Hesperian Health Guides

Dawa kwa ajili ya maambukizi tumboni

Kwa ajili ya homa za wastani wakati wa uchungu wa uzazi, ampisilini pamoja na jentamaisini kawaida zinakidhi. Lakini kwa ajili ya homa kali wakati wa uchungu, au kwa dalili za maambukizi baada ya kujifungua, tumia pia metronidazoli ilikupambana na bakteria ambazo zinaweza kusababisha maambukizi.Ni bora zaidi angalau kuchoma dozi ya kwanza ya ampisilini, lakini kama una vidoge tu, mpe hivyo vidonge.

AMPISILINI: Choma gramu 2. Subiri kwa saa 6, halafu choma au mpe kwa njia ya mdomo gramu 1 kila baada ya saa 6.
     NA
JENTAMAISINI: Choma miligramu 5 kwa kila kilogramu 1 ya uzito, mara moja kwa siku. Kama huwezi kumpima mama uzito, choma miligramu 80, mara 3 kwa siku.
     NA
METRONIDAZO Mpe miligramu 500 kwa njia ya mdomo, mara 3 kwa siku.

Mpe dawa zote 3 hadi siku 2 baada ya dalili za maambukizi kusimama.

Iwapo ana mzio na penisilini, mpe miligramu 500 za ethromaisini mara 4 kwa siku badala ya ampisilini. Michepuo mingine ya antibiotiki inaweza kutolewa iwapo ndiyo hiyo uliyonayo. Chagua mchepuo wenye uwezo wa kupambana na bakteria za aina nyingi.

Ampisilini


Ampisilini ni penisilini yenye wigo mpana, maana yake ni kwamba inaweza kuua aina nyingi za bakteria. Ampisilini inaweza kutumika badala ya amoksilini, na amoksilini kama mbadala wa amipisilini. Hii ina maana iwapo kitabu hiki au chanzo kingine kitapendekeza dawa hizi,unaweza kutumia moja badala ya nyingine, kwa kuzingatia kipimo sahihi.

Ampisilini ni salama sana na husaidia hasa dhidi ya maambukizi wakati wa kujifungua.


Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Ampisilini huwa na mwelekeo wa kusababisha kichefuchefu na kuharisha.

Madhara mengine ya kawaida ni upele. Lakini uvimbevimbe mwilini ukiwa na mwasho ambao huja na kutoweka ndani ya saa chache huenda pia ni dalili ya mzio wa penisilini. Simasisha kutoa dawa mara moja na usimpe mtu huyu penisilini tena. Mizio ya baadae inaweza kuwa mibaya zaidi na hata kutishia maisha. Kwa baadhi ya matatizo, erithromaisini inaweza kutumika kama mbadala. Upele uliotanda kama surua ambao kawaida huanza wiki moja baada ya kuanza dawa, na kuchukua siku kadhaa kutoweka huenda siyo dalili ya mzio. Lakini haiwezekani kujua kwa uhakika iwapo upele huo unatokana na mzio au la. Hivyo kawaida ni bora kusimamisha dawa iwapo hali hiyo itatokea.

MuhimuNBgrnimportant.png

Usugu wa vijidudu dhidi ya dawa hii unazidi kuongezeka. Kutegemea na eno unapoishi, dawa hii inaweza kutotibu tena stafilokokasi (staphylococcus), shigella, na maambukizi mengine.

Jinsi ya kutumiaNBgrninjectpill.png

Ampisilini hufanya kazi vizuri inapotumiwa kwa njia ya mdomo. Inaweza pia kutolewa kwa njia ya sindano lakini, inapaswa kuchomwa dhidi ya magonjwa makali kama vile maambukizi kwenye nyonga au kwenye tumbo la uzazi, au iwapo mgonjwa hawezi kumeza chochote au anatapika.

Kama ilivyo kwa antibiotiki nyingine, toa dawa kwa ajili ya siku chache zilizopendekezwa hapa. Kama mgonjwa bado ana dalili za maambukizi, aendelee kutumia kiasi kile cha dawa kila siku hadi dalili zote za maambukizi zitakapotoweka angalau kwa saa 24. Kama mgonjwa ametumia dawa hiyo kwa kiwango cha dozi ya juu zaidi na siku zinazopendekezwa na bado anaumwa, simamisha kumpa dawa hiyo na tafuta msaada wa daktari.

Vivyo hivyo, kiwango cha dozi ya antibiotiki hutegemea umri au uzito na ukali wa maambukizi.Hivyo toa dozi ndogo kwa mtu mwenye mwili mdogo au maambukizi madogo, na dozi kubwa zaidi kwa mtu mwenye uzito zaidi au maambukizi makali zaidi.


Kwa maambukizi tumboni
Mpe kwa kuunganisha na antibiotiki zingine na katika vipimo vilivyoorodheshwa vilivyoorodheshwa hapa.

Jentamaisini


Jentamaisini ni antibiotiki kali sana. Inaweza kutolewa tu kwa njia ya sindano au kwenye mshipa. Dawa hii inaweza kuharibu figo na uwezo wa kusikia, hivyo inatakiwa kutumika tu katika hali za dharura.

MuhimuNBgrnimportant.png

Jentamaisini lazima itolewe kwa kuzingatia dozi sahihi. Kuzidisha dawa kunaweza kusababisha uharibifu wa figo au uziwi kabisa. Ni bora zaidi kutoa dozi inayoendana na uzito wa mwili wa mgonjwa. Na usitoe jentamaisini kwa zaidi ya siku 10.

Jinsi ya kutumiaNBgrninject.png

Kwa maambukizi tumboni
Mpe dawa ikiunganishwa na antibiotiki zingine na katika vipimo vilivyoorodheshwa hapa.

Metronidazo


Metronidazo ni dawa imara katika kupambana na bakteria na maambukizi mabalimbali inapotumika peke yake au hata pamoja na antibiotiki nyingine.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Kichefuchefu,mkakamao wa misuli, na kuharisha ni kawaida. Kumeza dawa na chakula kunaweza kusaidia.Wakati mwingine husababisha ladha ya chuma mdomoni au maumivu ya kichwa.

MuhimuNBgrnimportant.png

Usitoe metronidazo katika miezi 3 ya mwanzo wa ujauzito kwa sababu inaweza kusababisha hitilafu kwa mtoto atakayezaliwa. Pia epuka kutoa metronidazo baadaye wakati wa ujauzito au wa kunyonyesha isipokua tu kama ndiyo dawa iliyopo yenye uwezo kwa tatizo hilo, na inahitajika hasa.

Usitumie pombe wakati unatumia metronidazo au angalau siku 2 au zaidi baada ya kuitumia dawa hii. Kuchanganya pombe na dawa hii husababisha kichefuchefu kikali. Pia usitumie metronidazoli iwapo una matatizo ya ini.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png

Kwa matatizo mengi, unaweza kutoa dozi kubwa ya dawa hii kwa siku 3, au dozi ya chini kwa siku 5 hadi 10.Wanawake wajawazito hawapaswi kupewa dozi kubwa za dawa hii.

Kwa ajili ya maambukizi tumboni
Mpe, ukichanganya na antibiotiki zingine na, kwa viwango vilivyoorodheshwavivyoorodheshwa hapa.