Hesperian Health Guides
Kwa nini baadhi ya wanawake hutoa mimba?
HealthWiki > Pale ambapo Wanawake hawana Daktari > Sura ya 15: Utoaji mimba na matatizo yanayotokana na utoaji mimba > Kwa nini baadhi ya wanawake hutoa mimba?
- Tayari anapokuwa na watoto ambao anaweza kuwahudumia.
- Ujauzito huo unapokuwa hatari kwa afya au maisha yake.
- Hana mwenzi wa kumsaidia kumhudumia mtoto atakayezaliwa.
- Anataka kwanza kumaliza shule.
- Hataki kupata watoto.
- Alipata mimba baada ya kubakwa.
- Kuna mtu ambaye anamlazimisha kuitoa mimba.
- Mtoto atazaliwa na matatizo makubwa ya kiafya au kimaumbile.
- Ana VVU au UKIMWI.
Njia za Uzazi wa Mpango wakati wa dharura |
---|
Mwanamke ambaye amefanya ngono pasipo kutumia kinga ndani ya siku 3 anaweza kuzuia kupata ujauzito kama atachukua hatua haraka. Angalia Njia za dharura za uzazi wa mpango.
Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Mei 2017