Hesperian Health Guides
Kuwahudumia wanawake wajawazito
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Ujauzito na kujifunguaa > Kuwahudumia wanawake wajawazito
Sehemu ya sura hii iliyobaki inatoa maelekezo hasa kwa wakunga na wafanyakazi wa afya wanaowahudumia wanawake wajawazito na watoto wachanga. Akina mama pia wanaweza kutumia taarifa hizi, kuelewa kipi ni kawaida na kipi ni hatari. Mkunga au mfanyakazi mwingine wa afya anapaswa kukutana na mwanamke mjamzito mara kadhaa wakati wa ujauzito. Baada ya takriban miezi 8, wakutane kila wiki. Katika mikutano hii, mkunga anaweza:
- Kujibu maswali ambayo ataulizwa.
- Kutoa elimu juu ya lishe bora, kupumzika, na mahitaji mengine ya wanawake wajawazito.
- Kuchunguza dalili za kiafya ambazo zinaonesha kama mama na mtoto wako vizuri au wanahitaji msaada.
Andika kwenye karatasi kila utakachojifunza katika kila ziara ili uweze kujibu maswali kama: âJe huyu mama anaongezeka uzito wa kutosha kumhimili mwanae?â na âJe, kiwango cha shinikizo lake la damu kinabaki palepale au kinapanda juu?â (Kupanda kwa kiwango cha shinikizo la damu kunaweza kuashiria hali inayotangulia kifafa cha mimba.)
Dalili za hatari wakati wa ujauzito |
Nenda kituo cha afya au hospitali kama utagundua moja wapo ya dalili za hatari kiafya zifuatazo. Zinaweza kuhatarisha maisha ya mwanamke mjamzito.
|
YaliyomoMaswali ya kumuuliza mwanamke mjamzito |
|||
Mjamzito kwa muda gani? Mtoto anatarajiwa lini?
|
Kila anapohudhuria, kadiria ujauzito ni wa wiki ngapi. Chunguza tena hedhi yake ya mwisho ilianza tarehe ngapi, na kuhesabu wiki ngapi zimepita tangu tarehe hiyo.
|
||
Baada ya kujua ujauzito una muda gani unaweza kufahamu kama mtoto anaongezeka vya kutosha au la.
|
|||
Mimba zilizopita zilikuwaje? |
|||
Alikuwa na shinikizo la juu la damu?
|
Shinikizo la juu la damu au shambulio viliashiria mwanzo wa kifafa cha mimba. Kutana na mama huyu angalau mara moja kwa wiki baada ya wiki 28 za ujauzito. Katika kila mkutano, pima shinikizo lake la damu, na mkojo wake kuhusiana na protini. Panga jinsi utakavyompatia msaada wa kitabibu haraka kama atauhitaji. Bonyeza hapa.
|
||
Je kuna watoto wake waliofariki kabla ya kuzaliwa? Kwa nini?
|
Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kuhusika na kifo cha mtoto katika miezi ya mwisho ya ujauzito. Ugonjwa wa kisukari ni miongoni mwa sababu hizo, hivyo mchunguze mama iwapo ana dalili za kisukari. Lakini mara nyingi hakuna anayejua fika, na hata hivyo sababu inayojulikana inaweza kutojirudia tena. Bila kuzingatia kipi kimesababisha kifo au vifo hivyo, sikiliza maelezo ya mama huyu kwa huruma.
|
||
Uzazi uliopita ulikuwaje? |
|||
Alivuja sana damu baada ya kujifungua mtoto wake wa mwisho?
|
Tafuta njia ya kumwezesha mwanamke huyu ajifungulie kwenye hospitali au kituo cha afya chenye vifaa vya kutosha. Iwapo hili haliwezekani, andaa dawa kumtibu kutokana na kuvuja damu sana atakapojifungulia nyumbani. |
||
Je uchungu wake wa uzazi huwa unakuja haraka au polepole?
