Hesperian Health Guides
Njia ipi itumike na lini?
HealthWiki > Mwongozo wa jamii juu ya afya ya mazingira > Sehemu ya pili: Kuongeza uelewa na mwamko wa jamii juu ya afya ya jamii > Njia ipi itumike na lini
Njia zilizoelezewa katika moduli hii zinafaa kwa ajili ya kuchunguza masuala mahsusi ya afya ya mazingira, na pia katika kuhamasisha jamii. Njia hizi zinaweza:
- Kusaidia katika utambuzi wa matatizo au kuanzisha mjadala wa kijamii kuhusu jambo fulani (soma “Kemikali zenye sumu huingiaje kwenye maji?”, “Maji yanaweza kuonekana safi kwa macho lakini yasiwe salama,” na “Miduara miwili.”)
- Kusaidia kikundi kufanya maamuzi au kuchagua kati ya mahitaji tofauti na njia mbalimbali mbadala (soma “Kuchagua aina ya choo inayokufaa” na Tumia maarifa ya kila mtu, zingatia mahitaji ya kila mtu”)
- Kusaidia kukusanya habari na taarifa, kubadilishana maarifa na kubadili mitazamo yetu juu ya mazingira na sisi wenyewe (soma “namna magonjwa ya kuhara yanavyosambazwa,” “Kusimamisha ueneaji wa kuharisha,”, na “Hadithi ya mpelelezi - Je ilikuwaje maji yakachafuliwa?”).
- Kusaidia kujifunza mawazo mapya, kupitia upya mawazo tuliyonayo au ambayo tulijifunza zamani.
- Kusaidia kuanza uhamasishaji na maandalizi ya kutatua tatizo fulani (soma “Kuondoa vizuizi kwa wanawake kunufaika na huduma ya vyoo bora.”)
- Kusaidia uelimishaji juu ya masuala magumu au kuelewa na kutatua migogoro (soma “Kuondoa vizuizi kwa wanawake kunufaika na huduma ya vyoo bora,” “Igizo dhima.”)
Baadhi ya njia zilizoelezewa zinaweza kutumika pamoja, mathalan njia ya uchoraji ramani wakati au baada ya matembezi ya kiutafiti wa afya, au kutumia igizo dhima kama sehemu ya uchambuzi wa mahitaji ya jamii. La muhimu zaidi ni kwamba njia hizo ziwasaidie watu kukusanya taarifa, kubadilishana maarifa na kuongeza uelewa wao.
Hii itasaidia juhudi zao za uhamasishaji, uwezeshaji jamii na utekelezaji wa hatua mbalimbali katika kutafuta ufumbuzi wa kina kwa matatizo ya afya ya jamii.