Hesperian Health Guides

Kuumwa au kung'atwa na wadudu au viumbe wengine

Katika sura hii:

NWTND fa Page 51-1.png

Usitoboe au kuchana wazi sehemu ulioumwa au kung’atwa au kujaribu kufyonza nje sumu. Pia, toniketi (bandeji au mpira unaofungwa sehemu Fulani ya mwili kudhibiti mzunguko wa damu) hazitasaidia kuzuia sumu kusambaa, lakini zitasababisha madhara mabaya zaidi.

Matukio mengi ya kuumwa au kung’atwa na viumbe husababisha maumivu lakini siyo hatari, na hata viumbe hatari kawaida haviachii sumu ya kutosha kuua binadamu. Kuwa mtulivu na tazama sehemu iliyojeruhiwa. Kama hakuna matatizo au matatizo yenyewe yanapungua baada ya saa chache (kutegemea na kiumbe) hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi. Kwa watoto wadogo,hasa kutokana na umri wao, sumu inaweza kuwaathiri na kusababisha madhara makubwa zaidi. Hivyo wanahitaji msaada zaidi na wa haraka.

Kung’atwa na nyoka

  1. Jiondoe kwenye nyoka. Baadhi ya nyoka wanaweza kung’ata ndani ya dakika chache hata baada ya kufa.
  2. Ondoa vito au nguo zote karibu na jeraha kwa sababu mwili unaweza kuvimba.
  3. Weka sehemu ya jeraha chini ya usawa wa moyo. Halafu tuliza sehemu ya jeraha kwa kufunga kitambaa cha kuishikilia sehemu yenye jeraha au ubao ili kupunguza kutikisika. Kutumia misuli au kuitembeza huchangia sumu kusambaa.
  4. Polepole safisha kidonda. Usipanguse.
  5. Kwa aina nyingi za nyoka, au kama hujui alikuwa nyoka wa aina gani, angalia na kusubiri kwa dakika chache. Kama kuna uvimbe mdogo au hakuna uvimbe wowote, maumivu, au wekundu, hakuna tatizo. Dalili za hatari zinajumwisha kuvimba sana au maumivu makali, kusikia kichwa kizito sawa na mtu anayetoka usingizini, vigubiko vya macho kuinama, kizunguzungu, udhaifu, kichefuchefu, au kutokwa damu puani au mdomoni.

Mwambie majeruhi kusukutua maji mdomoni na kutema kwenye bakuli jeupe au lenye uwezo wa kuonesha rangi halisi ya maji yatakayotoka mdomoni. Kama maji yaliyotemwa yataonekana pinki au yenye damudamu, ni dalili kwamba fizi zimeanza kutoa damu. Hii ni dalili ya hatari.

Kwa aina ya nyoka wafuatao, funga eneo la jeraha na kukaza:

NWTND fa Page 52-1.png
  • Nyoka waishio kwenye mawe na matumbawe(coral snakes)
  • Hongo (mamba)
  • Nyoka wengi wenye asili ya Amerika ya Kusini
  • Nyoka wa kwenye maji (sea snakes)
  • Aina nyingi za Kobra – zenye sumu zinazoathiri mwili mzima.
NWTND fa Page 52-2.png
Funga kwa kukaza — kusimamisha sumu kusambaa, lakini siyo kukaza sana ambako kunaweza kuzuia damu kutembea.Jaribu kuhisi mapigo ya moyo chini ya bandeji uliyofunga juu ya sehemu ya jeraha.
Tumia ubao kusaidia kiungo kisitikisike.
NWTND fa Page 52-3.png

Aina nyingi za nyoka wenye sumu kali wakiwemo viper na baadhi ya Kobra hudhuru tu mahali wanapouma lakini hawasababishi matatizo kwenye mwili mzima. Kwa nyoka hao, usifunge na kufunika jeraha.

Kwa nyoka wengi wenye sumu, kuna dawa ambazo zinaweza kusaidia kudhibiti sumu. Kama utapata msaada wa kitabibu, elezea kadri uwezavyo ni nyoka wa aina gani ili dawa sahihi ya kudhibiti sumu ya nyoka iweze kutumika. Kama inawezekana hakikisha una dawa ya sumu ya aina za nyoka wanaopatikana sana eneo lako katika sanduku lako la akiba ya dawa kabla dharura kama hizo hazijatokea.


NWTND fa Page 52-4.png

Kwa ajili ya Kobra mwenye asili ya kutema sumu: tiririsha maji mengi machoni. Kama huna maji au maziwa bia inaweza kutumika. Usitumie kemikali zinazowasha sana.

