Hesperian Health Guides

Mifupa iliyovunjika, kutenguka, na misuli au tishu zilizoumia

Katika sura hii:

Kwanza amua kama mfupa umevunjika au kutenguka (kutoka kwenye nafasi yake ya kawaida), au kama misuli au tishu imeumia aidha kwa kuchanika, kujisokota au kwa njia nyingine. Inaweza kuwa vigumu kutofautisha majeraha haya, na huduma ya eksrei huenda ikahitajika kujua kwa hakika. Kama huwezi kujua iwapo mfupa umevunjika, umetenguka au msuli au tishu kuumia, iweke sehemu hiyo ya mwili katika nafasi moja bila kutikiswa na tafuta msaada. Pia inawezekana kupata majeraha yote haya kwa wakati mmoja.

Mpe dawa ya kupunguza maumivu kama vile asetamonofeni (acetaminophen) au ibuprofeni kusaidia na maumivu.

Mkono umevunjika.
Umevunjika

Sehemu iliyovimba katikati kwenye mfupa au maumivu yakiwa sehemu moja kwenye mfupa,na maumivu kidogo au hakuna maumivu kabisa mkono unapobaki katika nafasi moja bila kutikiswa. Wakati mwingine mfupa unaweza kuwa umevunjika hata bila kuwepo sehemu iliyovimba. Picha ya eksrei itaonyesha kwa uhakika kama kuna sehemu iliyovunjika.
Bega lililotenguka.
Umetenguka

Umetengukia kwenye kiungio au haiwezekani kutembeza kiungio hicho.
sehemu ya mkono kuelekea kwenye kiganja imevimba.
Msuli au tishu kuumia

Uvimbe na maumivu karibu na kiungio.

Mifupa iliyovunjika

Usitikise mfupa uliovunjika hadi mtu mwenye uzoefu wa kunyoosha mifupa atakapourudisha katika nafasi yake na kuufunga kwenye plasta ngumu au piopi. Ili kusaidia ubaki sehemu moja bila kutikisika, tengeneza banzi kutoka kwenye kadibodi (karatasi ngumu iliyokunjwa), kipande chepesi cha ubao bapa,au kitu kingine kigumu kilichonyooka.

Tengeneza banzi

Hatua 1:
Weka mkono katika nafasi yake ya asili ya kupumzika. Kiwiko kinapaswa kuwa kimepinda kidogo.
NWTND fa Page 29-1.png
Hatua 2:
Zungushia bandeji, shashi, kitambaa chepesi au tumia mkono wa shati.
NWTND fa Page 29-2.png
Hatua 3:
Pumzisha mkono kwenye kibanzi. Weka kitambaa kichoviringishwa ndani ya kiganja. Kama jeraha liko kwenye mguu, banzi lifungwe pembeni.
NWTND fa Page 29-3.png
Hatua 4:
Zungushia bandeji au kitambaa kwenye banzi ili libaki kwenye nafasi inayohitajika.
NWTND fa Page 29-4.png

Vidole vya mikono au miguu visifunikwe na angalia mara kwa mara kama vinapata joto la kawaida na vipo katika hali ya kawaida.

NWTND fa Page 29-5.png
NWTND fa Page 29-6.png
Funga kidole cha mguu au mkono kwenye kidole kinachofuatia. Weka padi au kitambaa laini kati ya vidole hivyo.
Funga banzi kwenye mfupa wa paja uliovunjika kuanzia kwenye nyonga hadi chini kwenye kifundo.

Tangeneza tanzi

Unaweza kutumia tanzi kulinda na kuusaidia mkono au bega lililojeruhiwa.

Kunja kipande cha kitambaa cha pembe nne kupata pembe tatu; weka mkono kwenye mkunjo wa kitambaa.
Saidia kukinua kiwiko.
Funga kitambaa nyuma ya shingo.

Weka mfupa vizuri kwa ajili ya uungaji

Subiri hadi uvimbe uondoke ndiyo uweke mfupa vizuri kwa ajili ya uungaji.

Kama mfupa umetoka nje ya nafasi yake ya kawaida, kuurudisha husaidia uponyaji. Lakini kama hujui jinsi ya kuurudisha mfupa katika nafasi yake kwa usahihi, unaweza kusababisha uharibifu mkubwa kwa kufanya isivyostahili. Kama inawezekana, mtu mwenye uzoefu ndiyo aifanye kazi hiyo. Jamii nyingi zina watu wenye uzoefu wa kuunga mifupa au wafanyakazi wa afya wenye uwezo wa kuifanya kazi hii vizuri.

