Hesperian Health Guides
Kuzaliwa
Kichwa kinapoanza kutoka huonekana hivi:
Kamwe usizungushe kichwa cha mtoto au kukivuta.
Kamata kichwa cha mtoto taratibu. Kielekeze sehemu ya chini-kwenye makalio ya mama kutoka kwenye tumbo lake. Tega mikono yako ili mwili wa mtoto uliobakia ndani utue mikononi vizuri.
Iwapo kiungamwana kimejizungushia kwenye shingo ya mtoto, unaweza taratibu kukilegeza vya kutosha ili kipite juu ya kichwa cha mtoto au kuruhusu mwili wa mtoto kutereza na kupita ndani kwa urahisi. Katika hali isiyo ya kawaida, kama kitakuwa kimejifunga sana kwenye shingo ya mtoto na mtoto hawezi kukipita, unaweza kukibana na kukikata. Baada ya hapo, mama atatakiwa kusukuma mtoto nje haraka iwezekanavyo.
Kama mabega yatakwama kutoka baada ya kichwa kutoka, mwezeshe mama kutanua miguu, kupiga magoti na kuegemea kwenye mikono yake. Mwambie azuie pumzi yake halafu asukume kwa nguvu.
Kama mtoto bado amekwama, mgeuze mama alalie mgongo wake. Mwambie avute magoti yake nyuma kadri awezavyo hadi kwenye kwapa zake. Tafuta mtu wa kusaidia kumsukuma kwa nguvu, juu kidogo ya mfupa wa nyonga kama ilivyoelekezwa kwenye picha. Sogeza kichwa cha mtoto chini kuelekea kwenye sakafu kuweka huru mabega yaliyonaswa chini ya mfupa wa nyonga.
Unaweza kutakiwa kuigiza mikono ukeni na kumgeuza mtoto kwa kusukuma kwa ungalifu nyuma ya bega lake. Au kuuelekeza mkono wa mtoto chini ukipita katikati ya mwili wake na hatimaye nje ya uke. Mwili unapaswa kushuka kwa urahisi.
Baada ya kujifungua, mweke mtoto moja kwa moja kwenye kifua uchi cha mama yake-ngozi kwa ngozi. Sehemu hii ndiyo salama na yenye joto analolihitaji mtoto. Taratibu pangusa kamasi kwenye mdomo wa mtoto, halafu kwenye pua. Makaushe mtoto kwa kutumia nguo safi au taulo. Halafu mfunike mtoto na mama yake kwa nguo au blanketi. Kwa taarifa zaidi juu ya utunzaji wa mtoto mchanga, angalia Watoto wachanga na unyonyeshaji.
Yaliyomo
Mambo ya kuchunguza baada ya mtoto kuzaliwa:
- Mtoto anapumua? Kama mtoto hapumui, kupambana kupumua, au anageuka rangi ya blu, bonyeza hapa.
- Je mama yake anavuja sana damu? Kama anavuja damu baada ya kujifungua bonyeza hapa.
Funga kwa mikunjo ya kamba mara nne. |
Kiungamwana
Nawa mikono vizuri. Tumia kibanio kilichotakaswa au kamba ambayo imetoka kuchemshwa au kamba ya kitambaa safi ambacho imetoka kufuliwa na kupigwa pasi.
Funga kiungamwana takriban urefu wa vidole viwili kutoka kwenye mwili wa mtoto. Halafu funga tena fundo lingine vidole 2 kutoka kwenye fundo la kwanza.
Kata kiungamwana katikati ya fundo mbili. Tumia kiwembe kipya kabisa, au mkasi msafi au kifaa kingine cha kukata. Kila utakachotumia kukata kiungamwana lazima kwanza kioshwe vizuri na maji safi na kutakaswa. Kuchemsha ndiyo njia bora zaidi. Kama huwezi kukichemsha, kiweke juu ya ndimi ya moto au safisha kwa dawa ya kuua vijidudu ambavyo vinaweza kusababisha maambukizi. Baada ya kukata, acha kisiki chake huru kuzuia maambukizi. (Bonyeza hapa kwa ajili ya taarifa juu ya utunzaji wa kisiki cha kiungamwana.)
Kondo la nyuma
Kama hakuna uvujaji mkubwa wa damu, basi hakuna uharaka wa kujifungua kondo la nyuma. Subiri hadi mama atakapohisi msukumo wa kulitoa nje. Kama anavuja damu, mwambie asukume sana wakati misuli inaporudia kubana na kuachia. Iwapo kondo la nyuma halitatoka nje:
- Msaidie mama kunyonyesha. Kunyonyesha mara baada ya kujifungua husababisha munyukano wa misuli ambao hulisukuma nje kondo la nyuma.
- Mwambie mama akakojoe. Kibofu cha mkojo kilichojaa huzuia tumbo kubana na kulisukuma nje kondo la nyuma.
- Mwambie mama kuchuchumaa, halafu kusukuma tena.
Kama mama anapoteza damu haraka, au kama hatua zilizopendekezwa awali hazijafanikiwa, jaribu taratibu kuvuta kiungamwana hicho. Ukisikia kinakataa, acha. (Kuvuta sana kunaweza kusababisha kiungamwana kukatika au hata kuvuta nje kizazi).
Mara baada ya kondo la nyuma kutoka, lichunguze. Je, kuna sehemu yoyote inakosekana? Kama ndiyo, pangusa tumbo sehemu ya chini kwa nguvu ili iweze kutoka. Mpe mama oksitosini au misoprosto. Iwapo sehemu iliyobaki haitoki, tafuta msaada wa daktari. Sehemu ya kondo la nyuma ikibaki ndani ya tumbo huweza kusababisha maambukizi mabaya na uvujaji damu.
Mpe mama oksitosini au misoprosto. Iwapo sehemu iliyobaki haitoki, tafuta msaada wa daktari. Sehemu ya kondo la nyuma ikibaki ndani ya tumbo huweza kusababisha maambukizi mabaya na uvujaji damu.
Baada ya mama na mtoto kuwa salama, tumia muda kufanya usafi, safisha sehemu za uzazi za mama na miguu yake, na kumpa chakula na kinywaji. Msaidie mama na mtoto kuanza unyonyeshaji (bonyeza hapa) na toa baraka na pongezi zako kwa familia wanapomkaribisha mtoto mpya duniani!