Hesperian Health Guides

Tetanasi (pepopunda)

Katika sura hii:

Tetanasi ni ambukizo hatari ambalo huingia kwenye kidonda au kiungamwana, na baadae kusambaa mwili mzima.

Mgonjwa akiwa amelala chini, mgongo wake ukiwa umejipinda na akiwa amekunja ngumi.
Dalili za tetanasi zinaweza kuanza siku moja au wiki kadhaa baada ya kujeruhiwa.
Dalili
  • Kutokwa na jasho kusiko kwa kawaida.
  • Mapigo ya moyo kwenda haraka.
  • Misuli kukakamaa na kuuma.
  • Wakati wa mikakamao ya misuli, upumuaji unaweza kusimama.
  • Kukaza au kubana kwa misuli unaokuja na kuachia.
  • Mdomo hauwezi kufunguka kwa urahisi.
  • Shingo kukakamaa, tumbo kukaza kama ubao.


Tafuta msaada wa kitabibu haraka kwa ajili ya dalili hizi!

Uzuiaji

Ni rahisi kuzuia tetanasi kuliko kuitibu. Njia bora zaidi ni chanjo na matunzo mazuri ya kidonda. Kwa ajili ya ratiba ya chanjo, angalia Chanjo (kinaandaliwa).

Vidonda ambavyo ni rahisi kuambukizwa na tetanasi

  • Vidonda ambavyo vinatokana na kutobolewa na vitu vikali.
  • Vidonda vya risasi.
  • Mifupa iliyovunjika, hasa inapojitokeza nje ya ngozi.
Mguu wenye jeraha la mfupa uliovunjika, sehemu ya mfupa ikiwa imejitokeza nje.
  • Vidonda vikubwa vya moto au kutokana na ugonjwa wa kuganda tishu kutokana na barafu.
  • Utoaji mimba kwa njia zisizo salama na kuchoma sindano au utoboaji, au kuchanja kwa kutumia sindano na vifaa ambavyo tayari vimetumika, na havijatakaswa.


Mtu akikanyaga msumari ambao umejitokeza kupitia kwenye ubao.
Msichana akijidunga sindano wakati akiongea na kijana mwingine.
Zamu yangu.
Sengenge.
Sindano ikitoboa sikio.


Safisha vidonda hivi vizuri na kutoa dawa dhidi ya tetanasi (antitetanus immunoglobulin) kama ratiba yake ya chanjo ya tetanasi iko nyuma. Pia mpe metronidazo (metronidazole).

Tetanasi miongoni mwa watoto wachanga

Watoto wachanga huambukizwa tetanasi kupitia kiungamwana au kitovu. Unaweza kumkinga mtoto mchanga kwa kukata kiungamwana kwa kutumia wembe uliochemshwa kwenye maji, kutunza usafi wa kitovu, na kumchanja mama mjamzito. Angalia Chanjo (kinaandaliwa).