Hesperian Health Guides

Ujauzito na kujifungua

Katika sura hii:

Mwanamke mjamzito anapokuwa na afya nzuri na kupatiwa matunzo yanayohitajika, kuna uwezekano kuwa ujauzito wake utakuwa wenye afya pamoja na mtoto akayezaliwa. Akina mama, wakunga na wafanyakazi wa afya wanaweza kufanikisha afya bora inayohitajika wakati wa ujauzito na kuzuia, kutibu, au kupata msaada kwa ajili ya matatizo kama yatajitokeza.

Dalili za ujauzito

 "Familia yenye furaha"

Mwanamke mara nyingi hukisia kuwa ana mimba anapoona baadhi ya dalili zifuatazo:

  • Kukosa hedhi
  • Kichefuchefu
  • Kujisikia mchovu
  • Kukojoa mara kwa mara
  • Matiti huwa laini na kuongezeka ukubwa
  • Kuongezeka uzito


Kipimo cha damu au mkojo kinaweza kuthibitisha kwa uhakika kuanzia wiki 2 baada ya mimba kutunga (mwezi mmoja baada ya mwanzo wa hedhi iliyopita).

Ujauzito unapofikia miezi 4½, mama anaweza kusikia mtoto akijigeuza na mfanyakazi wa afya anaweza kusikiliza mapigo yake ya moyo kwa kutumia kifaa kiitwacho fetoskopu ambacho huwekwa juu ya tumbo la mama yake.

Mtoto atazaliwa lini?

Ujauzito huchukua takriban miezi 9 (miandamo ya miezi 10 au wiki 40). Kupata picha halisi lini mtoto atapozaliwa:

Mwanamke akihesabu kwa kutumia vidole vyake

Jumulisha miezi 9 na kuongeza siku 7 kwenye siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho. Hiyo ndiyo siku mtoto anatarajiwa kuzaliwa. Watoto wengi huzaliwa kati ya wiki 3 kabla hadi wiki 2 baada ya tarehe hii.

Kwa mfano, chukulia kwamba hedhi ya mwisho ya mwanamke ilianza Februari 30.

Februari 10 + miezi 9 = Novemba 10 Novemba 10 + siku 7 = Novemba 17 Tarehe ya mtoto kuzaliwa inatarajiwa kuwa Novemba 17.