mwanzo, ziba mwisho na kuulaza mpira chini ya tenki au chombo ukiwa umeviringishwa, matundu yakiangalia chini.
 5. Unganisha ncha ya mpira ambayo haikutobolewa na koki. Funga vizuri kwa kutumia nyaya au vyuma vingine vya kukazia mpira.
 6. Weka tabaka la kokoto la sentimeta 7 chini ya pipa au tenki likiwa limefunika mpira wa kupokea maji. Funika tabaka la kokoto na kitambaa laini na kujaza pipa au tenki na tabaka la mchanga safi wa sentimeta 10 chini ya koki. Baada ya hapo, tandaza kitambaa kingine laini juu ya tabaka la mchanga.
 7. Tengeneza mfuniko wa pipa au chombo, katikati ukiwa na tundu la kuingiza maji. Weka jiwe lenye umbo tambarare, au chombo chochote mithili ya sahani, chini ya tundu ili kuzuia mchanga usitibuliwe na maji yanayomwagwa ndani ya chombo au pipa.
 8. Safisha chujio mara kadhaa kwa kumwaga maji ndani na kuyaruhusu kupita hadi yatakaposafishika. Hii ni ishara kwamba chujio ni safi na tayari kuanza kutumika.
EHB Ch6 Page 96-1.png
Chombo chenye ujazo wa lita 200
Mfuniko
Jiwe lenye umbo tambarare
Mchanga safi
Kokoto safi
Mimina maji hapa ndani
Koki
Kitambaa laini
Mpira unaokunjika wenye milimita 20

Jinsi ya kutunza chujio la maji la mchanga

Baada ya siku chache za matumizi, utando wa kijani utaota juu ya mchanga. Utando huu husaidia kutibu maji, hivyo usiondolewe. Mchanga daima ufunikwe na maji. (Hii ndiyo sababu bomba linawekwa juu ya mchanga). Jaza chujio kila siku na kutumia maji kidogo kidogo. Kama chujio litakaushwa kabisa, halitafanya kazi vizuri na litahitaji kusafishwa tena na kujazwa.

Kabla ya kumimina maji kwenye chujio, ruhusu maji kutulia na uchafu mzito kutuama chini ya chombo. Maji hayo yatakuwa safi kiasi kabla ya kumiminwa kwenye chujio na hivyo kupunguza kazi ya kusafisha chujio. Maji yamiminwe kwenye chujio kama poromoko - hii husaidia kuongeza hewa kwenye maji na kuboresha ladha yake.

Maji kutoka kwenye koki yanapopungua, hii ni fursa ya kusafisha chujio. Ondoa maji yote pamoja na tabaka la kijani, na kiasi cha sentimeta moja ya mchanga kutoka juu. Baada ya chujio kutumika muda mrefu pale, zaidi ya nusu ya tabaka la mchanga utakuwa umeondolewa, badilisha tabaka zima la mchanga, na kokoto na kujaza upya. Hii inaweza kuhitajika mara moja au mbili kwa mwaka.

Chujio la kupunguza madini ya sumu ya Aseniki kwenye maji

Kuchuja madini ya aseniki kutoka kwenye maji, weka chombo kilichojaa misumari ndani ya chujio la mchanga-kwa juu. Tumia kilo 3 mpaka 5 za misumari - yenye urefu mdogo kabisa. Usitumie misumari iliyopakwa kinga ya kuzuia kutu kwa sababu misumari lazima iote kutu ili chujio liweze kufanya kazi. Madini ya chuma ya aseniki hujibanza kwenye kutu ya misumari na kuondolewa kutoka kwenye maji ya kunywa.

Kutibu maji

Tiba ya maji husaidia kuua vijidudu vya magonjwa na minyoo, na hivyo kuyafanya maji kuwa salama kwa ajili ya kunywa. Njia bora zaidi ya kutibu maji ni kuchemsha, kutumia klorini na mionzi ya jua.

MUHIMU! Njia hizi haziwezi kutakasa maji yenye kemikali zenye sumu kuwa salama.

Kuchemsha maji

A woman squats to stir a pot over a fire.
Chemsha maji hadi yatokote kwa dakika 1 ili kuua vijidudu vya magonjwa na kuyafanya kuwa salama kwa ajili ya kunywa.

