Hesperian Health Guides

Ujauzito na kujifungua: Madawa

Dawa kwa ajili ya uvujaji damu mkali baada ya kujifungua

Oksitosini


Oksitosini huzuia au kudhibiti uvujaji damu mkali baada ya kujifungua. Inaweza pia kutumika kuharakisha kutoa kondo la nyuma ambalo linaonekana kuchelewa au kukwama kutoka. Ikitumika kwa ajili ya kazi hizi, dawa hiyo ni salama na hufanya kazi vizuri.

Hospitalini, dawa ya oksitosini wakati mwingine hutumika kuharakisha uchungu wa uzazi, lakini kamwe isitumike nyumbani kwa lengo hili kwa sababu bila uangalizi makini wa kitabibu inaweza kusababisha tumbo la uzazi kubana sana na hata kuchanika.


Jinsi ya kutumiaNBgrninject.png
Kutibu au kuzuia uvujaji damu mkali baada ya kujifungua
Choma sindano yenye vipimo 10 kwenye msuli wa paja sehemu za pembeni. Kama uvujaji damu mkali untaendelea, subiri dakika 15 halafu choma tena vipimo vingine 10 vya dawa hii.

Misoprosto


Misoprosto huzuia au kudhibiti uvujaji damu mkali baada ya kujifungua.

Hospitalini, misoprosto wakati mwingine katika vipimo vidogo vidogo hutumika kuharakisha kasi ya uchungu wa uzazi. Lakini isitumike nyumbani kwa kazi hii kwa sababu bila uangalizi wa karibu wa kitaalaam inaweza kusababisha tumbo la uzazi kubana sana na kuchanika.

Wakati mwingine dawa hii hutumika kukatisha ujauzito katika miezi michache ya mwanzo, au kudhibiti uvujaji damu kutokana na mimba iliyotolewa au kuharibika.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Kichefuchefu, maumivu ya tumbo, au kuharisha.

MuhimuNBgrnimportant.png

Chunguza halijoto ya mama baada ya kumpa dawa hii kwani wakati mwingine husababisha homa kali. Kama homa kali itatokea, simamisha utoaji wa dawa ya misoprosto na tibu homa mara moja kwa kutumia parasetamo.

Misoprosto kawaida haipaswi kutumika kwa wanawake ambao wamefanyiwa operesheni ya uzazi hivi karibuni.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png

Yeyusha vidonge vya misoprosto chini ya ulimi au ndani ya shavu. Vidonge pia hufanya kazi vizuri vikiyeyushwa ndani ya uke au ndani ya unyeo. Hii hasa husaidia iwapo mwanamke ana kichefuchefu.

Kutibu uvujaji damu baada ya kujifungua
Yeyusha makrogramu 600 chini ya ulimi, ndani ya unyeo au ukeni.