Hesperian Health Guides

Uzazi wa mpango wa dharura (vidonge vya dharura vya kuzuia mimba)

Uzazi wa mpango: Kutumia vidonge vya majira

Unaweza kutumia vidonge vya dharura vya kuzuia mimba au baadhi ya vidonge vya kawaida vya majira kuzuia mimba ndani ya siku 5 baada ya kufanya ngono bila kutumia kinga. Idadi ya vidonge ambayo unahitaji hutegemea aina ya homoni na kiwango cha homoni katika kila kidonge. Chati hii imeorodhesha aina chache tu za vidonge hivi. Hakikisha unajua aina na kiwango cha homoni katika vidonge kabla hujavitumia. Chati inaonesha jumla dozi kamili ya homoni ambazo zinahitajika na vidonge vingapi unahitaji kutimiza dozi hiyo.

Madhara ya pembeni ya kawaida ya vidonge vya dharura vya kuzuia mimba ni maumivu ya kichwa, kichefuchefu au maumivu tumboni, lakini yote haya hutoweka ndani ya siku moja au mbili. Ni kawaida kutokwa na damu kidogo au kutokea mabadiliko katika siku zako za hedhi mwezi unaofuata. Unapotumia vidonge vya dharura vya kuzuia mimba, vidonge ambavyo ni maalum kwa dharura au dozi sahihi ya vidonge vya projestini tu husababisha madhara ya pembeni kidogo kuliko kutumia vidonge mseto vya majira. Kama utatapika ndani ya saa moja ya kutumia dozi hii, hii inamaanisha kwamba unapaswa kurudia dozi ile uliotumia. Kamwe usichanganye aina tofauti za vidonge vya dharura vya kuzuia mimba au vidonge vingine vya majira kwa sababu vinaweza kushindwa kabisa kufanya kazi.

Jinsi ya kutumia vidonge vya dharura vya uzazi wa mpango

JINSI YA KUTUMIA VIDONGE MAALUM KWA AJILI YA KUZUIA MIMBA KATIKA HALI YA DHARURA
Vidonge vya dharura vyenye miligramu 1.5 (makrogramu 1500 za levonorgestrel (NorLevo 1.5, Plan B One-Step, Postinor-1)
Dozi kamili ya kidonge 1 = miligramu 1.5 (makrogramu 1500) za levonorgestrel
Tumia kidonge 1, mara moja tu
Vidonge vya dharura vyenye miligramu 30 za ulipristal acetate (ella, ellaOne)
Dozi kamili ya kidonge 1 =miligramu 30 za ulipristal acetate
Tumia kidonge 1 , mara moja tu
Vidonge vya dharura vyenye miligramu 0.75 (makrogramu 750) za levonorgestrel (NorLevo 0.75, Optinor, Postinor, Postinor-2, Plan B)
Dozi kamili ya vidonge 2 = miligramu 1.5 (makrogramu 1500) za levonorgestrel
Tumia vidonge 2 , mara moja tu
Vidonge vya dharura vyenye miligramu 0.05 (makrogramu 50) za ethinyl estradiol na miligramu 0.25 (makrogramu 250 ) levonorgestrel (Tetragynon, Neogynon, Nordiol)
Dozi kamili ya vidonge 4 =miligramu 0.2 (makrogramu 200 za ethinyl estradiol na miligramu 1.0 (makrogramu 1000) za levonorgestrel
Anza kwa kutumia vidonge 2 Halafu tumia vidonge 2 zaidi baada ya saa 12


JINSI YA KUTUMIA VIDONGE VYA MAJIRA MSETO KWA AJILI YA KUZUIA MIMBA KATIKA HALI YA DHARURA
Kwa paketi ya siku 28 yenye vidonge mseto 28, tumia kidonge kutoka vidonge vya kwanza 21 ili kupata dozi iliyooneshwa hapo chini lakini usitumie vidonge vya mwisho 7 kwa sababu huenda vikawa havina homoni – ni kwa ajili ya kukumbusha kumeza kidonge kila siku.
Vidonge vya majira mseto vikiwa na miligramu 0.03 (makrogramu 30) za ethinyl estradiol na miligramu 0.15 (makrogramu 150) za levonorgestrel (Anna, Combination 3, Gestrelan, Microgynon, Microgynon-30, Nordette, Roselle)
Dozi kamili ni vidonge 8 =miligramu 0.24 (makrogramu 240) za ethinyl estradiol na miligramu 1.2 (makrogramu 1200) za levonorgestrel
Anza na vidonge4 Halafu tumia vidonge 4 zaidi baada ya saa 12
Vidonge mseto vikiwa na miligramu 0.03 (makrogramu 30) za ethinyl estradiol na miligramu 0.3 (makrogramu 300) za norgestrel (Lo-Femenal, 5Lo/Ovral)
Dozi kamili ya vidonge 8 = miligramu 0.24 (makrogramu 240) za ethinyl estradiol na miligramu 2.4 (makrogramu 2400) za norgestrel
Anza na vidonge 4 Halafu tumia vidonge 4 zaidi baada ya saa 12
Vidonge vya majira mseto vyenye miligramu 0.02 (makrogramu 20) za ethinyl estradiol na miligramu 0.1 (makrogramu 100) za levonorgestrel (Alesse, Loette, Lutera, Miranova)
Dozi kamili ni vidonge 10 = miligramu 0.2 (makrogramu 200 ) za ethinyl estradiol na miligramu 1 (makrogramu 1000) za levonorgestrel
Anza na vidonge 5 Halafu tumia vidonge 5 zaidi baada ya saa 12


JINSI YA KUTUMIA VIDONGE VYENYE PROJESTINI TU (VIDONGE VIDOGO) KWA AJILI YA KUZUIA MIMBA KATIKA HALI YA DHARURA
Katika paketi ya vidonge vyenye projestini tu, kila kidonge kina kiwango sawa cha dozi ya homoni.
Vidonge vya projestini tu (vidonge vidogo) vyenye miligramu 0.075 (makrogramu 75) za norgestrel (Ovrette, Minicon)
Dozi kamili vidonge 40 = miligramu 3 (makrogramu 3000 za norgestrel)
Tumia vidonge 40 mara moja tu (ni vidonge vingi lakini salama)
Vidonge vyenye projestini tu (vidonge vidogo) vikiwa na miligramu 0.0375 (makrogramu 37.5) za levonorgestrel (Neogest, Norgeal)
Dozi kamili ni vidonge 40 =miligramu 1.5 (makrogramu 1500 za levonorgestrel
Tumia vidonge 40 mara moja tu (vidonge vingi lakini salama)
Vidonge vyenye projestini tu (vidonge vidogo) vikiwa na miligramu 0.03 (makrogramu 30) za levonorgestrel (Microlut, Microval, Nortrel)
Dozi kamili ya vidonge 50 = miligramu 1.5 (makrogramu 1500) za levonorgestrel
Tumia vidonge 50 mara moja tu (vidonge vingi lakini salama)