Chemsha maji hadi yatokote kabisa. Pale yanapoanza kuchemka, acha yatokote angalau kwa dakika moja kabla ya kuepua jikoni na kuacha yapoe. Katika sehemu za milimani, maji yanahitaji kutokota angalau kwa dakika 3 ili kuua vijidudu vya magonjwa, kwani huanza kutokota mapema kuliko kawaida.

Kuchemsha maji hubadili ladha ya maji. Baada ya maji yaliyochemshwa kupoa, mimina kwenye chupa au ndoo na kutikisa kwa nguvu. Utikisaji huongeza hewa kwenye maji na hivyo kuboresha ladha yake.

Pale ambapo kuni ni adimu, uchemshaji wa maji unaweza kuwa mgumu. Inashauriwa kuchemsha maji ya kunywa baada ya kupika chakula, lakini moto wa jiko ungali na nguvu. Hii ni njia mojawapo ya kupunguza matumizi ya kuni.

Kutibu maji kwa klorini

Matumizi ya klorini ni njia yenye gharama nafuu na huweza kuua sehemu kubwa ya vijidudu vya magonjwa kwenye maji ya kunywa. Lakini, kiasi kidogo cha klorini hakiwezi kuua vijidudu hivyo; na kiasi kikubwa mno huyafanya maji kuwa na ladha mbaya. Klorini kawaida hutumika kutibu maji katika miradi ya maji kwa jamii kwa sababu ni vigumu kwa kaya moja moja kutibu maji yake wakati wote. Ili kutumia klorini kwa matumizi ya nyumbani, fuata maelekezo kwenye ukurasa 50.

Kiwango kikubwa cha klorini kina madhara kwa watu na mazingira. Hivyo, ni muhimu kufuata maelekezo ya wataalam katika kutibu maji kwa kutumia klorini.

Kiasi gani cha klorini kitumike?

Kiasi cha klorini kinachohitajika kutibu maji hutegemea na hali ya uchafu kwenye maji. Mathalan maji yana vijidudu wa aina gani na kiasi gani? Klorini hutumika kadri ya wingi wa vijidudu kwenye maji. Ni muhimu kutumia klorini ya kutosha ili nyingine iweze kubaki kwenye maji baada ya vijidudu kuuawa. Klorini inayobaki kwenye maji huitwa klorini ya akiba, na kazi yake ni kuangamiza vijidudu vipya vitakavyoingia kwenye maji. Maji yaliyo na klorini ya akiba huwa na harufu na ladha kidogo ya klorini. Hii ni ishara kwamba maji hayo sasa ni salama kwa ajili ya kunywa. Hata hivyo, klorini ikizidi harufu na ladha ya maji huwa kali na maji hunyweka kwa tabu.

Ili kutumia kiwango sahihi cha klorini, unahitaji kujua nguvu ya dawa yako ya klorini. Klorini husambazwa katika mifumo tofauti - gesi, poda, vidonge na majimaji. Kwa vile klorini inayotumika nyumbani mara nyingi ni ya maji, moduli hii inaelezea jinsi ya kutibu maji nyumbani kwa kutumia klorini ya maji.

Dawa ya kusafisha maji nyumbani inaweza kuwa na viwango tofauti vya klorini. Kawaida ni kati ya asilimia 3.5 hadi 5. Njia rahisi ya kupima kiasi kinachohitajika kutibu maji ni kwanza kutengeneza mchanganyiko wa dawa wenye asilimia 1 ya klorini, na kuchanganya kiasi hicho na maji ambayo unataka kutibu. Ili kuandaa mchanganyiko wa dawa:

 1. Weka kikombe kimoja cha dawa kwenye chupa safi ya lita moja.
 2. Jaza chupa hiyo na maji safi.
 3. Tikisa chupa kwa sekunde 30.
 4. Acha itulie kwa dakika 30.

Sasa mchanganyiko wa dawa ya kutibu maji utakuwa umekamilika. Iwapo kuna uchafu mwingi unaoelea kwenye maji, klorini haitafanya kazi vizuri. Hivyo chuja maji kwanza au ruhusu yatulie. Mimina maji safi yaliyotulia kwenye chombo kingine ndiyo uweke klorini.