Chatu huwa hawana sumu, lakini wanapong’ata wanaweza kusababisha maambukizi makali ya ngozi. Chunguza kidonda na kama kuna dalili ya maambukizi— wekundu kuongezeka, joto kuongezeka, kuvimba, au usaha, toa matibabu yanayostahili kwa kidonda ambacho kimepata maambukizi. Mara chache nyoka hao husababisha majeraha kwa kujiviringisha juu ya mwili wa mtu na kumkamua.

Kama eneo la jeraha linaonesha meno ya nyoka yalipoingilia, basi nyoka huyu ana sumu. Kama hakuna alama za meno ya nyoka, kuna uwezekano mdogo kwamba nyoka huyu ana sumu, lakini anaweza kuwa na sumu.

NWTND fa Page 53-1.png

Buibui na ng’e

NWTND fa Page 53-2.png

Ingawa wanaweza kusababisha maumivu makali, matukio mengi ya kuumwa na buibui na ng’e hayasababishi madhara makubwa au madhara ya muda mrefu. Usiitikise sehemu iliyoumia na tumia barafu au maji baridi kupunguza maumivu.Usikate au kuchana wazi sehemu ya jeraha au kufunga sehemu hiyo kwa kutumia toniketi au bandeji. Joto halisaidii, lakini kutoitikisa sehemu ya jeraha husaidia.

Kama unajua kuwa aina ya buibui au ng’e aliyemuuma ni hatari, au kama baada ya kuuma kuna dalili za matatizo kama vile maumivu ya tumbo, mwasho, kutokwa jasho, na shida katika kupumua, basi tafuta msaada wa kitabibu. Huenda kukawa na dawa dhidi ya sumu hiyo.

Kwa ajili ya matukio ya kunga’twa na buibui na ng’e hatari, unaweza kumpa majeruhi diazipamu kuzuia misuli kukakamaa na pia kumtuliza mgonjwa wakati mnafanya maandalizi ya kwenda hospitali au kituo cha afya.

Nyuki na nyigu

Baada ya kuumwa na nyuki, angalia kama mwiba wake umebaki kwenye ngozi na kuuondoa haraka iwezekanavyo. Eneo inayozunguka sehemu ya jeraha inaweza kuwa na wekundu, kuvimba na kutoa maumivu. Kuweka mgando wa amira na maji, au kitu kingine baridi kwenye eneo husika, kutasaidia kudhibiti uvimbe na maumivu.

Mzio mkali kuhusiana na matukio ya kuumwa na nyuki au nyigu ni nadra, lakini unaweza kuhatarisha maisha. Angalia Taarifa juu ya dalili na matibabu ya mzio mkali.

Kupe

Kupe wanaweza kusambaza maambukizi mengi hatari iwapo watakuuma. Kwa taarifa zaidi juu ya kupe na jinsi ya kuwaondoa, angalia Sura juu ya Ngozi(inaandaliwa).

NWTND fa Page 53-3.png

Samaki na Yavuyavu (jelly fish)

Jinasue kutoka kwa yavuyavu na kwangua miguu yake ambayo inaweza kuwa imekung’ang’ania. Tumia maji ya bahari kunawa sehemu hiyo. Kwa samaki wanaochoma na miba yao, ondoa miba yote iliyobaki kwenye ngozi kwa kutumia kibanio.

Ingiza sehemu iliyoumia kwenye maji ya moto kwa dakika 20 kupunguza maumivu, lakini hakikisha kuwa hayaunguzi. Hii inaweza kusaidia zaidi kutuliza majeraha kutokana na samaki wanaochoma kuliko yavuyavu.

Kuna tiba nyingi za asili lakini siyo zote hufanya kazi dhidi ya madhara ya aina zote za samaki au yavuyavu. Kwa mfano, mashambulizi ya samaki wengine yanaweza kutulizwa kwa kuosha na siki (vinegar). Lakini siki huzidisha madhara ya mashambulio ya aina zingine za yavuyavu. Papai au vilainisha nyama ni vitulizo muhimu v ya maumivu kutokana na mashambulizi ya yavuyavu,. Papai au vilainisha nyama ni vitulizo muhimu vya maumivu kutokana na mashambulizi ya yavuyavu, lakini siyo kwa aina zote za yavuyavu na wakati mwingine vinaweza kuzidisha maumivu.

Mhimize atumie na kutembeza viungo vyake —tofauti na matukio ya kung’atwa na nyoka au buibui, kutuliza kiungo bila mtikisiko hakusaidii. Tafuta msaada wa kitabibu kama kutakuwa na matatizo ya kupumua au iwapo dalili zitazidi kuwa mbaya.