Hatua 1:
Kwanza mpe dawa ya kupunguza maumivu. Unaweza pia kumpa dawa ya kusaidia kupunguza mfadhaiko na kutuliza kama vile lorazipamu (lorazepam) au diazipamu (diazepam).

Hatua 2:
Muombe mtu akusaidie kushikilia sehemu iliyojeruhiwa karibu na mwili ili isitikisike au funga kwenye kitu kingine ambacho hakitikisiki.

Mkono uliovunjika ukivutwa.

Hatua 3:
Vuta upande ulio mbali lakini taratibu na kwa mkazo. Usivute kwa nguvu ghafla, lakini vuta kwa mkazo wa kutosha kutenganisha mifupa.

Mifupa ikiwekwa vizuri kwa ajili ya uungaji.

Hatua 4:
Vipande vya mfupa vinapoachana, taratibu nyoosha ncha zake na kuruhusu ziunganike tena.

Usijaribu kuunganisha mfupa kama mvunjiko unaonekana kwenda hadi kwenye kiungio (jointi) au kama kuna zaidi ya mvunjiko mmoja, ukiacha kipande cha mfupa ‘kikielea’ katikati. Usitumie nguvu kuuweka mfupa katika nafasi kwa ajili ya uungaji. Hii inaweza kusababisha uharibifu wa kudumu. Tafuta msaada.

Tengeneza umbo kwa ajili ya kufunga sehemu ya mwili iliyovunjika

Maumbo haya yanaweza kutengenezwa kutokana na vipande vya nguo na sirapu, au plasta ambayo inapochanganywa na maji na kukauka huwa ngumu na imara.

Nchini Mexico, mimea tofauti kadhaa kama vile tepeguaje (kutokana na asili ya maharagwe), solda con solda (mmea mkubwa unaopanda na kutanda mitini) hutumika kutengeneza maumbo hayo. Nchini India, waganga wa jadi wa mifupa hutengeneza maumbo haya kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu nyeupe ya yai na mitidawa. Lakini kwa ujumla njia za utengenezaji hufanana. Mmea wowote ule utafaa kama unaweza kutumika kutengeneza sirapu ambayo itakauka na kuwa ngumu na imara, na haitasababisha mwasho. Kawaida mmea huchemshwa kwenye maji hadi unapoanza kutoa sirapu nzito. Au tumia plasta ngumu au piopi POP (Plaster of Paris) ikichanganywa na maji.

Subiri hadi uvimbe utoweke kabla ya kufunga piopi. Hii inaweza kuchukua hadi wiki moja. Wakati unasubiria, saidia kukishikilia kiungo kilichojeruhiwa katika nafasi moja kwa kutumia banzi na tanzi.

Hatua 1:
Hakikisha mifupa imefungamana vizuri. Linganisha upande uliojeruhiwa na upande ambao haukujeruhiwa kuhakikisha kuwa pande zote zinaonekana sawa na ukizigusa zinafanana.

Hatua 2:
Kiweke kiungo katika nafasi inayofaa:

Kiwiko kimepinda, kidole kiko juu, na vidole vimekunjwa kidogo-kama vile vinashika glasi. NWTND fa Page 31-1.png Goti limepinda kidogo. Kifundo kimepinda kama vile mtu anasimama. NWTND fa Page 31-2.png

Hatua 3:
Zungushia sehemu itakayofungwa piopi kwenye safu ya kitambaa chepesi, au safu kadhaa za shashi. Anza kutengeneza umbo la piopi kwenye eneo ambalo linajumwisha kiungio, juu na chini ya mvunjiko.

Hatua 4:
Baada ya hapo funika umbo kwenye pamba nyepesi. Ongeza safu za ziada maeneo yenye mifupa, lakini usizidishe, hasa kwenye mvunjiko.

Hatua 5:
Chovya vipande vya fulana, kitambaa au bandeji kwenye sirapu au mchanganyiko wa plasta.

NWTND fa Page 31-3.png

Hatua 6:
Tumia vipande hivyo vya vitambaa kuzungushia eneo hilo kwa safu kadhaa na kutengeneza umbo. Usifunike vidole vya mikono au miguu. Umbo au piopi lishike vizuri lakini siyo kubana sana na kumuumiza majeruhi.