Maji Kipimo cha dawa
Kwa lita moja ya maji
EHB Ch6 Page 99-1.png
EHB Ch6 Page 99-2.png weka matone 2
Kwa lita 2 za maji
EHB Ch6 Page 99-3.png
EHB Ch6 Page 99-4.png weka matone 8
Kwa lita 20 za maji
EHB Ch6 Page 99-5.png
EHB Ch6 Page 99-6.png weka kijiko ½

cha chai

Kwa lita 200 za maji
EHB Ch6 Page 99-7.png
EHB Ch6 Page 99-8.png weka vijiko 5 vya chai


Weka vipimo hivi vya mchanganyiko wa dawa kwenye maji safi na kusubiri angalau dakika 30 kabla ya kunywa. Iwapo maji siyo safi sana, utahitaji kuzidisha kipimo cha mchanganyiko wa dawa mara mbili.

Kutibu maji kwa kutumia mimea

Katika sehemu nyingi, watu hutumia mimea kusafishia maji ya kunywa. Mbegu za mibono (moringa) hutumika katika Afrika ya Mashariki. Ili kutumia mbegu za mibono:

 1. Kausha mbegu kwa siku 3.
 2. Leaves next to a mortar and pestle.
 3. Grind the seeds to powder. It takes 15 ground moringa seeds to clear 20 liters of water.
 4. Saga mbegu ili ziwe unga. Unga wa mbegu 15 za mibono unatosha kusafisha lita 20 za maji.
 1. Koroga unga na maji kidogo ili kutengeneza kama vile uji mzito halafu changanya kwenye maji.
 2. Koroga kwa muda wa dakika 5-10. Kadri utakavyokoroga kwa haraka ndivyo utakavyotumia muda mchache.
 1. Funika chombo na kukiweka pembeni ili maji yaweze kutulia. Baada ya saa1-2, mimina maji kwenye chombo safi. Hakikisha uchafu wote unabaki kwenye chombo cha kwanza.
Kutibu maji kwa kutumia mionzi ya jua

Maji yanaweza kutibiwa pia kwa kutumia mionzi ya jua. Njia hii huhitaji mionzi ya jua na chupa - basi! Yanapochujwa kwanza na kuacha yakatulia, tiba hukamilika haraka. Njia hii ya kutibu maji kwa mionzi ya jua hutumika zaidi katika nchi zilizopo karibu na Ikweta, kwa sababu kuna nguvu ya jua ya kutosha katika maeneo haya.

EHB Ch6 Page 98-1.png
 1. Safisha chupa ya plastiki au ya bilauri.
 2. Jaza maji nusu chupa halafu tikisa kwa sekunde 20. Hii itaongeza hewa kwenye maji. Kisha jaza chupa mpaka juu. Hewa iliyomo itasaidia maji kutibika haraka.
 3. Weka chupa chini ya jua na ambapo watu na wanyama hawataigusa kama vile kwenye paa la nyumba. Acha chupa ikae muda wa saa 6 chini ya jua kali au siku 2 katika hali yenye mawingu.
 4. Kunywa maji moja kwa moja kutoka kwenye chupa. Hii itazuia kuchafuliwa tena kutokana na mikono au vyombo vingine.


Maji yanaweza kutibiwa na mionzi ya jua haraka na kwa ukamilifu zaidi kwa kuiweka chupa ndani ya jiko maalum linalotumia mionzi ya jua

EHB Ch6 Page 98-2.png
Tumia limau au ndimu 1 kwa kila lita moja ya maji

Kutibu maji kwa kutumia maji ya limau

Ongeza maji ya ndimu au limau katika lita moja ya maji ya kunywa na yakae kwa muda wa dakika 30. Hii itaua vijidudu vingi vya kipindupindu na magonjwa mengine. Njia hii haifanyi maji kuwa salama kabisa, lakini ni bora kuitumia kuliko kutotibu maji kabisa katika maeneo yenye hatari ya kipindupindu. Kuongeza maji ya limau au ndimu kwenye maji kabla ya kutibu kwa kutumia mionzi ya jua, au kutumia njia ya kuchuja maji kwa kutumia vyombo vitatu, huyafanya maji kuwa salama zaidi


Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Juni 2022