Hesperian Health Guides

Kuvia damu kutokana na majeraha chini ya ngozi

Katika sura hii:

Kuvia damu humaanisha kuwa tishu chini ya ngozi imejeruhiwa na damu inavuja kutoka kwenye mishipa ya damu. Kuvia damu kunaweza kuwa na maumivu makali na kusababisha kero kwa majeruhi, lakini kawaida sio tatizo kubwa. Tibu tatizo la kuvia damu kama jinsi inavyotakiwa kutibu tatizo la majeraha ya tishu au kiungo chini ya ngozi (kutokana na kujisokota au au kuchanika): tibu kwa kupumzika vya kutosha, barafu, mgandamizo, na kuinua sehemu iliyojeruhiwa.

Kuvia damu kichwani au tumboni inaweza kuwa dalili ya tatizo kubwa zaidi. Angalia jinsi ya kufanya kama siku za karibuni mtu huyu alipata kipigo kikali kichwani au tumbo.

Kama utaona mtu anavilia damu mara kwa mara, au ana majeraha ya aina hiyo katika hatua tofauti za uponaji, hii inaweza kuwa dalili kuwa anafanyiwa mateso na ukatili. Angalia Vurugu (kinaandaliwa).