Hesperian Health Guides

Kupimwa kisukari

Katika sura hii:

mfanyakazi wa afya akimpima mwanamke shinikizo la damu.

Kiwango cha sukari kwenye damu kinaweza kupimwa kwa kipimo cha damu au mkojo. Kipimo cha damu huwa na uhakika zaidi.

Nani anapaswa kupimwa?

Mtu anaweza kupimwa kwa ajili ya kisukari kama:

mwanaume na mwanamke wakielekea kwenye kiliniki ya kisukari.

Vipimo vya damu

Aina zote za kisukari zinaweza kugundulika kwa kupima viwango vya sukari kwenye damu. Mfanyakazi wa afya anaweza kukupima vipimo tofauti kwa ajili ya kisukari au anaweza kurudia kipimo. Vipimo vinaweza pia kutumika kukidhibiti kisukari kwa kukusaidia kuangalia matokeo kulingana na mabadiliko ambayo unafanya katika ulaji wako, kujishughulisha, au dawa.

Vipimo vya damu hupima iwapo kiwango cha sukari kwenye damu ni sawa, au kama kiko juu kiasi, au kama kuna ugonjwa wa kisukari. Kama sukari kwenye damu iko juu lakini siyo kufikia kiwango cha kuashiria kisukari, mtu anaweza kuzuia kupata kisukari kwa kula vyakula vyenye afya, na kufanya mazoezi zaidi.

Kuna vipimo 2 vya kawaida vya kisukari, FBS na A1C.

Kipimo cha sukari kwenye damu kabla mtu hajala chochote -FBS au FPG). FBS au FPG ndiyo kipimo kikuu. Kipimo hiki hufanyika asubuhi kabla mtu hajala chochote. Baadhi ya kliniki hupima sukari kwenye damu kwa kutumia kifaa cha glukomita, kwa kupima tone la damu kutoka kwenye ncha ya kidole. Au kliniki inaweza kuchukua damu kwenye bomba la sindano na kuipeleka maabara. Matokeo ya kipimo hiki kabla mtu hajala chochote hutegemea mfumo wa vipimo ambao unatumika katika eneo lako au taasisi ya afya husika. Kama vipimo vinatumia mfumo wa mmol/l (millimols kwa lita), matokeo yatakuwa kati ya 4 na 20. Kama matokeo yataonesha una 6.9 mmol/l au zaidi, unaweza kuwa na kisukari. Kama eneo lako linatumia mfumo wa mg/dl (miligramu kwa decilita), matokeo yatakuwa kati ya 80 na 350. Kwa kipimo hiki, watu wenye 125 mg/dl au zaidi wanaweza kuwa na kisukari.

Baadhi ya vipimo vinaweza kufanyika kwa kutumia tone la damu kutoka kwenye ncha ya kidole. Kuhusu vipimo vingine, damu kutoka kwenye mshipa wa mkono itachukuliwa. Mfanyakazi mwenye uzoefu anaweza kulifanya zoezi hili kwa usalama kwenye kliniki, bila maumivu kabisa au kwa maumivu kidogo. mfanyakazi wa afya akitoa damu kwenye mshipa wa mkono wa mwanamke.


Kipimo cha A1C hutoa matokeo ya wastani wa kiwango cha sukari kwenye damu ya mtu kwa miezi 3 iliyopita. Mtu hahitaji kutokula ili kufanyiwa kipimo hiki. Kliniki itatoa sampuli ya damu kwa kutumia sindano na kuipima kwenye maabara. Matokeo ya kipimo cha A1C yatakuwa katika asilimia (%) kawaida kati ya 4% na 14%. Kama matokeo yatakuwa karibu na 6.4%, au zaidi, unaweza kuwa na kisukari. Kama matokeo yatakuwa chini kidogo ya 6.4% utahitaji kujilinda mwenyewe kwa kuchukua hatua kadhaa, na kupimwa tena kisukari siku zinazofuata.

Kipimo cha mkojo

Kipimo cha mkojo kinaweza kuonesha kama mtu ana kisukari. Vipande vya karatasi maalum vya kupimia mkojo hubadili rangi kama kuna sukari kwenye mkojo. Pima mara baada ya mtu kukojoa. Mtu hahitajiki kujizuia kula au kunywa chochote kabla ya kipimo kufanyika.

Vipimo vya mkojo vinaweza kushindwa kubainisha uwepo wa kisukari katika baadhi ya sampuli kwa sababu kiwango cha sukari kinapaswa kupanda sana (10 mmol/l au 180 mg/dl) kabla ya sukari kuingia kwenye mkojo. Hivyo kama kipimo cha mkojo hakioneshi kisukari lakini kuna sababu nyingine ya kufikiria kuwa huenda kuna kisukari, fanya kipimo cha damu.Ukurasa huu ulihuishwa: 20 Mei 2017