|
Kama huko nyuma alipata uchungu wa uzazi wa haraka, muwahi kadri uwezavyo au andaa mpango wa namna atakavyopelekewa haraka hospitali au kwenye kituo cha afya.
|
||
Kama amekuwa akipata uchungu wa uzazi wa polepole au taratibu, anaweza kuwa na nyonga ndongo au tatizo lingine. Kuwa tayari kwenda hospitali iwapo uchungu wake ni wa polepole au taratibu mno.
|
|||
Je kuna baadhi ya watoto wake ambao walizaliwa na uzito mdogo sana? Je walikuwa wakubwa â wenye uzito mkubwa sana?
|
Watoto wenye uzito mdogo sana wanaweza kupatwa na matatizo ya kupumua na maambukizi kwa urahisi zaidi. Jaribu kumsaidia mama kutengeneza angalau mtoto mwenye uzito mkubwa zaidi katika uzazi huu. Iwapo kuna uhaba wa chakula, je unaweza kutafuta njia za kumwezesha kupata zaidi?
|
||
Moshi wa sigara na sumu zingine huchangia mtoto kuwa na uzito mdogo. Je mabadiliko gani yanahitajika ili kumkinga mama na mtoto dhidi ya madhara hayo?
|
|||
Mtoto mkubwa, mwenye uzito zaidi ya kilogramu 4 anaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa kisukari.
|
|||
Aliwahi kufanyiwa operesheni wakati wa kujifungua? Aliwahi kujifungua kwa msaada wa fosepsi â aina ya kishikio ambacho hutumika katika operesheni kusaidia kumtoa mtoto nje wakati wa kujifungua? Je, anajua ni kwa nini?
|
Operesheni ya kawaida au kujifungua kwa kutumia kifaa cha fosepsi huenda vilitokana na uchungu wa uzazi kuwa taratibu au polepole mno, jambo ambalo linaweza kujitokeza tena. Je uchungu wa uzazi ulichukuwa muda mrefu mno? Kama hapana, huenda operesheni haikuhitajika.
Inawezekana akajifungua kwa njia ya kawaida katika uzazi mwingine baada ya kujifungua kwa operesheni. Lakini ni bora zaidi kuenda hospitalini.
|
||
Je kuna watoto wake ambao waliwahi kufariki mara baada ya kuzaliwa?
|
Vifo vya watoto wachanga hutokana na sababu nyingi. Pepopunda (Tetanasi), kichomi (nimonia), kuharisha, na maambukizi baada ya kuzaliwa ambayo huchangia sumu kuingia kwenye damu - yote yanaweza kuzuilika. Jifunze jinsi ya kuzuia na kutibu maambukizi hayo kutoka Sura ya watoto wachanga na unyonyeshaji.
|
||
Alipata matatizo katika kunyonyesha?
|
Bonyeza hapa kwa ajili ya msaada juu ya unyonyeshaji.
|
||
Afya yake ikoje hivi sasa? |
|||
Je ana maambukizi yoyote ya hatari kama vile malaria, kifua kikuu, VVU, au mengineyo?
|
Maambukizi yoyote hatari lazima yatibiwe.
|
||
Ana muwasho, harufu mbaya, au anatokwa na majimaji ya njano ukeni? Anasikia maumivu ukeni au eneo la tumbo la uzazi anapokuwa anafanya tendo la ngono?
|
Ongezeko la majimaji ya meupe au yasiyo na rangi kutoka ukeni ni kawaida wakati wa ujauzito. Lakini majimaji ambayo yanatoa harufu mbaya au maumivu ukeni ni dalili za maambukizi. Angalia Matatizo na maambukizi ya via vya uzazi (kinaandaliwa).
|
||
Je anasikia maumivu au mwako au mchomo anapokojoa? Au maumivu mbavuni au katikati mgongoni.
|
Chunguza uwezekano wa kuwepo maambukizi kwenye njia ya mkojo (maambukizi ya kibofu). Angalia Matatizo katika kutoa mkojo (kinaandaliwa).
