Hesperian Health Guides

Ubakaji

Katika sura hii:

Ngono ya kulazimisha, ngono ambayo haihitajiki au siyo ya kuridhia, ni ubakaji. Wanawake na wasichana wanaweza kubakwa na watu wanaowafamu, wapita njia, wanafamilia, au waume zao au marafiki wa kiume. Wanaume na wavulana nao wanaweza kubakwa. Kwa taarifa zaidi juu ya ubakaji, angalia sura juu ya Vurugu (inaandaliwa).

Mtu ambaye amebakwa atahitaji huduma ya kwanza kwa ajili ya majeraha ya kimwili. Pia atahitaji msaada wa kisaikilojia na huduma mbalimbali. Mhudumie kwa huruma na uelewa wa hali yake. Usimlaumu.

NWTND fa Page 36-1.png

Ubakaji unaweza kusababisha mimba. Dozi kubwa ya vidonge vya majira inaweza kuzuia mimba. Angalia Uzazi wa mpango. Ubakaji pia unaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa ya ngono. Angalia Maambukizi sehemu za ukeni au umeni na matatizo mengine (kinaandaliwa). Ili kuzuia maambukizi ya VVU baada ya ubakaji, angalia VVU na UKIMWI (kinaandaliwa).

Inaweza kuwa vigumu kwa mtu aliyebakwa kukurusu kumuangalia au kumgusa. Elezea utakachofanya katika kumchunguza na kutoa matibabu na omba ruksa yake kabla ya kumgusa.

Kama via vyake vya uzazi vina michaniko au michubuko, vinaweza kutoa maumivu. Mpe asetaminofeni au ibuprofeni. Kama kuna damu nyingi inatoka kwenye njia ya haja kubwa au ukeni, tumia mgandamizo kusimamisha uvujaji damu. Mfundishe jinsi ya kuizuia mwenyewe, kama damu itaendelea kutoka tena baadaye.

Kwa ajili ya mikwaruzo na michubuko midogo, loweka via vya uzazi kwenye maji ya vuguvugu mara 3 kila siku. Kumwaga maji juu ya via vya uzazi wakati wa kukojoa husaidia kupunguza hisia za mwako au kuungua. Michaniko mikubwa inaweza kuhitaji kushonwa.

Taarifa ya kitabibu ambayo inajumuisha mchoro wa mtu ukiwa na alama za majeraha.
Weka alama juu ya majeraha yote utakayoyagundua na piga picha kama ataruhusu. Hii itakusaidia katika ufuatiliaji kuhakikisha kuwa anapona. Inaweza pia kutumika kama kielelezo iwapo ataamua kwenda polisi.

Chunguza iwapo kuna majeraha sehemu zingine za mwili pia. Angalia sehemu zingine za sura hii jinsi ya kutibu matatizo mahsusi. Kutunza kumbukumbu au taarifa za uchunguzi wa kimwili na majeraha ni muhimu kama mwanamke atatoa taarifa juu ya tukio polisi—hata kama atakwenda kutoa taarifa baadaye sana.

Mfuatilie mwanamke huyu baada ya siku chache kujua anaendeleaje kisaikolojia na kimwili. Chunguza michaniko na michubuko kwa ajili ya dalili za maambukizi. Maambukizi ya kibofu (angalia Matatizo katika kukojoa — kinaandaliwa) hujitokeza sana baada ya ngono ya kulazimisha au isiyoridhiwa.