Hesperian Health Guides

Jinsi vitu vyenye sumu vinavyoingia kwenye miili yetu

Katika sura hii:

A woman drinking from a cup.
A man next to a can spewing toxic fumes.
A man scratching a rash on his arm.
Kula na kunywa Kupumua na Kupitia ngozi

Jijini Bhopal, maelfu ya watu walijikuta mara moja wakivuta gesi ya sumu na pia sumu hiyo kufunika miili yao. Hayo ndiyo yalikuwa madhara ya kwanza. Kwa sababu uvujaji huo haukudhibitiwa na kusafishwa, na mabaki ya kemikali hizo yakasalia eneo zima la kiwanda na maeneo yanayokizunguka, sumu hiyo iliingia kwenye udongo na kuchafua akiba ya maji iliyoko chini ya ardhi. Sasa baada ya miaka kadhaa, watu wanaendelea kunywa maji yenye sumu. Hii ni sehemu ya maafa ambayo bado yanaendelea. Hata kama ni tukio kubwa kama maafa ya Bhopal au tukio la kawaida kama vile kutokana na rangi za nyumba, au bidhaa zingine, jambo la kwanza ni kujiondoa kutoka eneo la kemikali hizo, au kuziweka mbali ili usiendelee kudhurika na sumu hiyo. Baada ya hapo, chukua hatua kuzuia hatari zingine kama hizo.

Pigania mabadiliko

Kwa kuziandaa jamii zao kupigania afya njema na ustawi wa muda mrefu, walionusurika katika maafa ya Bhopal wamewatia moyo watu wengi duniani kuchukua hatua kwa ajili ya haki za kimazingira na upatikanaji wa haki hizo kwa ujumla. Kanuni zifuatazo zimeonekana kusaidia:

  • Epuka vitu vyenye sumu katika maisha ya kila siku: Kwa ajili ya kufanya usafi nyumbani, kwenye taasisi au sehemu za kazi, tumia kemikali zisizo na sumu. Usitumie viuatilifu au mbolea za kemikali shambani. Kula vyakula ambavyo vimelimwa bila kutumia kemikali. Osha matunda na mboga za kijani vizuri kabla ya kula, au kupika. Kwa sababu inawezekana tayari kuna vitu vya sumu katika jamii zetu, hatuna budi kushinikiza serikali kuacha kuruhusu mashirika au kampuni kuwaweka watu katika hatari ya kudhurika na sumu, hususan wale walio katika hatari zaidi.
  • Jiandae kwa ajili ya kuzuia uchafuzi Chukua hatua mbalimbali kuzuia maafa ya sumu. Hatua hizo ni pamoja na maigizo, vyombo vya habari, intaneti na njia zingine za mawasiliano kuelimisha watu; au maandamano, migomo nk. Kama kiwanda kinachafua, fikiria pia njia zingine za wafanyakazi kupata riziki, kwa sababu wengi wao kawaida hujali tu ajira na pato.
A woman speaking as she holds her child.
Iwapo serikali zetu zingelinda mazingira yetu, jamii ingekuwa na uhakika zaidi wa afya bora.
  • Lazimisha kampuni au viwanda kusafisha uchafuzi wao. Ingawaje hili ni jambo gumu kufanikisha, kukitaka kiwanda au shirika kusafisha uchafuzi wake ni sehemu muhimu ya kila harakati ya kupigania haki za kimazingira. Watu wengi huamini-ingawa mashirika na kampuni hawakubali- kwamba kampuni lazima ziwajibike kuzuia madhara na kukarabati uharibifu wote watakaousababisha.
  • Shinikiza serikali kwa ajili ya viwango bora vya usalama. Bahati mbaya, serikali hulinda maslahi ya mashirika makubwa kuliko maslahi ya jamii. Hali hii huchangia ukiukwaji wa haki za kimazingira na kusababisha maafa, hasa kampuni zinapolichukulia swala la usalama wa mazingira kuwa gharama inayoepukika badala ya kuwa wajibu wao. Serikali hazina budi kubadilisha vipaumbele na kuwalinda watu wote, hasa walio katika hatari zaidi.
  • Kubadili mitazamo ya viwanda. Kampuni ya Union Carbide huko Bhopal ilitengeneza viuatilifu kudhibiti wadudu wanaoathiri mazao. Lakini kuna njia bora zaidi za kudhibiti wadudu hao kuliko kutumia kemikali. Kwa ukweli kuna njia zisizo na madhara makubwa na zilizo endelevu. Sasa kwa nini inaruhusiwa watu kuathiriwa na viwanda, lakini hawaruhusiwi kuamua jinsi gani viwanda vinapaswa kutengeneza bidhaa zake?

Kiwango cha hatari kinachokubalika? Kwa nani?

Viwanda na serikali mara nyingi huhalalisha uharibifu wa mazingira, hata yale ya Bhopal kwa hoja kwamba kiasi fulani cha uharibifu wa mazingira hakiwezi kuepukika kwa ajili ya maendeleo. Hii inamaanisha kwamba watu wenye uwezo mdogo mara nyingi hutolewa kafara ili kampuni ziendelee kutengeneza faida kama kawaida. Kwa wengi, hili halikubaliki. Lengo la faida haliwezi kuwa sababu ya kuhalalisha madhara makubwa kwa watu, na ukiukwaji wa haki za msingi za kiafya na kuishi katika mazingira salama.

Kama kampuni ya Union Carbide na serikali ya India ingetumia kanuni ya tahadhari kwanza, huenda maafa hayo yasingetokea.

Kudai tahadhari

Hatua za kiusalama zinaweza kupunguza madhara. Lakini hata kama hatua za kiusalama zitachukuliwa, bado kuna kiwango cha hatari kwenye viwanda. Iwapo hatari hii haiwezi kuepukika kabisa, basi bora ibebwe kwa usawa badala ya watu wenye hali ya chini tu ndiyo kubebeshwa mzigo huo.

Katika mipango ya muda mrefu, viwanda vinapaswa kujipanga kwa msingi ambao huheshimu usalama na uendelevu kuliko faida kubwa. Ili kufanikisha lengo hili, mashirika au kampuni zinawajibika kutumia njia salama na zenye haki zaidi katika utendaji na uzalishaji, na serikali zinapaswa kuwawajibisha kwa kutekeleza sheria zinazolinda afya na mazingira. Njia moja wapo ya kuchangia upatikanaji wa haki za kimazingira ni kuwataka viongozi na wengine wenye mamlaka kufanya maamuzi kwa kutumia kanuni ya tahadhari kwanza.

Illustration of the following: The shape of the factory turned sideways becomes a gun.
Wenye viwanda watakiwe kuchukuwa tahadhari....
EHB Ch4 Page 43-2.png
Kiwanda chenye dalili ya kuchafua mazingira... ...kinaweza kugeuka kuwa silaha ya maangamizi!


Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Juni 2022