|
||
Je anatokwa na damu ukeni?
|
Kuvuja damu kabla ya wiki 20 kawaida huashiria mimba kuharibika, na mara nyingi siyo hatari kwa afya ya mwanamke. Lakini kuvuja damu baada ya wiki 20 (miezi 4½) ni hatari na dharura. Tafuta msaada haraka.
|
||
Mama huyu ana ugonjwa wa kisukari (sukari nyingi kwenye damu)?
|
[[
Mwanamke mwenye kisukari anapaswa kuendelea na tiba yake ya insulini wakati wa ujauzito. Ni muhimu kupima kiwango cha sukari kwenye damu kila baada ya mlo, kama anaweza. Atahitaji msaada wa madaktari wakati wa kujifungua.
|
||
Inawezekana pia kupata kisukari kwa sababu ya mimba. Kisukari cha aina hii huitwa kisukari cha ujauzito. Pima kiwango cha sukari kwenye mkojo kwa kutumia vipima mkojo vya kuchovya. Iwapo ana sukari kwenye mkojo, anahitaji kupata kipimo kamili cha damu cha ugonjwa wa kisukari.
|
|||
Je kuna dawa ambazo anatumia?
|
Tumia Orodha ya dawa (kinaandaliwa) au tumia rejea nyingine kujifunza juu ya dawa ambazo mama huyu anatumia. Jiulize, âni lazima atumie dawa hiyo?â na, âni salama wakati wa ujauzito?â Ingawa inaweza kuwa inahitajika lakini siyo salama, tafuta dawa nyingine salama ambayo anaweza kutumia kama mbadala.
|
||
Ana mzio na dawa yoyote?
|
Chunguza mzio wowote kutokana na dawa. Epuka kumpa dawa ambazo zinampa mzio, na andaa kutumia dawa zingine ambazo ni salama kama mbadala.
|
||
Je huwa anatumia mimea/mitidawa au tiba za asili?
|
Baadhi ya mimea/mitidawa inaweza kusababisha madhara inapotumika wakati wa ujauzito. Angalia Dawa, vipimo na matibabu (kinaandaliwa) kwa msaada katika kuamua zipi zinaweza kuwa salama.
|
||
Je huwa kemikali kali zinatumika nyumbani au kazini kwake? Vitu vyenye hatari zaidi ni viuawadudu, dawa kali za kufanyia usafi, kemikali na bidhaa ambazo hutumika viwandani.
|
Kemikali kali ni hatari kwa kila mtu. Baadhi zinaweza kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa na hitilafu au tayari akiwa amekufa. Je unawezaje kumlinda mama huyu dhidi ya kemikali hatari?
|
||
Huwa anakula nini katika siku zake za kawaida?
|
Tumia sura ya Lishe bora hutengeneza afya bora kuongea na mama huyu kuhusu kula vizuri kila siku.
|
||
Kuna mtu yoyote ambaye humsaidia kuwahudumia watoto wake wengine na kazi za nyumbani? Kuna anayemsaidia na chakula, maji, kuni au mkaa wa kupikia kila anapohitaji msaada?
|
Ongea na familia ya mama mjamzito kuhusu kusaidia zaidi na kazi za nyumbani. Kama familia haitoi msaada wa kutosha, majirani, jamaa zake kutoka kanisani au msikitini, au wafanyakazi wenzake wanaweza kuhimizwa kusaidia.
|
||
Amepanga kujifungulia wapi?
|
Kama amepanga kujifungulia nyumbani, amua jinsi atakavyopata msaada wakati wa dharura. Bonyeza hapa.
|
||
Kama anatarajia kujifungulia hospitalini au kwenye kituo cha afya, waandae mpango wa kumfikisha huko, pamoja na jinsi gharama za usafiri na gharama zingine za hospitali zitakavyolipiwa.
|