Hesperian Health Guides

Sura ya 15: Utoaji mimba na matatizo yanayotokana na utoaji mimba

HealthWiki > Pale ambapo Wanawake hawana Daktari > Sura ya 15: Utoaji mimba na matatizo yanayotokana na utoaji mimba

Katika sura hii:

Kama njia za uzazi wa mpango zitashindikana, angalau utoaji mimba kisheria ni njia salama kiasi kwa mwanamke
mwanamke akianguka kwenye ‘shuka’ lililotegwa maalum kumnusuru likiwa na maandishi 'utoaji mimba kisheria', ili asitumbukie kwenye shimo chini yake lenye maandishi 'utoaji mimba usiyo salama'

Ukosefu wa huduma za uzazi wa mpango na ukosefu wa taarifa sahihi juu ya ngono huchangia mimba zisizotakiwa na utoaji mimba.

Mwanamke anapofanya kitendo chochote kukatisha ujauzito ni utoaji mimba. Katika kitabu hiki, neno utoaji mimba linaelezea tu kitendo cha makusudi ambacho kimepangwa. Tukio la ujauzito kutoka au kukatishwa kwa bahati mbaya hujulikana kama mimba kuharibika (miscarriage).


Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Jan 2024