Hesperian Health Guides
Sehemu ya tatu: Haki za kimazingira na upatikanaji wake
HealthWiki > Mwongozo wa jamii juu ya afya ya mazingira > Sehemu ya tatu: Haki za kimazingira na upatikanaji wake
Katika sura hii:
Baada ya kusoma sehemu ya tatu, utakuwa umejifunza: |
|
Kila mtu katika jamii ana haki ya kuwa na afya njema na kuishi katika mazingira salama na yenye afya. Kwa bahati mbaya, haki hizi mara nyingi haziheshimiwi. Watu wengi wanaathirika kutokana na matatizo ya kiafya yanayosababishwa na uhaba wa mahitaji ya msingi na kukithiri kwa vitu hatari katika mazingira. Walio katika hatari zaidi ni wale wenye hadhi ndogo kwa sababu ya rangi, kabila, dini, jinsia, tabaka, umasikini au kwa sababu zingine. Kawaida huwa ndiyo wanaathirika kwanza, na vibaya zaidi.
Mapambano ya kuishi katika mazingira yenye afya, salama, yenye tija na ambayo yanapendeza, hasa kwa jamii ambazo kawaida haziheshimiwi na watu wenye mamlaka yanaweza kuitwa mapambano kwa ajili ya haki za binadamu na kimazingira.
Kuna taarifa nyingi kutoka sehemu mbalimbali duniani kuhusu jamii ambazo zinaathirika kutokana na maafa ya kiafya kuhusiana na uharibifu wa mazingira. Vile vile, kuna taarifa nyingi zinazoelezea jinsi gani watu wanavyoendesha harakati mbalimbali katika kulinda na kutetea haki zao za kiafya na kimazingira. Sehemu hii inaelezea moja ya hadithi muhimu kuhusiana na mapambano hayo.