NWTND fa Page 31-4.png Kufunga tabaka la ndani juu ya umbo.

Step 7:
Lainisha tabaka la ndani juu ya umbo kama hivi:

Baada ya kufunga umbo hilo au piopi, pumzisha kiungo na kukiinua pale itakapowezekana. Kama ni mguu uliovunjika, tumia magongo kuepuka kuweka uzito wowote juu ya mguu huo.

Kama, wakati wowote baada ya kufunga piopi vidole vya miguu au mikono vitaanza kuvimba, kuuma, kugeuka kuwa vyekundu, vyeupe au kupauka, au bluu, au kupoteza hisia, ondoa umbo mara moja. Kushindwa kuondoa piopi ambalo limekaza sana kunaweza kusababisha mtu kupoteza kiungo hicho.

Je mfupa uliovunjika huchukua muda gani kupona? Mfupa wa mtoto mdogo huchukua wiki kadhaa kupona. Mfupa wa mtu mzima huchukua miezi na pia unaweza kutopona vizuri. Piopi ibaki kwenye mkono angalau kwa mwezi mmoja. Piopi kwenye mguu inapaswa kuvaliwa angalau kwa miezi 2.

Ili kuliondoa piopi, loweka kwenye maji kulainisha na kata taratibu. Baada ya kuliondoa piopi, kuwa mwangalifu na mtaratibu na mkono au mguu uliovunjika angalau kwa muda unaolingana na ule uliotumia kulivaa piopi. Anza kazi za kawaida polepole, kama vile kuweka uzito juu ya mguu uliojeruhiwa.

Mfupa ambao umevunjika na kujitokeza nje ya ngozi ya mwili


NWTND fa Page 32-1.png

Mifupa ambayo imevunjika na kuwa wazi inakabiliwa na hatari kubwa ya kupata maambukizi. Safisha kidonda vizuri na maji mengi yanayotiririka kwa dakika 5 au zaidi. Funga banzi kwenye mguu, mpe seftriaksoni (ceftriaxone), kloksasilini (cloxacillin), klindamaisini (clindamycin), AU sefaleksini (cephalexin) na tafuta msaada.

Kama huwezi kupata msaada haraka, safisha kidonda vizuri na kukifunga kwenye shashi iliyotiwa dawa ya kuua vijidudu. Badilisha shashi mara kwa mara. Kama hakuna dalili ya maambukizi ndani ya siku 3, weka mfupa vizuri kwa ajili ya uungaji, funika kidonda, na tengeneza piopi.

Kutenguka mfupa (mfupa kutoka kwenye kiungio)

NWTND fa Page 32-2.png

Rudisha mfupa uliotenguka kwenye nafasi yake mapema iwezekanavyo. Kadri utakavyoendelea kusubiri ndivyo itazidi kuwa vigumu kuurudisha na pia utatoa maumivu makubwa zaidi.

Njia ya kawaida ni kuuvuta mfupa taratibu na polepole kutoka kwenye kiungio, na kuuwezesha kudumbukia kwa usahihi kwenye nafasi yake. Mpe majeruhi dawa ya kupunguza mfadhaiko kama vile diazipamu, na dawa za kawaida za kupunguza maumivu kama vile ibuprofeni nusu saa kabla hujajaribu kuurudisha mfupa katika nafasi yake. Kama huwezi kuurudisha mfupa kwenye kiungio, tafuta msaada.

Baada ya kuurudisha mfupa uliotenguka, ukae kwenye nafasi hiyo bila kutikisika kwa wiki 2 au 3 kwa kuushikilia na tanzi au kitambaa. Tumia dawa ya kupunguza maumivu kama vile ibuprofeni kadri itakavyohitajika. Mara baada ya maumivu kupungua kiasi cha kutosha na kuruhusu kuutembeza, ondoa kiungio kilichojeruhiwa nje ya tanzi au kitambaa kila baada ya saa chache na taratibu kufanya mazoezi ya kukunja, kukunjua, na kuuzungusha. Kwa ajili ya bega, shusha mkono chini na kuuruhusu kutembezwa mbele na nyuma na katika miduara midogo. Anza majaribio polepole kukitumia kiungio kichojeruhiwa kwa miezi 2 au 3 inayofuatia. Jeraha la kutenguka huchukua muda mrefu kupona.

Kama kuna maumivu makali baada ya kurekebisha kiungio kilichotenguka, huenda kuna mfupa uliovunjika.


Kiwiko kilichotenguka

Vuta sehemu ya juu ya mkono kwa nguvu kuelekea chini. Au mgonjwa ashike ndoo yenye kilo 5 au 7 za maji kwa dakika 15 hadi 20. Uzito huo utavuta mkono chini na kiwiko kitapaswa kurudi katika nafasi yake.

Mwanaume amelala mezani mwenzake akisaidia kuvuta chini mkono wake.
Sukuma kwenye mifupa nyuma ya kiwiko (skapula.)
Kama kiwiko hakitarudi kwenye nafasi yake, taratibu sukuma kwenye ncha ya skapula na vidole vyako. Mkono unapaswa kurudi kwenye nafasi yake.
AU

Taratibu zungusha mkono uliyojeruhiwa kuelekea kwako kama hivi. Ni bora zaidi kuwa na msaidizi akishika mwili wa mgonjwa ili mkono tu ndiyo uweze kuzungushwa.
Mwanaume amelalia mgongo wakati mwenzake akizungusha mkono wake.
Tanzi au bandeji zikiushikilia mkono ili kusaidia kiwiko kibaki katika nafasi yake.

Baada ya hapo funga mkono kwenye tanzi au bandeji kama hivi kuushikilia mkono na kuzuia usitoke kwenye kiungio:


Kiwiko kilichotenguka


Hatua 1:
Mlaze mgonjwa chini halafu nyoosha mkono wake mzima ili kuiweka mifupa kwenye msitari mmoja.
Hatua 2:
Pata msaidizi kukamata kwa nguvu sehemu ya juu ya mkono. Vuta sehemu ya mkono ya mbele kuelekea kwako,na taratibu kupinda kiwiko.
NWTND fa Page 34-1.png
Hatua 3:
Sasa sukuma chini sehemu ya juu ya mkono katika msitari ukiwa umepinda kiwiko. Unapaswa kusikia sauti kama ya mgongano wa vitu viwili. Funga kiwiko kwenye banzi na tanzi kuushikilia ili kuzuia kiwiko kisichomoke tena kutoka kwenye kiungio.
NWTND fa Page 34-2.png

Mkono ambao umefungwa kwenye banzi kuanzia kifundo hadi kiwiko na kushikiliwa na tanzi.
MUHIMU! Kama kuna ukinzani, acha! Unaweza kuuvunja mfupa. Ning’iniza kiwiko hivi na kutafuta msaada zaidi.

Kidole kilichotenguka

Kwa nguvu vuta kidole kilichotenguka kuelekea nje, na baada ya hapo sukuma shina la kidole hicho kwenye nafasi yake ili kukifungamanisha.

NWTND fa Page 34-4.png
Funga kidole kilichotenguka kwa kidole jirani.

Majeraha yanayotokana na tishu au kiungo chini ya ngozi kuumia (kujisokota au kuchanika)

NWTND fa Page 35-1.png
Dalili
  • Kuvimba
  • Maumivu
  • Vilio la damu au wekundu
Matibabu
  • Pumzika: usiweke uzito juu ya sehemu iliyojeruhiwa. Tumia tanzi au magongo kwa wiki 3 hadi 4.
  • Weka barafu: kwa takriban dakika 30 kila ya saa 2 hadi 4. Weka mara chache baada ya siku kadhaa.
  • Bana: Funga vizuri kwa kutumia bandeji.
  • Inua juu: inua kiungo husika juu ya mto au blanketi kadhaa zilizokunjwa muda wote siku za mwanzo, na kwa saa chache baada ya siku chache.


Hatua hizi zitapunguza maumivu na uvimbe. Kama zitafanyika tangu mwanzo na kwa mpangilio, zinaweza kusaidia sehemu iliyojeruhiwa kupona haraka na matatizo machache ya muda mrefu.

Usiweke mgandamizo au uzito juu ya jeraha. Kawaida majeraha ya msuli au kiungo chini ya ngozi (kujisokota au kuchanika) huchukua wiki 1 hadi 2 kupona.

Jinsi ya kufunga bandeji

Kufunga bandeji juu ya kikanyagio na kifundo cha mguu.
Anzia karibu na vidole vya miguu au mikono.
Funga vizuri lakini usikaze sana. Vidole vya mguu au mkono vinapaswa kuwa na joto na pia hisia za kawaida.